Nafikiria kufungua kesi ya Madai dhidi ya Lissu na Wenzie

Nafikiria kufungua kesi ya Madai dhidi ya Lissu na Wenzie

Wilderness Voice

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
921
Reaction score
1,649
Baada ya kusoma taarifa alizozitoa Lissu katika vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa kuhusu afya ya Rais na hatimae kueneza taarifa kuwa Rais karejea kwa muumba, ilinisababishia mshituko mkubwa na kuleta tatizo kiafya:

Kwanza nilipata mshituko wa moyo ikizingatiwa Rais ni kiongozi wa nchi. Ni nembo ya Taifa. Hivyo naipenda nchi yangu. Na mnampenda Rais wangu.

Pili, Kutokana na uwasilishaji wa hiyo taarifa ya Lissu na wenzake katika Twitter. Walitumia maneno ya kashifa kwa kiongozi wa nchi. Hii ilileta usumbufu kwangu kwa baadhi ya watu huku niliko kutumia maneno ya Lissu na wenzie kumsema vibaya Rais. Hii ilishusha hadhi ya nchi yangu na kusababisha dharau na kejeli.

Lissu alisababisha jamii za watu tofauti kumwamini hivyo kujenga sura hasi kwangu kama Mtanzania. Niliathirika kisaikolojia.
Hivyo Lissu na wenzake wanawajibika katika kunisababishia maumivu ya moyo na kisaikolojia.

Nipo tayari kuwasilisha ushahidi wa daktari. Na wataalamu wa saikolojia.

Pia na jiandaa kuishitaki Serikali kwanini haijachukua hatua dhidi ya Lissu na wenzake waliosababisha habari hizi za uongo kuenea wakati wakijua Rais ni nembo ya Taifa. Kuumwa ni swala la kawaida. Lakini kwanini waeneze uongo na hata habari za kifo.

Je, walikusudia kuleta sintofamu katika nchi? Eti Polisi wanaenda kumkamata fundi wa simu. Nadhani wanatania. Ingieni huko Twitter muone kama ni huyo fundi kaeneza hz taarifa pekee. Source anaachwa.

Hivyo nitashitaki Jeshi la polisi kwa uzembe wakutochukua hatua na kuacha taarifa kusambaa wao wametulia tu na kuzua taharuki kwa jamii.
 
Mpaka sasa umeshafungua kesi ngapi, maana kama taarifa za misiba za ndugu/ jamaa zako wa karibu kwa vyovyote umeshakumbana nazo sana!!???!!??!!??
Tofautisha msiba wa kweli wa ndugu na kuzusha habari za uongo za msiba tena Rais wa nchi. Ndugu akifa nitaarifa halisi si uongo. Ni hakika.
 
Mpaka sasa umeshafungua kesi ngapi, maana kama taarifa za misiba za ndugu/ jamaa zako wa karibu kwa vyovyote umeshakumbana nazo sana!!???!!??!!??
Soma uelewe. Sijawahi pewa taarifa za uongo za vifo kwa ndugu zangu. Hata hivyo mambo ya ndugu umalizwa kiukoo ktk vikao. Hapa nimeongelea Rais.
 
Back
Top Bottom