Mi nilipita pale kwata walikaza kama kawa, siwez sahau Kuna Babu mmoja anavuta sigara atar ni staff sajent anaitwa "Babu Venue" mzee alituzungusha round 25 za mwendo wa pole, Kila saa tuna maliza unaskia "Samahani afande warudie tena". Mkifanya vizur anafurah anataka mrudie tena aone mkifanya vibaya mtakula kazi na mtarudia Yani ile siku tulitoka paredi kama tumeganda mpaka ma private wakawa wanasepa kula Tano alafu wanarudi mzee yupo na sisi. 😂😂😂 Kesho yake asubuhi akatuamkia tena mzee akatushtua kwata kidogo tukarudisha silaha Amala tukanywa chai tumerudi akatupiga ruti ndefu ile tumefika😂😂😂 tukawekwa kivulini Ili tufundishwe silaha alafu ma private wamejaa kibao, oya😂😂😂😂 tulikua tuna kula mabanzi vibaya mno sababu watu tunasinzia pale kwenye vivuli vya miti Kuna upepo balaa afu watu tumechoka mnoo. Yani jirani yako anapigwa banzi pembeni yako unashtuka 😂😂😂 baada ya dk 5 mnasinzia tena, daah