Ikitokea naenda tuu, maana hakuna namna. Ili mradi niwe nalinda usiku, kupiga kwata kwa unaa mkubwa, kombati ya jeshi niwe naitupia kwa mwili ile imenyooshwa kwa pasi mpaka nzi anakatika akijichanganya ! Buti inang'ara kama kioo ....kidevu kiwe kipara kichwani kuwe na upara, kila siku mabio mazoezi ya kukata na shoka, niwe napiga Combat karatee balaa niwe napambana na adui kwa silaha ile kama vitani hiviii .... na kupata raha zingine za kijeshi kama hizo, ndio nafsi yangu itaridhika na siku hiyo ntamshukuru sana mwenyezi Mungu ikitokea.