Mnadhimu mkuu jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othmani ,amewataka askari wapya waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika shule ya mafunzo ya RTS Kihangaiko kutokujihusisha na vikundi vya ushawishi wa vyama vya siasa,matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ,pamoja na makundi ya kiuhalifu.Katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika shule hiyo Luteni Jenerali Salum Haji Othmani ,amesema kwa yeyote atakaebainika kushiriki katika vitendo hivyo ataondolewa jeshini.Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya mafunzo RTS Kihangaiko Kanali Michael Mayala, amewataka askari hao wapya kwenda kufanya kazi kwa bidii katika maeneo yao ya kazi watakaopangiwa pamoja na kuzitunza afya zao.
View attachment 2675055