Yeah mkuu ndio maana nikasema tukifikiria sana vitu vinavyoshindikana ni vingi haviishi, hii nchi kwenye ajira hakuna linaloshindikana asee, kuna ndugu yangu mwaka jana alizama TISS hii kambi yao ya Mbweni na hakuwa na cheti cha jakata
Sasa hivi kashamaliza course yuko zake kazini, watu huko vyomboni wanaingia tu kuna mtu ana vigezo vyote anachomolewa na kuna mtu hana vigezo vingi ila anapita bila kupingwa, wengine nasikia wanaingia katikati ya course hata baada ya six weeks kuisha
Mimi huwa najisemea kwa hatua hii niliyofikia sidhani kama kuna cha kunishangaza tena, maana hii nchi yetu wengi ishatushangaza hadi tushakuwa masugu, ukijumlisha na mambo tuliyopitia kwenye maisha yetu yani hatuoni cha ajabu wala kipya tena