Nafikiria kumtoa mtoto IFM na kumpeleka chuo cha mifugo; waungwana mnashauri vipi?

Nafikiria kumtoa mtoto IFM na kumpeleka chuo cha mifugo; waungwana mnashauri vipi?

Unajua hapa tunamuongelea kijana ambaye yupo Chuo na Sio mtoto wa Chekechea ?, Kama mtu umefika mpaka form six haujajua unataka nini sio vibaya sana unaweza ukauliza au ukafanya research mwenyewe na kuangalia available options..., Ila kama unajua unataka kufanya nini hata kama upo Primary School (follow your Dreams)

Kumbuka kwenye maisha its not all about kipato (unaweza kupata kipato hata bila kusoma) kwenye maisha ni kuishi na kuishi ni kufanya kile unachokipenda..., haukatazwi ukiwa lawyer ukafungua mgahawa na ukapika na ukifungua mgahawa sio mpaka ujue kupika..., biashara inahitaji discipline, experience na uvumilivu (nikupe siri non of them are taught in school)..,

Basic business skills ni selling; buying/producing;reselling yaani investing and reinvesting hivyo ndivyo anavyofanya muuza nyanya mtaani mpaka Azam viwandani....., mimi ninayejua hizo theory huenda nisiweze kufanya hayo.. WHY? maybe I lack discipline.... (kwahio ndio maana mtu akija kununua product haulizi una cheti kipi) unless otherwise unachokiuza ni skills zako.., mfano Daktari, Muhasibu (kutoa services) au Services yoyote ile inayohitaji knowledge (thus you are selling your knowledge)

Pili Elimu knowledge haipatikani kwenye mashule tu hata experience ya kuuza karanga kwa miaka kumi hio ni shule tosha ambayo mtu fresh from school hana....

Mkuu, hiyo kitu unaita 'follow your dream' ni nadharia ya kimagharibi na haitekelezeki kwa vijana wetu walio wengi hapa Tanzania na sehemu nyingi Afrika kwa sababu mifumo yetu ya elimu haiandai vijana kuweza kufanya hivyo . Hata huko Magharibi kwenyewe vijana wanaachwa wajichagulie kwa sababu mifumo wao wa elimu na maisha kwa ujumla imewaandaa kutambua hizo 'dream' zao kwa kuzilinganisha na -'options' nyingine nyingi na hatimaye wanafanya uchaguzi wanaouelewa vizuri. Huwezi kumlinganisha A-level/college graduate wa Uingereza na wa hapa kwetu aliyemaliza shule ya kata huko mikoani. Kule kwa wenzetu kuna masomo ya 'career guidance' toka awali kabisa kuwezesha vijana kufanya maamuzi wanayoelewa vizuri hapo baadae. Hapa kwetu vijana wanaishia kushauriana wenyewe kwa wenyewe na wengi wanaishia kusaka ajira na vibahasha mitaani na wanakuja kujifunza fursa zingine baadae wakiwa wameshapoteza muda mwingi.

Yaani wewe unataka kijana apoteze muda kusoma akitegemea atakuwa 'lawyer' halafu baadae maisha yakimchapa mtaani ndio aanzishe 'business' ya kuuza mgahawa? Huko ndio ku - 'follow your dream'? Kwani kama angeshauriwa mapema kabisa kwamba asomee 'business' ili aanzishe biashara yake mwenyewe kwa sababu siku hizi lawyers hawana ajira za kutosha, kuna ubaya gani?
 
Tukubaliane kutofautiana kitu kinachofanywa na mtaalam si sawa na asiyejua. Infact wengi hukosa kufanikiwa kwa kufikiri kuwa kufuga vikuku vinne na vimbuzi haihitaji utaalam
una uwezo wa kuwa mtaalamu wa vitu vingapi ?, practically hii ni impossible (kwahio ukifungua hotel ) inabidi uwe mtaalamu wa marketing, finances, hotel management, hospitality, chef. kitchen porter, store management, room services bila kusahau business na investment management (ukizingatia wewe ni mfanya biashara)... haoni hapo unaweza ukawa effective ila sio efficient ?

Je ni bora kufanya hivyo au wewe sababu unajua biashara na mambo ya investment kwanini usinunue hio hoteli na kuweka mtu wa hotel management ashughulikie yote hayo na wewe mwisho wa siku ni kuangalia profits / losses ? Kumbuka siku ina masaa 24 tu..., na ni bora kupata 5% ya kitu ambacho hakitumii muda wako kuliko 100% ya kitu ambacho kinachukua 100% ya muda wako..

By the way sio kwamba usipokuwa mtaalamu wa mifugo hautajua kwamba kuku huwa anataga na mbuzi anakula majani na sio nyama (you need basic knowledge) sio kuwa Expert..., na ukifuga hao kuku kwa miaka kumi lazima utakuwa na utaalamu kuliko mtu aliyetoka chuo (tena vyuo vya kibongo ambavyo havina hata shamba darasa).. sababu wewe utakuwa na kitu ambacho yeye hana... (experience)
 
Yaani wewe unataka kijana apoteze muda kusoma akitegemea atakuwa 'lawyer' halafu baadae maisha yakimchapa mtaani ndio aanzishe 'business' ya kuuza mgahawa? Huko ndio ku - 'follow your dream'? Kwani kama angeshauriwa mapema kabisa kwamba asomee 'business' ili aanzishe biashara yake mwenyewe kwa sababu siku hizi lawyers hawana ajira za kutosha, kuna ubaya gani?
Duh... hivi unajua business ngapi zinafail percentage-wise ?, au unajua waliofanikiwa wamefeli mara ngapi mpaka wakafanikiwa.., Tatizo unadhani kujua theories za business ni kufanikiwa katika business.., hata mtu akisomea hio business majority bado wanatafuta ajira...

Desire, discipline na ambition ndio zinamfanya mtu awe self made/ self employed hata huyo lawyer sio mpaka apate ajira anaweza kuuza skills zake (that is business) pia fahamu kabisa kwamba elimu haina mwisho kwahio kama mtu yupo creative anaweza tangia yupo huko chuo akaanzisha chochote ambacho angekianzisha siku anamaliza chuo, sababu elimu atakayoipata through practical ni tofauti na theory... Na siku anapewa cheti kwamba amehitimu elimu inaendelea haibakii chuoni...
 
yeye mwenyewe anasemaje ?

Kufuga vikuku vinne na vimbuzi na kuanzisha mradi mpaka usomee mifugo ?
Yes, kufuga kitaalam kunalipa sana. Kuna jamaa yupo Kibamba alisoma udaktari wa mifugo na sasa ni mfugaji mkubwa mno. Sidhani kama yule jamaa anahitaji ajira ya mtu. Ng'ombe 20 wa maziwa, kuku wa nyama na mayai sidhani kama kuna ajira inalipa zaidi ya hiyo, labda siasa ndio zaidi.
 
Yes, kufuga kitaalam kunalipa sana. Kuna jamaa yupo Kibamba alisoma udaktari wa mifugo na sasa ni mfugaji mkubwa mno.
Kufanya jambo lolote kwa utaalamu kuna tija kuliko kufanya holela... Swali ni kwamba lazima uwe mtaalamu ili ufanye jambo kitaalamu...

Huyo jamaa sio kwamb anaweza kufuga tu.., pia ana option ya kuuza skills zake (yaani kutibu wagonjwa wa wenzake kama soko lipo) wewe hapo ambaye sio daktari wa mifugo mfugo wako akiugua haukatazwi kumuita jamaa yako ili afanye hio kazi kwa ujira.. Kwa ufupi sio madaktari wote wa mifugo ni wafugaji...

Sidhani kama yule jamaa anahitaji ajira ya mtu. Ng'ombe 20 wa maziwa, kuku wa nyama na mayai sidhani kama kuna ajira inalipa zaidi ya hiyo, labda siasa ndio zaidi.
Hapa sijakuelewa kwamba veterinary science ndio inalipa zaidi au ? Jamaa yako amefanikiwa sababu ameweza kupata soko la bidhaa yake contionously.., kuna wafugaji wengine wanalia hawapati masoko, kwahio issue sio kupata product tu, bali how to sell your product, pia hata wewe ukipata soko la uhakika ukafuata kanuni za ufugaji unaweza kupata zaidi ya jamaa yako hata kama wewe hauna utaalamu au utaalamu wako ni lugha ya kifaransa.., ila fahamu kwamba mwaka wa kwanza elimu/ujuzi wako hauwezi ukawa sawa na mwaka wa kumi (experince) you will become better with the time and learn through experience...
 
Habarii!

Nimefikiria kufanya hivyo baada ya kuona kuwa elimu ya mambo ya fedha itolewayo na IFM ajira zake ni ngumu sana; yahitajika uwe na wigo mpana wa wakubwa ili kuweza kuajirika. Makapuku sisi tutasubiri sana. kama hiyo haitoshi, inakuwa ni vigumu kwako kujiajiri ikiwa utakosa ajira.

Chuo cha mifugo naona kama ni rahisi hata mtoto mwenyewe kujiajiri ikiwa atakosa ajira. Anaweza akatafuta vikuku au vimbuzi vyake vinne akaanzisha mradi. ushauri wenu wadau
Kongole sana mkuu naunga mawazo yako by 100%
 
Mkuu vipi ulifanikisha?
 
mkuu siyo mbaya mimi pia ni mojawapo wa mwanafunzi wa chuo cha mifugo mpwapwa naingia mwaka wa 3 uzuri wa hii course ni tamu sema kama mtoto kaipenda ila msuli unahitajika maana kuna muda kuamka saa 11 alafu baridi muingie kwenye ng'ombe cyo poa mi kabla sijamalza chuo nina mifugo yangu tu kuku na bata nafua pia kuna hata wenzangu wanafuga na manguruwe yaani full raha atuwazi ajira sana tukiajiriwa poa tusipo ajiriwa fresh ila vitu vingi tunasoma tu na nivyakujiajiri
 
Wacha asome mambo ya fedha kisha umfungulie 'benki' yake aiendeshe mwenyewe.. Hizi bank zinatoa fursa kwa watu kuendesha huduma za uwakala.. Mf mzuri ni Fahari huduma.
 
mkuu siyo mbaya mimi pia ni mojawapo wa mwanafunzi wa chuo cha mifugo mpwapwa naingia mwaka wa 3 uzuri wa hii course ni tamu sema kama mtoto kaipenda ila msuli unahitajika maana kuna muda kuamka saa 11 alafu baridi muingie kwenye ng'ombe cyo poa mi kabla sijamalza chuo nina mifugo yangu tu kuku na bata nafua pia kuna hata wenzangu wanafuga na manguruwe yaani full raha atuwazi ajira sana tukiajiriwa poa tusipo ajiriwa fresh ila vitu vingi tunasoma tu na nivyakujiajiri

NTA Levo gani?
 
komaa aisee
Wasalimie dr Madoshi, dr veneranda..
 
Habarii!

Nimefikiria kufanya hivyo baada ya kuona kuwa elimu ya mambo ya fedha itolewayo na IFM ajira zake ni ngumu sana; yahitajika uwe na wigo mpana wa wakubwa ili kuweza kuajirika. Makapuku sisi tutasubiri sana. kama hiyo haitoshi, inakuwa ni vigumu kwako kujiajiri ikiwa utakosa ajira.

Chuo cha mifugo naona kama ni rahisi hata mtoto mwenyewe kujiajiri ikiwa atakosa ajira. Anaweza akatafuta vikuku au vimbuzi vyake vinne akaanzisha mradi. ushauri wenu wadau
Anaweza kuwa na degree ya IFM na akafanya ufugaji.
 
Sem ukweli bhana ulishapataga maono kwa yaliotokea kwa grace
 
Habarii!

Nimefikiria kufanya hivyo baada ya kuona kuwa elimu ya mambo ya fedha itolewayo na IFM ajira zake ni ngumu sana; yahitajika uwe na wigo mpana wa wakubwa ili kuweza kuajirika. Makapuku sisi tutasubiri sana. kama hiyo haitoshi, inakuwa ni vigumu kwako kujiajiri ikiwa utakosa ajira.

Chuo cha mifugo naona kama ni rahisi hata mtoto mwenyewe kujiajiri ikiwa atakosa ajira. Anaweza akatafuta vikuku au vimbuzi vyake vinne akaanzisha mradi. ushauri wenu wadau
Umefanya uamuzi sahihi kabsaa,wataalamu wa mifugo wana fursa pana kujiajiri sanaa kuliko fani nyingi .mpeleke haraka akimaliza mpe million tatu tu afungue kiofisi cha kuuza dawa za mifugo na vyakula

Atapata wateja wa kuwatibia na kukuza mtaji Mara tatu zaidi ndani ya mwaka mmoja

Chukua hii itakusaidia sanaa
 
Back
Top Bottom