Nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania ni ipi, Kwanini Rais wa Zanzibar awe Msaidizi wa Rais Samia?

Nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania ni ipi, Kwanini Rais wa Zanzibar awe Msaidizi wa Rais Samia?

Kulikuwa hakuna haja kuanzisha cheo cha makamu wa Rais ingebaki tu kama awali makamu ni Rais wa Zanzibar na Waziri mkuu basi hata kama ingetokea Zanzibar inaongozwa na Rais kutoka chama tofauti.
Huko mbali sana na waziri mkuu msaidizi?
 
Ujio wa mfumo wa vyama vingi ulitukanganya...
Kwa itifaki za Muungano, Rais wa Zanzibar alipaswa kuwa ndiye Makamu/Makamo wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hisia zikaja kwamba, ikitokea kule Zanzibar kashinda mtu wa Chama fulani, itakuwaje? Katiba ikabadilishwa na Rais wa Zanzibar akawekwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Muungano; ili apate fursa ya kushiriki masuala ya Muungano. Sasa wengine huchukulia u-Rais wa SMZ kuwa sawa na u-Waziri wa Muungano..HII SI SAHIHI. Ukiwaweka pamoja viongozi wa juu wa JMT na SMZ, Rais wa Zanzibar ni No. 3; na si kwa majukumu, bali HADHI ya kulinda Muungano!
 
Screenshot_2024-09-03-01-26-28-1-1.png
 
Watanzania wanahitaji sana kufundishwa katiba yao, Rais wa Tanzania ni executive president na sio ceremonial leader, amepewa mamlaka inayoitwa presidential appointment ya kumteua mtu yeyote kumsaidia au kumwakilisha popote as long as ni Mtanzania and sometimes sio lazima awe Mtanzania!. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania ambao Watanzania wote wa pande zote wana haki sawa za Utanzania hivyo kiuraia Wanzanzibari wote wana haki sawa za Utanzania kama wabara, hivyo wana haki ya kuteuliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi popote ndani ya JMT na Rais wa JMT yuko huru kumteua mtu yoyote kumwakilisha popote katiba jambo lolote!.

Inapotokea Rais hayupo kabisa au hawezi kutekeleza majukumu yake ya urais kwa sababu yoyote ile ikiwemo kifo, then hierarchy ya Katiba ya JMT inafuatwa
No.1 ni Rais wa JMT
No.2 ni VP
No.3 ni PM
No.4 ni Spika
No. 5 ni CJ

Lakini inapotokea Rais yupo busy, anaweza kumteua mtu yoyote kumwakilisha popote.

Pia kuna hierarchy ya ki Protokali
No. 1. Rais
No. 2 VP
No. 3 ZnZ President
No. 4 PM
No. 5. DPM
No. 6 VP 1- ZnZ
No. 7 VP 2- ZnZ
No. 8 -Spika
No. 9- CJ
No. 10- CDF

P
Kwa kutokuitaja Tanganyika, hoja yako imekosa mashiko!
 
Leo umeamkia wapi? huyu ndiyo Paschal Mayalla (2016) na siyo nani hii wa 2024, aibu tupu kabisa Kinondoni ni Wilaya na wakati na wakazi zaidi ya milioni 2 Zanzibar nchi ina wakazi 1.2M.
The determinant ya jimbo, mkoa na wilaya is not determined by idadi ya watu. Zanzibar ina special status, ilikuwa nchi, tulipoungana kuwa nchi moja, Zanzibar ilipewa independent status ya mambo yake ya ndani. Nimeshauri ipewa status ya jimbo ili rais wa Zanzibar awe Gavana wa jimbo la Zanzibar.

Yes ndiyo maanake Tz iwe na majimbo 7 bara na 1 Zanzibar, tuwe na Rais mmoja pekee na Waziri Mkuu ambaye ndiyo Makamu wa Rais, tuondoe hizi gharama za hovyo nchi masikini lakini ina utitiri wa viongozi na misafara ya hovyo ambayo haina tija kwa mlipa kodi, hili jambo Mbowe kalisema sn na ndiyo mataifa ambayo yameendeleo yanafanya hivyo hata SA.
 
Naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom