Mult tasking
Unaandika sms huku unafanya hesabu kwa calculator huku unaangalia video huku unasoma PDF.....[emoji23][emoji23][emoji23]
I reserve my comment
No headphone jack
Hii ndio habari ya dunia kwa sasa sema ni vile haufahamu umezoea kutumia simu za kichovu
Simu zote za kampuni nguli kwenye Flagship zao wamemfuata Apple hawana hizo takata za mashimo
Wingi wa Apps
Tatizo huwa sio wingi wa App bali ni UBORA wa Apps
Appstore kuna apps zote MUHIMU na BORA Duniani
Playstore kuna app muhimu na mataka taka kibao
Multi user
Simu ni a very private thing, huu ushamba wa simu moja kutumia ukoo mzima ni USHAMBA..... not a big deal
Free internet
Unasifia UHALIFU hadharani kwamba ni sifa ya simu?
Huo ni udhaifu wa Simu na Os kwamba zina ruhusu watu kufanya uhalifu
No Memory card
Tunarudi pale pale, hii ni kutokana na kutumia low budget phones
Flagship zote za kibabe hazina hiyo takataka zimemfuata Apple
Bei ghali
Bado tupo pale pale, swala la bei ghali ni kutokana na level zako za kipato na simu unayotumia
Iphone kwa kiasi kikubwa wanatengeneza High-end phone ambazo zipo daraja moja na Flagship za manguli wa Android phones na bei wakati mwingine iphone anasubiri
Files
Huo ugumu unao usemea ni upi mkuu
Unaweza kutuma na kupokea file lolote na ukalifungua kwa Whatsap, Telegram, email, Messenger, Xender nk
No Radio Fm
Tupo pale pale
Flagship zote za kibabe zimemfuata Iphone hazina FM Radio
User interface
Haya mambo ya “kitoto kitoto” hayana nafasi kwenye simu classic
Always on
Watumiaji wa iphone muda wanaangalia kwenye saa ya mkononi sio unataka kuangalia saa unachomoa lisimu mfukoni kuangalia eti saa ngapi
Ikitokea ulazima wa kutumia simu si unakandamiza tu home button
Ringtones
Aliyekudanganya huwezi kuweka ringtones unazotaka ni nani?
Jailbrake
Ukiona unahangaika na jailbrake ujue iphone sio kaliba yako
Kanunue Tecno
Nimejibu kama mtani wa jadi [emoji23]