Kijana vipi hizo comments umelazimishwa kuzisoma, mbona ni kama zinakuumiza sana, hivi hujaachaga tu kulalamika
We jamaa ujue nimeanza kukuona kumbe hamnazo, we mwaka jana nilikuwa naziona sana comments zako kwenye huu uzi na ule wa Magereza, kipindi unajiita
Gpili ulikuwaga unalalamika sana
Katika watu niliokuwa naombea muingie kwenye haya majeshi ni wewe na kina
MrGeneous,
dean05 na
Kunguru wa Manzese maana inaonekana mmepambania sana, wenzio tayari washazama Magereza wewe bado uko hapa unapambana
Lakini badala ya kujadili vitu unavyoona vina faida kwako umekomaa na mengine yasiyokuhusu, huu uzi una lonja za kila aina, wewe chukua kile kinachokuhusu kisichokuhusu achana nacho tu
Wala hakuna aliyesema kwamba majeshi ya mambo ya ndani ni inferior huko ni kujishitukia tu, kila jeshi lina umuhimu wake kwa nafasi yake, sisi hapa tulikuwa tunajadili mambo ya protocol tu, hayo mambo ya heshima sijui maslahi mmeyaleta ninyi, mbona wenzio wengi wanapita kimya wanajadili yanayowahusu tu
Tena kuna wenzio wametoka kusema humu kwamba huu uzi unaweza kuwa unahusu Polisi na Uhamiaji, ila si vibaya watu wakijadili na majeshi mengine maana si kila mtu anataka huko, na ukizingatia vyote ni vyombo vya ulinzi na usalama tu
Halafu cha kushangaza comments zinazokuumiza ni zile zinazohusu JWTZ tu, mbona hadi Magereza na Zimamoto huu uzi hauwahusu ila wanajadiliwa sana humu na hulalamiki chochote, mimi majeshi yote nayakubali tu sijali cha heshima wala maslahi, mimi nasoma lonja za majeshi yote huku nipo na kule Magereza pia nipo, japo sijaomba kokote napenda tu kuyafuatilia
Au wewe TPDF unapapenda ila unaleta mambo ya sizitaki mbichi hizi sababu imeshindikana kuingia, maana nakumbuka mwaka jana ulisema unapenda Jeshi ila mwaka huu umehama mara unapenda Polisi tena FFU, ukikosa na huko sijui utapenda wapi kwingine
Acha kulalamikia kijana