Back in days.
Huu uzi ulikuwa ni kama faraja yangu ya kutafuta fursa hizi nikiwa na Id yangu ya LYOBA.
Nililiwa kichwa mapema sana kwenye saili za mwezi wa 1 za Polisi.
Nilichanganyikiwa sema pia panicking ilikuwa inafaida kwa muda huo.
Nina kielimu na ni mtaalamu wa Physics since high school though sio mwalimu.
Basi nikapata chaka (Shule) mwezi wa pili hiyo nikawa nalipwa 200k Chakula nakula scul hapo hapo.
Buddy nilikubalika hapo maskuli jina likasambaa sana kwamba ni mtata(wananiita Eisten siku hizi).
Buddy huwez amini kuna shule za watu wenye hela zao wakaja mwez wa 6 wakanichukua , wananilipa 500k bila makato na nakula shule na nyumba nimepewa(Alhamdulillah).
Kwasasa nawaza nifanye vizuri mwakani nimalize nina kimtaji cha kuanzia maisha maana kazi za private hazina dhamana.
Tusikate tamaa wapambanaji, Mwenyezi mungu anamipango mizuri sana na sisi.