Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Kama halmashauri ndio wataachiwa wawafanyie watu usahili...basi mchezo utakuwa umekwisha hapo maana hapo wazee wa UV watachakachua na kuweka makada
 
Samahani wazee kwa mwenye taarifa za majina ya waliochaguliwa nafasi ya ukarani Arusha mjin atupe info, jana moshi naskia washatoa majina.
 
Anna makinda anasema hakuna pesa za kumwaga eti utegemee kutoka na million anadai ni zoezi LA kizalendo itatakiwa itumike hela ndogo as much as possible ukizingatia expectations za vijana walio wengi wanahisi watatajirika kupitia zoezi
Inasikitisha sana ,pesa hakuna za kuwapa watu wanao toa jasho lao katika zoezi la kitaifa na wengine majobless ila pesa za wakubwa kupiga na kujaza matumbo yao pasipo kufanyia kazi zipo.

Mfano mimi kuna ndugu yangu kijijini zoezi la anuani ya makazi kwenye kata yao wameambulia elfu 30 tu mpaka zoezi linaisha.
 
Hii dunia ni nzito sanaaaaa! Wakati mwenye degree anaomba Mungu apate kibarua cha sensa apate mataji wa laki 5, muda huo huo kuna mvuvi kapata 450k ya sangara kwa usiku mmoja anakula maisha bar.

Mlango mmoja ukifungwa pitia dirishani bila kujali kiwango cha shule ulichonacho
binadamu tuna safari ndefu kwenye dunia hii.
 
Huu uzi unadhihirisha hali ya maisha tuliyonayo mtaani.

Kuna mdau hapo kalalama kuhusu wasio na elimu kuchanganywa na wenye kisomo.

Labda nimwambie tu kuna baadhi ya kazi wakiitwa hao wa form 4 wewe ukaachwa kweli unaweza kulalamika mfano kazi zihusuzo kada fulani, lakini hii ya sensa ndgu yangu hata hao form 4 wanafanya vizuri kabisa coz kufeli form 4 sio kutokua na akili na wengine hawakuendelea kwa sababu mbalimbali ila as long as ana cheti huyo anafaa.
Mwisho kabisa, tafuta njia ya kujikwamua ili usiwabebeshe watu lawama.

Tukutane kwenye usaili.
 
Inasikitisha sana ,pesa hakuna za kuwapa watu wanao toa jasho lao katika zoezi la kitaifa na wengine majobless ila pesa za wakubwa kupiga na kujaza matumbo yao pasipo kufanyia kazi zipo.

Mfano mimi kuna ndugu yangu kijijini zoezi la anuani ya makazi kwenye kata yao wameambulia elfu 30 tu mpaka zoezi linaisha.
Ukihoji wanadai huo uzalendo kwa taifa
 
Umeandika Upupu Tuuu,, hao wasomi wanausumbufu gani? yaan Ww unauhakika Kuwa Wasomi ni wasumbufu kuliko Form 4 ebu lete ushahidi hapa....Eti uchukue kilaza aliyepata mswaki wa hesabu akahesabu watu unamuacha Msomi mwenye uelewa mpana zaidii wa hesabu na Technologia...... Alafu unapanua Domo lako kuongea na kuandika hovyo hovyo,,,,,,, Ebu waacheni waliokomaa Na Elimu mkashindwa kuwaajiri Wapate pesa za kujiajirii
Unaongea kama vile hesabu zinazotumika kuhesabu watu ni expansion na caliculus za kutisha kuna watu wana degree lakini hesabu ilikuwa ni ugonjwa ukisema hivo manake wanaofaa kwenye zoezi ni wale waliosoma advanced mathematics na BAM

Ni possible kabisa kukuta mtu ana degree ya sheria ila hesabu ya O level ana mswaki kwa hiyo na yeye ni kilaza
 
Back
Top Bottom