Nafikiria kumtoa mtoto IFM na kumpeleka chuo cha mifugo; waungwana mnashauri vipi?

Acha kumdanganya mwenzio mifumo ya elimu ya Tanzania 99% huwa tunategemea kuajiriwa mara baada ya kugraduate ni hitaji la mfumo wa elimu yetu wala si matakwa ya msomaji
ni kweli kabisa
 


Aisee umewaza vema sana. Binafsi nina elimu ya juu ila nawaza kwenda VETA kuchukua fani itakayoniwezesha nijiajiri mwenyewe.

Juzi kwenye mkutano wa maaskofu wa TAG na Mh. Rais Magufuli nilisikia wanasema wana mpango wa kujenga chuo kikuu dodoma.

Nawashauri tu viongozi wa TAG wafuate ushauri wa Mh. Rais kufungua kiwanda, na guvu nyingine wawekeze kwenye kujenga VOCATIONAL TRAINING COLLEGES ....Vyuo vya kati ni msingi mzuri sana kwa maendeleo ya taifa letu.

Najua serikali kupitia wizara ya elimu ina mikakati madhubuti juu ya vyuo vya kati....iende mbele kuviboresha na kuanzisha karakana nyingi zenye kubeba mirengo yote ya sayansi, uhandisi, usanifu na teknologia....hata ikiwezekana kuingia miktaba na labour force (expatriates but cheap toka Uchina, India, na Urusi) kukaa na vijana wetu kuwafunza kuanzia ukarabati, ku-assemble na kutengeneza vitu. Kwa hivi tunaweza jikuta tuna Sillicon Valley yetu ya aina yake.
 
ahsante mkuu!
 
Mkuu hiyo haiwezi kuwa sababu ya mtu kwenda kukaa chuoni miaka miwili, naamini mwisho wa siku naye ataingia tena mtaani kusaka ajira. Nakushauri acha dogo apige shule kama ni interest yake kusoma uhasibu. Hayo mengine ya kumuhamisha baadaye yanaweza kukuletea lawama huko mbeleni labda kama unasababu nyingine nyuma ya pazia. Huu upepo wa ajira utapita tu na akimaliza hapo uhasibu aendelee kufuga ila usiwe na ushawishi wa kumtoa hapo kwa kisingizio cha ajira. utaweza kuwa umemkosea sana huko mbeleni.
 
Amalize kwanza ifm ndio aende mifugo
 
marehemu mkapa alisemawakati Fulani kuwa elimu yetu tunahtaji mjadala mzito sana lakini nadhani hatukulitendea haki swala husika na bado liko chni ya uvungu tu

Kiukweli elimu ya juu kwa Tanzania imekuwa kama fashion tu...na ndio maana elimu inashuka kila uchao.

Kuna mzungu mmoja alishawahi mwambia Prof. mmoja wa Udsm (Mungu amlaze mahali pema peponi) kuwa Tanzania inahitaji kuwa na vocational training colleges sio universities...it was early 1990s.....wako waliomuona huyu mzungu ni beberu lenye wivu ila kuna ukweli mchungu ndani yake.

Tunatakiwa kuwa vyuo vya juu vichache vyenye kupokea na kuendeshwa na the top layer of cream of intellectuals. I come to realize that high learning is not for everyone, na maisha mazuri hayaletwi na elimu ya juu.
 

Watoto wanahitaji kuwa guided/mentored ili wafanye maamuzi sahihi kwa future yao. Elimu yetu haiwapi wanafunzi mwanga wakutosha wa maisha wanayoyaendea. Wengi wao wanamaliza shule/vyuo hawana 'exposure' na, kwa hiyo, hawana 'options' za kutosha kwenye kuamua maswala muhimu kama vile kuajiriwa vs kujiajiri. Siku hizi ukimuacha mwanao ajichagulie kulingana na 'interest' uwezekano wa yeye kupotea ni mkubwa sana. Utasikia 'nataka kuwa mhasibu, daktari, engineer n.k., lakini hajui vizuri maisha yakoje mtaani huku. Kama mzazi ana uelewa wa kutosha, kumchagulia mwanae course ya kusoma ni jambo la busara sana.
 
Kama ni skills tu si unaenda hizi short course kibao tena zimetengenezwa vizuri kabisa. Kwa nini upoteze miaka miwili ambayo mengine unayoyasoma wala hayakusaidii chochote. Nenda short kozi ambayo inakuwa ni mahususi kwa kile unachokitaka.
Yeah true
 
ni kweli kabisa
 
Unajua hapa tunamuongelea kijana ambaye yupo Chuo na Sio mtoto wa Chekechea ?, Kama mtu umefika mpaka form six haujajua unataka nini sio vibaya sana unaweza ukauliza au ukafanya research mwenyewe na kuangalia available options..., Ila kama unajua unataka kufanya nini hata kama upo Primary School (follow your Dreams)

Kumbuka kwenye maisha its not all about kipato (unaweza kupata kipato hata bila kusoma) kwenye maisha ni kuishi na kuishi ni kufanya kile unachokipenda..., haukatazwi ukiwa lawyer ukafungua mgahawa na ukapika na ukifungua mgahawa sio mpaka ujue kupika..., biashara inahitaji discipline, experience na uvumilivu (nikupe siri non of them are taught in school)..,

Basic business skills ni selling; buying/producing;reselling yaani investing and reinvesting hivyo ndivyo anavyofanya muuza nyanya mtaani mpaka Azam viwandani....., mimi ninayejua hizo theory huenda nisiweze kufanya hayo.. WHY? maybe I lack discipline.... (kwahio ndio maana mtu akija kununua product haulizi una cheti kipi) unless otherwise unachokiuza ni skills zako.., mfano Daktari, Muhasibu (kutoa services) au Services yoyote ile inayohitaji knowledge (thus you are selling your knowledge)

Pili Elimu knowledge haipatikani kwenye mashule tu hata experience ya kuuza karanga kwa miaka kumi hio ni shule tosha ambayo mtu fresh from school hana....
 
Watoto wasome elimu inasaidia pia kumfanya awe na confidence, msiwashauri waache kusoma, hata akijiajiri pia inatakiwa elimu.

Watoto wa miaka hii wanatakiwa wasome kweli

Nawashauri hata hawa wakwangu wenye digrii ya kwanza wakasome zaidi ila kwa hela zao.
 
Si ndiyo maana nimekuambia si wote.
Kuna Kaka nae amesoma vizuri tu..sasa hivi anatengeneza vipodozi vya kike anapiga pesa vibaya mno..wachache mnaothubutu
Mwanzoni nilikua mtu wa kuona nishai Sana (Bitozi Nyangema). Nikaanzaga Uber ila Mambo ya rating nikashindwa nikaja kufungua Banda la kitimoto na bia hapa kwangu Kerenge silipi Kodi Wala nn
 
Mwanzoni nilikua mtu wa kuona nishai Sana (Bitozi Nyangema). Nikaanzaga Uber nikaanzaga Uber ila Mambo ya rating nikashindwa nikaja kufungua Banda la kitimoto na bia hapa kwangu Kerenge silipi Kodi Wala nn
Inapendeza sana..
 
Kufuta ujinga inatosha.hizo elimu za juu tuwaachie walimu na maprofesa
 
Tuna mdogo wetu wa kike hajafaulu vizuri sana ila hataki tena kusoma na kasema anapenda kujifunza kushona awe fundi.
Mpelekeni ufundi itamsaidia Sana..ingawa ajitahidi huko mbeleni arudi shule
 
Hivyo vyuo vya vocational vikiwa vingi na demand ya wahitimu si itapungua!Issue ni kuwa nchi ijenge mifumo imara ya uchumi.
 
Elimu ya ngazi ya kati ni rahisi kuipata kwa mhitimu wa chuo kikuu.Usimtoe,mwache amalize
 
Kwa jicho la mbele 10+ mwache amalize degree.Hata akitaka kuingia ktk siasa anakidhi,ktk kampuni napo atakidhi. Njoo pm nikupe maujanja anayotakiwa kufanya akiwa hapo chuo, kama utamwezesha na bongo yake Ilinafanya kazi at a jutia.
 
yeye mwenyewe anasemaje ?

Kufuga vikuku vinne na vimbuzi na kuanzisha mradi mpaka usomee mifugo ?
Tukubaliane kutofautiana kitu kinachofanywa na mtaalam si sawa na asiyejua. Infact wengi hukosa kufanikiwa kwa kufikiri kuwa kufuga vikuku vinne na vimbuzi haihitaji utaalam
 

Umemuuliza mtoto hobby au malengo yake ni yapi? Tanzania hii sasa hivi inahitaji skilled financial management personnel kuliko kipindi chochote tangu awamu ya tatu. Na skilled bookkeeper tu (achana na CPA) hawezi kukosa kazi hata sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…