Nafikiria kumtoa mtoto IFM na kumpeleka chuo cha mifugo; waungwana mnashauri vipi?

Nafikiria kumtoa mtoto IFM na kumpeleka chuo cha mifugo; waungwana mnashauri vipi?

marehemu mkapa alisemawakati Fulani kuwa elimu yetu tunahtaji mjadala mzito sana lakini nadhani hatukulitendea haki swala husika na bado liko chni ya uvungu tu
 
Kwanza usipoteze muda wako kumoa mtoto elimu kwa nua ya ajira,utamharibu kabisa,kwani ajira ni big problem,pili muachie mtoto asome anacho kitaka
nakuelewa mkuu lakini pamoja na hayo wanahitaji kuelekezwa kwenye uhalisia
 
Mkuu kila koz inafaida na hasara yke,binafsi ungeeleza hapo IFM anasoma kozi gan,pia mtoto wko yupo tyr na iyo koz ya mifugo .
anasoma masuala ya usimamizi wa fedha.........nimepanga kumuelimisha kwanza, nitatumia ukweli halisi na kisha nguvu ya uzazi
 
Kama Elimu ni kwa manufaa yake mwache asomee atakacho but kama ulimzaa apate kazi unufaike nayo kabla haujafa basi kamsomeshe hayo madude. Namhurumia sana mwanao maana utamtolea radhi lazima pale atakaposhindwa kukutumia pesa kisa Halmshauri mishahara midogo. Hata huko IFM vijana wanaajiriwa hadi BOT na TRA, so ukimuona mtoto wa jirani yako kamnunulia Kluger baba yake basi utamrudisha tena IFM mwanao nawe akununilie.
Badili mtazamo mzazi maana hatuwazai watoto watulishe bali wawe rafiki zetu nguvu zitakapotuishia kwa kutuondolea upweke.
 
Hapo amekurahisishia kazi mpeleke tu veta akasomee ushonaji ada ni kidogo tu kama laki 3 hv
Tuna mdogo wetu wa kike hajafaulu vizuri sana ila hataki tena kusoma na kasema anapenda kujifunza kushona awe fundi.
 
Habarii!

Nimefikiria kufanya hivyo baada ya kuona kuwa elimu ya mambo ya fedha itolewayo na IFM ajira zake ni ngumu sana; yahitajika uwe na wigo mpana wa wakubwa ili kuweza kuajirika. Makapuku sisi tutasubiri sana. kama hiyo haitoshi, inakuwa ni vigumu kwako kujiajiri ikiwa utakosa ajira.

Chuo cha mifugo naona kama ni rahisi hata mtoto mwenyewe kujiajiri ikiwa atakosa ajira. Anaweza akatafuta vikuku au vimbuzi vyake vinne akaanzisha mradi. ushauri wenu wadau
Unaweza ukawa unapiga hesabu ngumu kiasi kama unampeleka mifugo ili aje kufuga mwenyewe. Kama ni hivyo angeanza tu kufuga asipoteze hiyo miaka miwili chuoni. Ila cha msingi vijana waliohitimu mifugo ni wengi sana sana mtaani na si rahisi kwa wao pia kujiajiri kama walivyo hao wa uhasibu. Acha mtoto asome aelimike anaweza kufuga hata akiwa ni mhasibu kwa taaluma.
 
yeye mwenyewe anasemaje ?

Kufuga vikuku vinne na vimbuzi na kuanzisha mradi mpaka usomee mifugo ?
Mkuu hata kama akitaka kufuga ng'ombe 1000 hana haja ya kusomea mifugo. Wataalamu kibao mtaani anakuja unamlipa anafanya kazi ya kitaalamu anaondoka zake.
 
Anaongeza skills tusiwe wajinga sana
Kama ni skills tu si unaenda hizi short course kibao tena zimetengenezwa vizuri kabisa. Kwa nini upoteze miaka miwili ambayo mengine unayoyasoma wala hayakusaidii chochote. Nenda short kozi ambayo inakuwa ni mahususi kwa kile unachokitaka.
 
Muache mwanao Achague anachopenda, usimchagulie wewe,yeye ndio anajua Kama anawezana na Masuala ya fedha au Kilimo!
 
Kama Elimu ni kwa manufaa yake mwache asomee atakacho but kama ulimzaa apate kazi unufaike nayo kabla haujafa basi kamsomeshe hayo madude. Namhurumia sana mwanao maana utamtolea radhi lazima pale atakaposhindwa kukutumia pesa kisa Halmshauri mishahara midogo. Hata huko IFM vijana wanaajiriwa hadi BOT na TRA, so ukimuona mtoto wa jirani yako kamnunulia Kluger baba yake basi utamrudisha tena IFM mwanao nawe akununilie.
Badili mtazamo mzazi maana hatuwazai watoto watulishe bali wawe rafiki zetu nguvu zitakapotuishia kwa kutuondolea upweke.
kiufupi mkuu siwazi kabisa habari za yeye kuja kunisaidia (nasema hili kutoka moyoni kabisa huku Mungu akiwa shahidi yangu kwani naamini ye anayajua yaliyo mioyoni mwetu)......nahitaji maisha ya kawaida tu na katika kujiandaa na maisha ya uzeeni ninaendelea kuandaa kashamba ka ekari tatu haka ambapo nitakuwa naishi humo na kujiandalia mwenyewe bamia za kulia ugali pale nitakaposhindwa kukimbizana na dunia.

tatizo kubwa ni kuwa ninatatizika na future yake. najiuliza mtoto huyu na umaskini huu, na kutojulikana huku, na tatizo hili la ajira lililopitiliza, na kutojulikana huku kwa hatima ya maisha yangu n.k.; ataishi vipi kwa ujuzi tu wa utunzaji fedha? si bora ajifunze kitu kitakachomsaidia kuzitafuta hizo fedha milele na milele hata bila kutegemea kujulikana au uwezo wa kifedha?
 
Me mtoto wangu PhD na masters awachie akina professor mkumbo atasoma Mwisho A level baada ya apo aje tupambane ninapo pambana!
Kuowa lazima ndani miaka 25
 
Kwanza usipoteze muda wako kumoa mtoto elimu kwa nua ya ajira,utamharibu kabisa,kwani ajira ni big problem,pili muachie mtoto asome anacho kitaka
Acha kumdanganya mwenzio mifumo ya elimu ya Tanzania 99% huwa tunategemea kuajiriwa mara baada ya kugraduate ni hitaji la mfumo wa elimu yetu wala si matakwa ya msomaji
 
Mkuu hata kama akitaka kufuga ng'ombe 1000 hana haja ya kusomea mifugo. Wataalamu kibao mtaani anakuja unamlipa anafanya kazi ya kitaalamu anaondoka zake.
sawa lakini kuna utofauti mkubwa kiongozi kati ya dereva anaejua kutia gia tu na dereva mwenye ujuzi wa makenika
 
gpa za maana hizo kwio....mmhh sio kwa IFM mkuu pale ni shida ..kikubwa elimu yetu iko kwenye kuajiriwa sana kuliko kujiajiri
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ausioo...!! Kwa hiyo aende kwenye kilimo
 
Back
Top Bottom