Kiongozi kiuhalisia nyota moja ya JWTZ si sawa na nyota moja ya Polisi na wenzao wote wa mambo ya ndani, kule Monduli maluteni usu kila mwaka huwa wanaapishwa na President tu, na hajawahi tuma mwakilishi 'kwa niaba yake' ni lazima aende yeye mwenyewe
JWTZ hakuna gazetted officers wote kuanzia Luteni usu hadi Generali huitwa commissioned officers
Anyway labda mapolisi wa humu ndani watuambie hapo kwenye masuala ya protocol, kwamba kwa mfano Luteni usu (nyota moja wa jwtz) na ASP (nyota tatu wa polisi) wakikutana, nani ataanza kudondosha Salute kwa mwenzake
Wapo wanaosema hayo ni majeshi tofauti yenye mifumo tofauti, hivyo haina haja ya kupigiana salute, labda wao wenyewe wa mambo ya ndani ndio vyeo vyao viko sawa ila siyo kwa JWTZ
Lakini as far as i know ni kuwa JWTZ ndio jeshi senior na superior kiprotocol, ndio maana hata kwenye mikutano ya viongozi mfano ikulu au bungeni mpangilio wao wa kukaa mara nyingi huwa anaanza CDF, IGP, DGIS, CGP, CGF then CGI, halafu ndio wanafuata hao wa PCCB na DCEA
Hata kipindi cha Magufuli alitaka aanzishe system ya kuteua general officers wa JWTZ kuwa wakuu wa vyombo vya usalama vya mambo ya ndani, mfano alimteua Suleiman Mzee kuwa CGP Magereza ambaye alikuwa ni Major General cheo cha tatu kutoka juu, na tena hiyo ilihesabika ni kama demotion
Wakati kwa magereza cheo cha tatu kutoka juu ni DCP, so maana yake ni kwamba, Major General wa JWTZ na DCP wa Magereza kiprotocol hawako sawa MG ni mkubwa