Unajua hapa tunamuongelea kijana ambaye yupo Chuo na Sio mtoto wa Chekechea ?, Kama mtu umefika mpaka form six haujajua unataka nini sio vibaya sana unaweza ukauliza au ukafanya research mwenyewe na kuangalia available options..., Ila kama unajua unataka kufanya nini hata kama upo Primary School (follow your Dreams)
Kumbuka kwenye maisha its not all about kipato (unaweza kupata kipato hata bila kusoma) kwenye maisha ni kuishi na kuishi ni kufanya kile unachokipenda..., haukatazwi ukiwa lawyer ukafungua mgahawa na ukapika na ukifungua mgahawa sio mpaka ujue kupika..., biashara inahitaji discipline, experience na uvumilivu (nikupe siri non of them are taught in school)..,
Basic business skills ni selling; buying/producing;reselling yaani investing and reinvesting hivyo ndivyo anavyofanya muuza nyanya mtaani mpaka Azam viwandani....., mimi ninayejua hizo theory huenda nisiweze kufanya hayo.. WHY? maybe I lack discipline.... (kwahio ndio maana mtu akija kununua product haulizi una cheti kipi) unless otherwise unachokiuza ni skills zako.., mfano Daktari, Muhasibu (kutoa services) au Services yoyote ile inayohitaji knowledge (thus you are selling your knowledge)
Pili Elimu knowledge haipatikani kwenye mashule tu hata experience ya kuuza karanga kwa miaka kumi hio ni shule tosha ambayo mtu fresh from school hana....
Mkuu, hiyo kitu unaita 'follow your dream' ni nadharia ya kimagharibi na haitekelezeki kwa vijana wetu walio wengi hapa Tanzania na sehemu nyingi Afrika kwa sababu mifumo yetu ya elimu haiandai vijana kuweza kufanya hivyo . Hata huko Magharibi kwenyewe vijana wanaachwa wajichagulie kwa sababu mifumo wao wa elimu na maisha kwa ujumla imewaandaa kutambua hizo 'dream' zao kwa kuzilinganisha na -'options' nyingine nyingi na hatimaye wanafanya uchaguzi wanaouelewa vizuri. Huwezi kumlinganisha A-level/college graduate wa Uingereza na wa hapa kwetu aliyemaliza shule ya kata huko mikoani. Kule kwa wenzetu kuna masomo ya 'career guidance' toka awali kabisa kuwezesha vijana kufanya maamuzi wanayoelewa vizuri hapo baadae. Hapa kwetu vijana wanaishia kushauriana wenyewe kwa wenyewe na wengi wanaishia kusaka ajira na vibahasha mitaani na wanakuja kujifunza fursa zingine baadae wakiwa wameshapoteza muda mwingi.
Yaani wewe unataka kijana apoteze muda kusoma akitegemea atakuwa 'lawyer' halafu baadae maisha yakimchapa mtaani ndio aanzishe 'business' ya kuuza mgahawa? Huko ndio ku - 'follow your dream'? Kwani kama angeshauriwa mapema kabisa kwamba asomee 'business' ili aanzishe biashara yake mwenyewe kwa sababu siku hizi lawyers hawana ajira za kutosha, kuna ubaya gani?