Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Majina yanatangazwa na kata kabla ya NBS, nini maoni yako?
 
Hii nchi ni ngumu sana. Kuna wengine wameandikiwa status ya hana ajira wakati ni walimu waajiriwa wa serikali ambao tunaishi nao mtaani na hapa ndipo naamini kuwa hili zoezi linafanyika kwa maelekezo na connection za hapa na pale
 
Aisee,nilihangaika sana kufika kenye usaili.wilaya yetu ilikiwa ya mwisho kutoa majina ya walioitwa kwenye usaili.wakati yanatoka nilikuwa niko kigoma kuripoti ajira mpya.sasa ikanidi niombe ruhusa fasta ya kwenda kujiandaa siku 14.

Majina yalitoka j5 usaili alhamis, nikapita halmashauri nikasainiwa fomu.nikapanda mchomoko,gari wanazotumia kusafiria hadi kasulu.nikasubiri gari kutoka kigoma mjini ikafika kama satano imejaa balaa,nikaona isiwe tabu nilisimama hapo naelekea mwanza.aisee nilisimama miguu ikawa inawaka moto.tulifika kibondo saa kumi jion.nikaona hapa usaili umeshanipita mana uhakika wa kufika mwanza siku hiyo haukuwepo.

Basi tukaendelea na safari hadi lunzewe tulifika sa2 usiku ikabidi kulala pale.asubuhi siku ya usaili ndo natoka lunzewe kupitia Geita hadi busisi.matumaini yakaanza kurejea tulipofika kivukoni busisi sa tano huvi...cha kushangaza mtandao wa kukatia tiketi kivukon ukaroga nikasubiri lisaa pale.nilivuka kama sa sita na ushee.kwa ujumla nilifika Nikakuta watu wengi mno.

Kwenye usaili;waliokuwa wanahoji watu walikuwa wamechoka yani tulikiwa tumefungiwa kwenye ofisi akija anaita watu ka sita,baada ya dktatu anarudi tena.

Kimbembe kilikuja nilipoitwa nikaambiwa taja majina yako na elimu...naitwa x nina bachelor degree. Hee wakashangaa,degree ya nini...elimu mwaka 2015...hujaajiliwa ...ndio bado...wewe tambi lote hilo hujaajiliwa...nikaona isiwe tabu...napiga partime shule x ...hapo sawa.

Sijui kwanini walikiwa wanauliza sana kuhusu ajira.
 
Mbona huku Bongo hakukuwa na mambo mengi

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Sio sawa ata kidogo wanaume tudai haki zetu[emoji23]
Wachache ambao wapiga kazi wengi ila wengine haswa masista duuh hawataweza nimeona kwenye postikodi mwanzoni,wanawake wanaacha kabisa au kazi inachelewa akisema kachoka kachoka.
Kutembea na kuhoji watu sio mchezo kama nilivyoona madodoso ni 5 dadeki lets wait and see

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Huo.mchakato ndio upo hivyo ?
 
Mtaannkwangu ktk postikodi alikuwa ana tuhoji sister duu eti alikuwa ana kodi boda boda inamtembeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…