NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

Ni wachache ndio maana hiyo sony haiko hata kwenye top 10 ya kampuni zinazoongoza kwa mauzo.
iPhone haijawahi kuwa na memory card toka wameanza tengeneza na imekuwa iko top 3 kwa mauzo na hapo anauza highend phones.
Na wengine wamefuata hawana memory card kama yeye.
Iphone haijawahi kuwa na betri la kutoa mwanzo waliisema wee, sasa hivi karibu simu zote highend na low end kampuni almost zote hazina betri la kubandua mfuniko na kutoa.
Iphone kaondoa earphone jack, mwanzo hadi samsung walitoa tangazo la kuimock, sasa almost highend phones zote zinafuata hivyo.
Hata mleta mada sidhani kama ana highend phone ya recently na kama anayo haiwezi kuwa hiyo sony maana hata hawezi kuafford kuinunua hiyo sony ni ghali sana, maana tayari ashalalamika bei huko juu.
mleta mada haelewi chochote.
 
iphone ndo simu ambayo huwezi kubadili account, ambayo ni icloud. hata ufanyeje hutaitoa labda ubadili hardware.
Mkuu haupo serious, japokuwa me situmii iPhone Ila najua kama unaweza kuchange iCloud account, labda uelezee unaongelea kuchange kivipi?

Watu wanauziana iPhone na wanachange iCloud account, hayo Mambo ya kurithi iCloud account ya mwenzio km mikoba ya uchawi ilikuwa Mambo ya kizamani

Me Kwa macho Yangu nimeshuhudia watu wanachange iCloud account, inawezekana wewe ndio umebakia hujajua wenzio wanafanyaje, inabidi ufanye ku update knowledge yako juu ya Hilo Jambo Mkuu
 
i cloud inakupa gb 5 bure na hii ndio wabongo wengi wameizoea, sasa vuta picha una files zako gb 200 huko, zitatosgha huko i cloud ? hata kama mtu kanunua space ya i cloud atalazimika tena kununua bando la laki 2 hapo kufanya backup tena itabidi asubirie hata masaa 7 ili kupandisha hizo gb 200..

ukiwa na memory card yako unahamisha fasta tu

Kwani lazima kuhamisha kwenye memory card?
Kompyuta zi zipo
 
nikilipia hii natumia internet mwaka mzima ndani ya iPhone

6EEA0E84-1030-4FF4-8B25-5A59C17CCB6E.png
 
Mkuu haupo serious, japokuwa me situmii iPhone Ila najua kama unaweza kuchange iCloud account, labda uelezee unaongelea kuchange kivipi?

Watu wanauziana iPhone na wanachange iCloud account, hayo Mambo ya kurithi iCloud account ya mwenzio km mikoba ya uchawi ilikuwa Mambo ya kizamani

Me Kwa macho Yangu nimeshuhudia watu wanachange iCloud account, inawezekana wewe ndio umebakia hujajua wenzio wanafanyaje, inabidi ufanye ku update knowledge yako juu ya Hilo Jambo Mkuu
namaanisha ikiibiwa au kupotea haibadilishiki, nilikosea kidogo kwenye kuandika
 
namaanisha ikiibiwa au kupotea haibadilishiki, nilikosea kidogo kwenye kuandika
Ok, nimekupata ila ata hapo pia kuna utofauti Sana na zamani, Mzee wangu Mie anatumia iPhone 8 na alisahau password za iCloud akahangaika Sana bila mafanikio na simu ilikuwa na Mambo yake muhimu Sana ya biashara, kishingo upande ikabidi aiweke Tu ndani almost 7months

Siku moja yupo job, akawa anashea na mtu kuhusu kupoteza vitu muhimu kwenye simu baada ya kushindwa kufungua iPhone yake, jamaa akamwambia me nawajua watu wanaweza kufungua, Mzee akabisha Jamaa akamwambia Kesho njoo nayo pamoja na laki 2

Kesho yake mshua akampelekea Yule mtu simu na laki 2,akataka nayeye aende pamoja na mshkaji ila Yule jamaa akasema hawa watu hawataki kujulikana we kaa Tu usubiri simu yako, baada ya km masaa 3 simu ikarudi imefunguka, na ndio anatumia tena Hadi saizi
 
ANDROID INAWEZA KUFANYA ZAIDI YA KITU KIMOJA KWA MPIGO (Multi tasking)

View attachment 2167558

kufanya shughuli Zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho hakipo kwenye iphone, mfano kwenye iphone ukiwa kwenye video call halafu ukahamia kwenye app nyingine basi video call ndio kwa heri, Android unaweza kutumia apps hata 10 kwa mpigo, uzuri ni kwamba kwenye android kuna split screen ambayo unaweza kuseti screen ijigawanye vyumba vitatu kwa shughuli unazofanya na hii unaikuta ndani ya simu, kwa iphone haiji kwenye simu labda ujiongeze sana uwe mtundu mtundu.

KWENYE IPHONE HAKUNA TUNDU LA KUCHOMEKA EARPHONES
View attachment 2166337

hakika huu uamuzi haukuwa na maana, ni uamuzi uliofanyika kibiashara zaidi bila kujali mahitaji ya wateja, kitu walichofanya ni kulazimisha wateja kununua wireless earphone zao au kama watahitaji kutumia earphone za waya basi wanunue kiunganishi chao cha ziada. Kwa android uchagyzi ni wako uamue kutumia za waya au wireless, binafsi headphone za waya zimewahi kunisaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia kuna Rafiki yangu alitaka kuibiwa simu, ilipovutwa alistuka mwizi akakimbia.

IPHONE IMEPIGWA GEPU REFU KWENYE APPS
View attachment 2166329

Sio siri wala kitu cha kubishana, Android kuna apps nyingi sana kuliko Iphone, Sababu kuu ni kwamba ili kuweka app kwenye playstore ya android gharama yake ni elf 50 mara moja tu lakini kwa upande wa iphones kuweka app kwenye apple store ni laki 2 unalipia kila mwaka, pia kwenye android unaweza kudownload na ku install apps ambazo hazipo playstore.

SIMU YA ANDROID YAWEZA KUTUMIKA NA MTU ZAIDI YA MOJA (Multi user)
View attachment 2166326

Hii inaitwa multiple user, simu inaweza kutumika na Zaidi ya mtu moja bila kuingiliana taarifa, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k, utampa simu aitumie bila wasi wasi. simu muhimu ikipigwa unaweza kuseti iite ili akuletee, ukimaliza maongezi unampa simu akaendelee. Unaweza kutengeneza hata accounts 4 za watu tofauti zitumike ofisini. Kwa iphone hawana hii.

ANDROID UTATUMIA INTERNET BURE BILA BANDO
View attachment 2166352

Hapa ndo napopenda aisee! mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, hizo mambo za kujibana hazipo huku android kwenye apps kibao kama ha tunnel, napster, n.k. unacheza tu na settings unaanza kuserereka, unaweza kushusha hata gb 20 kwa siku na wala isiwe habari lakini kwa iphone itabidi ununue kifurushi cha elf 30 ili upate hizo gb, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone matoleo mapya pale mlimani city mtu haoni taabu kulipia milioni 3 na hio simu anaiweka mfukoni, ishu ni hawa ambao wanaokwepa panga la bei kali kwa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.

IPHONE HAINA MEMORY CARD
View attachment 2166333

Iphones hazina memory card, Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ikaleta changamoto kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card , Lakini pia simu inaweza kuwa na gb 500 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card maana funguo mbili za gari ni bora kuliko moja, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ukapoteza kila kitu, ila kama ilikuwa na memory card, hata ikidondoka utachomoa memory card utakuta mafaili yako, hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako, unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu.

BEI
View attachment 2166316

Bei kali ya simu ya iphones ni kwa sababu ya kampuni ya apple kucheza na akili za watu kwenye branding, Kwenye swala zima la bei wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” kwa mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta kuna t shirt zenye ubora wa hali ya juu zinauzwa elf 20 lakini nyingine zina ubora wa kati zinauzwa elf 60, ukiuliza kwanini unaambiwa kwasababu ina nembo ya Nike, Gucci, n.k. wanacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu kwa kununua bidhaa hio, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones pale mlimani city, wengi hawana pesa kwa hio wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished), wengi zaidi hupendelea matoleo ya nyuma zaidi ili kupunguza makali ya bei (umelipenda boga kwanini uchukie maua yake ?), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la pili Mid range mfano OnePlus 8T, daraja la bajeti hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imekamata soko kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.

NI SHUGHULI PEVU KUPERUZI / KUHAMISHA MAFAILI YA IPHONE
View attachment 2166322

huku android tunatumia file managers tunaona mafaili yote kirahisi kwenye folders lakini system ya iphones haishirikiani kwenye kushare storage na apps kirahisi hivyo inakuwa ngumu kuperuzi mafaili yako, Hali inakuwa mbaya zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi, Mimi naweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android nikifika stationary nachomeka fasta tu naprint file, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes, na hapo inabidi anunue bando ili kudownload hio software, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.

IPHONE HAINA RADIO
View attachment 2166334

Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. Nikiwa na android yangu hata kile kipindi cha uchaguzi internet ilivyokatwa niliweza kuendelea kusikiliza vipindi vya redio navyovipenda.

MIPANGILIO YA MUONEKANO IMEBANWA SANA IPHONE
View attachment 2166317

Kwenye iphones kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa gepu refu sana kwasababu android unaweza kuweka launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako, utaweza kujipangilia icon kwa kuweka unazotaka wewe, kuzifinya na kuzitanua, n.k kucheza na elements zozote utakavyo kwenye home screen, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe commands, scrolling effects, lock screen customization, n.k. kuna vitu vichache kama widgets vimeongezewa kwenye iphone mwaka 2020 toleo a ios 14 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo, ajabu ni kwamba hapo zamani watumiaji wa iphones walikuwa wanadai wdgets za android zilikuwa hazina maana ila walipowekwa kwenye iphones wakaanza kuzisifia, kwa hakika sizitaki mbivu hizi.

IPHONE HAINA ALWAYS ON DIPLAY
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana ukitumia hii feature, Hadi sasa hii feature muhimu haipo kwenye iphones officially.


IPHONE WANACHELEWA SANA KUWEKA MAHITAJI YA WATEJA
View attachment 2166343

Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september, Tukija kwenye widgets za homescreen, iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo kitambo sana.

HUWEZI KUSETI RINGTONE UNAYOTAKA KWENYE IPHONE
View attachment 2166320

Ili kuseti ringtone yako kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari, utaweza kuweka mziki wowote uwe ringtome. kwenye iphones hii kitu hakuna, ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload app ya garageband, uingize mziki kwenye app, ufanye ku save ndio utaweza kuset hio ringtone, shida yote ya nini hii jamani? Hii ndio sababu wengi simu zao zina ringtone ile inalia kama vingoma vya Watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.

CAMERA
View attachment 2166341

kamera zimeboreshwa sana kwa simu zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kanera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali tu, hizi ishu za kamera nadhani kwa sasa zipewe kigezo chepesi maana teknolojia ya kamera imekuwa mno, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda sitashangaa simu za elf 80 zikitoa picha kali sana.

ULINZI
View attachment 2166338

Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand ni simu yenye ulinzi kamili walipoombwa kiroho safi waifungue wenyewe simu ya gaidi ila wakakataa, wataalam wakaingia kazini wakaifungua chapchap bila msaada, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. Pia nawakumbusha sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza nywila zako utadukuliwa tu, n.k.

JAIL BREAKING (IPHONE) v/s ROOTING (ANDROID)
View attachment 2166335

Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.


Ohhh mambo ni mengi sana jamani, wacha niishie hapa nisije wachosha zaidi
Nimesoma yote, sina cha kukosoa ila cha kuongezea labda unge tuma na ubora wa ios ndipo tuweke mlingano wake.

Mfano kwenye muonekano, hardware nk maana kwenye maelezo yako umegusia camera mabayo sizan kama ipo kwenye upande wa os .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok, nimekupata ila ata hapo pia kuna utofauti Sana na zamani, Mzee wangu Mie anatumia iPhone 8 na alisahau password za iCloud akahangaika Sana bila mafanikio na simu ilikuwa na Mambo yake muhimu Sana ya biashara, kishingo upande ikabidi aiweke Tu ndani almost 7months

Siku moja yupo job, akawa anashea na mtu kuhusu kupoteza vitu muhimu kwenye simu baada ya kushindwa kufungua iPhone yake, jamaa akamwambia me nawajua watu wanaweza kufungua, Mzee akabisha Jamaa akamwambia Kesho njoo nayo pamoja na laki 2

Kesho yake mshua akampelekea Yule mtu simu na laki 2,akataka nayeye aende pamoja na mshkaji ila Yule jamaa akasema hawa watu hawataki kujulikana we kaa Tu usubiri simu yako, baada ya km masaa 3 simu ikarudi imefunguka, na ndio anatumia tena Hadi saizi
Sio kama nabisha
Lakini naamini hizi ni hadithi za kusadikika

Kuna iphone 6+ moja na 7 tatu na na iphone x moja tumehangaika nazo weee hakuna aliyeweza kuzifungua

Hao jamaa wanatakiwa kutengeneza pesa ndefu sana
Nipe connection nifanye nao kazi
Najua chimbo la iphone bei bwerere ambazo zipo iCloud locked nizinunue jamaa wanifungulie kwa 200k nipige hela
 
Sio kama nabisha
Lakini naamini hizi ni hadithi za kusadikika

Kuna iphone 6+ moja na 7 tatu na na iphone x moja tumehangaika nazo weee hakuna aliyeweza kuzifungua

Hao jamaa wanatakiwa kutengeneza pesa ndefu sana
Nipe connection nifanye nao kazi
Najua chimbo la iphone bei bwerere ambazo zipo iCloud locked nizinunue jamaa wanifungulie kwa 200k nipige hela
Mkuu Una haki ya kudhania kwamba ni hadithi za kusadikika ata Mie nilikuwa naamini hivo, Hadi pale mtu ambae nipo nae yalipomkuta namie kama kijana wake nikatembea na simu hiyo weeee bila msaada, nikamrudishia mwenyewe

sio kama me sitaki kupata hizo connection za huyo jamaa, nahitaji Sana maana najua kuna pesa, Ila Mzee alizingua kunipa direct info kulingana na terms alizopewa na mshkaji, niliishiia Tu kuangalia simu ya Mzee ikiwa uchi na mazaga yake yapo, kilichofanya niandike hapa ni kuongeza hamasa Kwa walio interested na hizo Mambo wasikate Tamaaa coz inawezekana

Kwa nyie ambao mpo karibu na watu wanaodeal na iPhone basi fanyeni utafiti wenu vizuri, trust me brother kuna watu wanafungua, na naamini kuna watu wanawajua hao crackers ni kina nani ila wanafanya Tu privacy

nilichogundua wanafungua Kwa mpunga mrefu inategemea na umuhimu wa vitu vilivomo kwenye simu, Mzee alitoa laki 2 ni Kwa sababu anajuana na huyo aliempelekea simu, coz jamaa alibenefit kibiashara kupitia hiyo issue

Bahati mbaya siwezi kuthibitisha hii tofauti na maelezo yangu, ila atakaeamua kuniamini aamini na kisha ajikite kwenye kutafuta ukweli wa Mambo, na atakaeamua kuona kama ni uzushi fresh Tu, it doesn't cost me a damn Thing
 
namaanisha ikiibiwa au kupotea haibadilishiki, nilikosea kidogo kwenye kuandika
Uwe unatulia wakati unaandika, naona ulikuwa ume panic so ukaja kuitetea iphone kwa kukurupuka (utani)

Hizo iphone ulinzi wake ni 1 na 0 na siku zote kwenye ulimwengu wa computer hakunaga ishu isiyopenyeka inayokuwa na 1 na 0.

Hizo iphone kuna kipindi iliwahi kukamatwa ya gaidi aliekataa kutoa loki, polisi kwa roho safi wakaenda kampuni ya apple kuomba waiotoe wenyewe ila wakakataliwa, ikabidi wao wenyewe wacheze nayo wakaifungua chap chap tu 😂😂

kuna software kama itoollab, passfab, iN-Box, n.k zinaweza haya mambo ila ni uhalifu kufanya hivi ndio maana mafundi simu wengi hawataki kutoa hii huduma.
 
Tuhitimishe tu kwa kusema Android phones nyingi nikwajili ya sisi masikini.

Huwa najaribu kutafakari Apple wanatoa simu za hadhi ya juu pekeake hawana matolea ya bei ndogo kwajili yetu walalahoi ila bado inashindana na kina Samsung ambao wanatengeneza simu za hadhi ya juu na matakataka mengine kibao ambayo wengi ndo tunayatumia
 
Ishu sio ulazima, Ishu ni kwamba iphone HAIWEZI

Sio kila mtu ana computer
Na sio kila mtu ana memory card

Akili ya kawaida tu inakataa kufanya backup ya simu kwenye SD card badala ya Computer
Watu makini wanafanya backups zao kwenye computer au online na sio SD card ambayo ni rahisi kupotea na rahisi sana ku corrupt mazima
 
Ishu sio ulazima, Ishu ni kwamba iphone HAIWEZI

Sio kila mtu ana computer
Na sio kila mtu ana memory card

Akili ya kawaida tu inakataa kufanya backup ya simu kwenye SD card badala ya Computer
Watu makini wanafanya backups zao kwenye computer au online na sio SD card ambayo ni rahisi kupotea na rahisi sana ku corrupt mazima
 
Back
Top Bottom