Napata tabu sana kwa watu wenye mawazo yakuajiriwa hasa wazazi wetu kwangu naona ndio tatizo,
Binafsi nimesoma biashara na mwanzoni nilipata ajira lakini sikuwahi kuona faida yoyote na nilipoamua kuacha kwa wazazi ilikuwa ni tatizo sana,
Ndani ya miezi sita niliacha kazi na sasa napambana na maisha mtaani faida yakufanya biashara ni kubwa sana kuliko hizi ajira ,
Binafsi nafanya kilimo,mifugo na biashara najisikia amani sana,
Ninaendesha miradi na ninao hao wenye fikra za ajira na kwa mwezi nalipa mishahara milioni plus,
Nashauri wazazi tuwejenge watoto wetu sumu mbaya waichukie ajira,
Nashauri sumu ifanane kama ile nyerere alioipanda Tz kumchukia Idd Amini tangu tukiwa mashuleni nyimbo nyingi za mchakamchaka asubuhi zilikuwa za chuki dhidi ya Amini.
Mwache mtoto asomee apendacho kwani fursa ipo popote kwa chochote mtu anaezingatia vizuri anachojifunza anafanikiwa.
Nilidhani ungehitimisha kwa kusema asisome akafanye biashara.
Mleta mada ana tania tu, maisha haya nani anaijua future?!
Zame zile madaktari walikuwa hot, siku hizi wafanyakazi wa TRA na TAKUKURU ndio wanakimbiza mjini.
I wish RUSHWA INGEKUWA INASOMEWA, hata mimi ningepeleka wanangu wakaisomee inafanya TRA, TISS na TAKUKURU wamekuwa na mvuto kwa jamii kuliko hata vitu vyenye tija.
Anyway someni na somesheni ila kumbukeni kinachotafutwa siyo elimu bali pesa.
Mtu anatafuta pesa unataka kumtoa kwenye course za pesa umpeleke kwenye ufugaji?!
Muache akae karibu na pesa.
Mifugo yenyewe inafaida mijini,huko vijijini haina faida yoyote, tizama wanaofaidika na kilimo na ufugaji sio wakulima wala wafugaji, ni wafanyabiashara wa mazao ya mifugo na kilimo.
Unadhani kwanini hata benki ya wakulima iko mjini?!
Jamani kuna kozi zinalipa na kuna kozi za sifa.
Angalia madaktari wako busy 24/7 kukimbizana na wagonjwa na shift za kazi, wahasibu na wafanyabiashara wanakula bata.
Kozi ngumu zinafanya maisha yawe magumu tu.
Elimu nzuri ni pesa tu, wala sio vyeti.