NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

Hiyo ni feature tu ya app logic behind ni kwamba video unaitazama ukitoka kwenye app ya kutazama inajipause mpaka urudi.

Feature ya app gani, youtube ?

Youtube kwenye android inaweza kuwaka wakati unafanya vitu vingine. Kwa hiyo, hiyo ya kufanya jambo moja kwa wakati sio feature ya app, bali ni feature ya Iphone! Feature ya hiyo A15 BIONIC

Processor kali kuliko zote duniani lakini ukiwasha kitu lazima uzime kitu, then what’s the point of being “most powerful”?
 
Ni feature ya Youtube app ya iPhone. Ufanyaji kazi wa app za iPhone na android ni tofauti wana approach tofauti kuanzia graphics mpaka utendaji kazi.
Unatumia iPhone gani wewe maana unalalamika vitu ambavyo havipo. Yes, bionic A15 ni powerful processor imeirithi bionic A14.
Mengine ni implimentation, ndio maana mpaka leo Apple hajawahi ruhusu tablet zipige simu na alipoona watu wanazihack zinapiga simu kwenye tablet zake za zamani, akaacha tumia same chip ambazo zinasupport simu akaanza weka chip ambazo hazisupporr calls.
Video kazi ni kutazama sio kusikiliza ukiondoka kwenye app ya video inabidi ijipause.
 


Tutafute hela tu mjomba..Eti kwamba ubora wa camera ya Iphone 13 Pro ni sawa na simu ya laki 2??
 
Ila kitu kikiwa kwenye icloud sometime hata nikisahau flash nakivuta tu kwenye simu na simu ikiwa imezima nakivuta tena kupitia kwenye PC kwa kuwa ninakuwa doc zangu nimezifanyia arrangement flan hivi

Nimependa "keep data local" ila usiwe local ukapitiliza maana hata mwenye iPhone anaweza akaweka kwenye SD Card kumbuka 5gb free storage ya icloud na nilisema hapo juu kwamba kuna option ya ku-share doc kwa iPhone na PC kwa sekunde chache tu hivyo ukiona hutaki kununua unakuwa unazi-save document zako kwenye PC kwa utaratibu wa kawaida huku kwenye icloud unaacha space ya kutosha kwenye 5GB zako za kitonga.
 
hii ni point kubwa sana, wacha niingize
 
upele umepata mkunaji hapa
 
maji ya kilimajaro tunayoyapenda ni buku, maji ya dew drop ni buku, maji ya mkwawa ni buku, maji ya dasani ni buku....

-hustuki hapo kwamba kuna ushindani tofauti na iphone asietaka ushindani kwa kuibania os yake?

-nitaftie maji yanayouzwa buku 3 bei juu kama iphone yanayoizidi kilimanjaro tunayolipia thamani yake kama android ?

-cha kukushauri nenda hata kwa mwanafunzi wa form 5 anaesomea hge akufundishe masoko kabla hujakurupuka kuandika usivyovijua.
 
Tutafute hela tu mjomba..Eti kwamba ubora wa camera ya Iphone 13 Pro ni sawa na simu ya laki 2??
Full stop. Nimekuelewa ndugu yangu kitu chochote kizuri au kitamu lazima kiwe na thamani tutafute ela.😂 Ni sawa na kufananisha dagaa mwanza na nyama ya ng'ombe au kuku ziwe bei sawa.
Exactly....hizi nguvu kubwa tunatumia ni umaskini tu.

Naona mmejiunga kumsifia iphone ana kamera nzuri, basi wacha niwakusanye niwape makavu.

Nataka niwajuze tu kwamba hio iphone 13 pro max, kwenye ipande wa camera inakimbizwa na simu nyingi tu za androd, mfano google pixel 6.

Android tunalipia thamani, sio bei ya monopoly anaetengeneza simu kwa laki 8 anaziuza milioni 3 na nusu 🤣
 
Hivi Pixel 3xl ni nzuri hii...vipi kwenye upande wa chaji mkuuu....nataka ninunue hii
 
Hivi Pixel 3xl ni nzuri hii...vipi kwenye upande wa chaji mkuuu....nataka ninunue hii
Ni simu nzuri sana hizo hasa kwenye kamera wapo vizuri tangu kitambo

naona kuna uzi maalum

 
Hatutaki kupitia ICLOUD iliyopo Marekani tunapotaka ku access data zetu na kubadilishana hapa Makete. Tunatumia SD Card na flash zinazouzwa hapa stendi. That is for the vast majority of the minimalist masses of us.

Hatuna bundles za kuchezea, na hatuna minara kila tarafa, na hatuna broadband connectivity kila nyumba. Hatuwezi ku justify, hatuna hoja na haja ya status symbol Apple phones, Apple icloud and Apple stores.

Again, we keep data local, here at Makete Stendi.
 


Nakubaliana nawe kuwa kwa benchmarks tofauti tofauti, some android phones zinaishinda Iphone kwenye baadhi ya vigezo vya ubora wa picha.

Ubora wa Iphone 13 Pro Max unapatikana kwenye consistency ya camera yake na zaidi ubora wa video. Jaribu kucheki renowned reviewers kama MKBHD, Lew (Unbox therapy), Dave2D na MrWhoistheBoss.

lastly, simu za android zinazoweza leta upinzani ni flagships only kama Samsung S22 Ultra na mwisho wa siku inategemea zaidi na personal preferences.

Buy flagship kuanzia Sony, Huawei na Samsung na camera zake zitakuwa almost the same na tofauti pekee itakuja kwenye your personal preferences only.
 
Nakazia
 
Ubora wa Iphone 13 Pro Max unapatikana kwenye consistency ya camera yake na zaidi ubora wa video. Jaribu kucheki renowned reviewers kama MKBHD, Lew (Unbox therapy), Dave2D na MrWhoistheBoss.
Yote kwa yote ni kwamba Iphone 13 pro max hafui dafu wala hakaribii mbele ya mashine kama pixel 6, anakaa chini vizuri kabisa,

lastly, simu za android zinazoweza leta upinzani ni flagships only kama Samsung S22 Ultra na mwisho wa siku inategemea zaidi na personal preferences.
Post imeshaweka wazi hapo zaidi ya vitu 20 iphone kapigwa kanzu na android, hakuna upinzani hapo bali kuna kuburuzwa,
Buy flagship kuanzia Sony, Huawei na Samsung na camera zake zitakuwa almost the same na tofauti pekee itakuja kwenye your personal preferences only.
Yes, lakini nakukumbusha tu kwamba iphone sio simu yenye kamera bora kama wengi wanavyo danganyika, kuna wababe wa android wanamkalisha
 


Naomba twende kwa facts mkuu...nakuwekea hapa link ya DXOMark na screenshot yao kuonesha camera scores.

Naomba na wewe uweke yako twende sawa.....https://www.dxomark.com/smartphones/

 
Naomba twende kwa facts mkuu...nakuwekea hapa link ya DXOMark na screenshot yao kuonesha camera scores.

Naomba na wewe uweke yako twende sawa.....https://www.dxomark.com/smartphones/

View attachment 2176718
Kwahio iphone na kelele zote zile ni ya 5 😂😂.

Kwangu binafsi nmewahi cheki review, google pixel 6 ni mashine nyingine,
 
Umekazia, na mimi nakaza.

Nilikuwa kwa kinyozi akapiga miziki mikali nikadhani labda ipo Spotify, au Icloud au Amazon Music, au sijui XM Satellite. Nikamwambia nazipataje hizo ngoma Kiongozi ?

Akasema ziko kwenye flashi hapa hapa saluni. Hakuna mtu analipia ma iCLOUD na ma SPOTIFY viunga hivi. We have higher priorities on spending. Data zetu haziko kwenye servers San Fransisco mjini.

Tunatunza data zetu hapa hapa Makete Stendi.

For the overwhelming majority of us, our phones are powered by Android, the gold-standard of everything open-source.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…