NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

i cloud inakupa gb 5 bure na hii ndio wabongo wengi wameizoea, sasa vuta picha una files zako gb 200 huko, zitatosgha huko i cloud ? hata kama mtu kanunua space ya i cloud atalazimika tena kununua bando la laki 2 hapo kufanya backup tena itabidi asubirie hata masaa 7 ili kupandisha hizo gb 200..

ukiwa na memory card yako unahamisha fasta tu
Mbona kuna option ya ku-share files zako na PC bila itune yaani naweza nikatengeneza folders kwenye iCloud drive na nikifungua PC nakuta zile files muda huo huo na uki-save files kwenye PC wakati huo huo unalikuta kwenye iPhone, shida yetu sie Watz tunatumia simu kama mbadala wa PC na ndio maana tunalilia sana na watu wanaomilki simu za iPhone wakati ukweli simu ni kifaa saidizi mpaka mtu amenunua iPhone maana yake ana vifaa vingine vya ziada ambavyo vipo linked na simu yake
 
ANDROID INAWEZA KUFANYA ZAIDI YA KITU KIMOJA KWA MPIGO (Multi tasking)

View attachment 2167558

kufanya shughuli Zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho hakipo kwenye iphone, mfano kwenye iphone ukiwa kwenye video call halafu ukahamia kwenye app nyingine basi video call ndio kwa heri, Android unaweza kutumia apps hata 10 kwa mpigo, uzuri ni kwamba kwenye android kuna split screen ambayo unaweza kuseti screen ijigawanye vyumba vitatu kwa shughuli unazofanya na hii unaikuta ndani ya simu, kwa iphone haiji kwenye simu labda ujiongeze sana uwe mtundu mtundu.

KWENYE IPHONE HAKUNA TUNDU LA KUCHOMEKA EARPHONES
View attachment 2166337

hakika huu uamuzi haukuwa na maana, ni uamuzi uliofanyika kibiashara zaidi bila kujali mahitaji ya wateja, kitu walichofanya ni kulazimisha wateja kununua wireless earphone zao au kama watahitaji kutumia earphone za waya basi wanunue kiunganishi chao cha ziada. Kwa android uchagyzi ni wako uamue kutumia za waya au wireless, binafsi headphone za waya zimewahi kunisaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia kuna Rafiki yangu alitaka kuibiwa simu, ilipovutwa alistuka mwizi akakimbia.

IPHONE IMEPIGWA GEPU REFU KWENYE APPS
View attachment 2166329

Sio siri wala kitu cha kubishana, Android kuna apps nyingi sana kuliko Iphone, Sababu kuu ni kwamba ili kuweka app kwenye playstore ya android gharama yake ni elf 50 mara moja tu lakini kwa upande wa iphones kuweka app kwenye apple store ni laki 2 unalipia kila mwaka, pia kwenye android unaweza kudownload na ku install apps ambazo hazipo playstore.

SIMU YA ANDROID YAWEZA KUTUMIKA NA MTU ZAIDI YA MOJA (Multi user)
View attachment 2166326

Hii inaitwa multiple user, simu inaweza kutumika na Zaidi ya mtu moja bila kuingiliana taarifa, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k, utampa simu aitumie bila wasi wasi. simu muhimu ikipigwa unaweza kuseti iite ili akuletee, ukimaliza maongezi unampa simu akaendelee. Unaweza kutengeneza hata accounts 4 za watu tofauti zitumike ofisini. Kwa iphone hawana hii.

ANDROID UTATUMIA INTERNET BURE BILA BANDO
View attachment 2166352

Hapa ndo napopenda aisee! mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, hizo mambo za kujibana hazipo huku android kwenye apps kibao kama ha tunnel, napster, n.k. unacheza tu na settings unaanza kuserereka, unaweza kushusha hata gb 20 kwa siku na wala isiwe habari lakini kwa iphone itabidi ununue kifurushi cha elf 30 ili upate hizo gb, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone matoleo mapya pale mlimani city mtu haoni taabu kulipia milioni 3 na hio simu anaiweka mfukoni, ishu ni hawa ambao wanaokwepa panga la bei kali kwa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.

IPHONE HAINA MEMORY CARD
View attachment 2166333

Iphones hazina memory card, Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ikaleta changamoto kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card , Lakini pia simu inaweza kuwa na gb 500 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card maana funguo mbili za gari ni bora kuliko moja, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ukapoteza kila kitu, ila kama ilikuwa na memory card, hata ikidondoka utachomoa memory card utakuta mafaili yako, hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako, unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu.

BEI
View attachment 2166316

Bei kali ya simu ya iphones ni kwa sababu ya kampuni ya apple kucheza na akili za watu kwenye branding, Kwenye swala zima la bei wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” kwa mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta kuna t shirt zenye ubora wa hali ya juu zinauzwa elf 20 lakini nyingine zina ubora wa kati zinauzwa elf 60, ukiuliza kwanini unaambiwa kwasababu ina nembo ya Nike, Gucci, n.k. wanacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu kwa kununua bidhaa hio, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones pale mlimani city, wengi hawana pesa kwa hio wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished), wengi zaidi hupendelea matoleo ya nyuma zaidi ili kupunguza makali ya bei (umelipenda boga kwanini uchukie maua yake ?), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la pili Mid range mfano OnePlus 8T, daraja la bajeti hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imekamata soko kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.

NI SHUGHULI PEVU KUPERUZI / KUHAMISHA MAFAILI YA IPHONE
View attachment 2166322

huku android tunatumia file managers tunaona mafaili yote kirahisi kwenye folders lakini system ya iphones haishirikiani kwenye kushare storage na apps kirahisi hivyo inakuwa ngumu kuperuzi mafaili yako, Hali inakuwa mbaya zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi, Mimi naweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android nikifika stationary nachomeka fasta tu naprint file, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes, na hapo inabidi anunue bando ili kudownload hio software, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.

IPHONE HAINA RADIO
View attachment 2166334

Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. Nikiwa na android yangu hata kile kipindi cha uchaguzi internet ilivyokatwa niliweza kuendelea kusikiliza vipindi vya redio navyovipenda.

MIPANGILIO YA MUONEKANO IMEBANWA SANA IPHONE
View attachment 2166317

Kwenye iphones kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa gepu refu sana kwasababu android unaweza kuweka launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako, utaweza kujipangilia icon kwa kuweka unazotaka wewe, kuzifinya na kuzitanua, n.k kucheza na elements zozote utakavyo kwenye home screen, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe commands, scrolling effects, lock screen customization, n.k. kuna vitu vichache kama widgets vimeongezewa kwenye iphone mwaka 2020 toleo a ios 14 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo, ajabu ni kwamba hapo zamani watumiaji wa iphones walikuwa wanadai wdgets za android zilikuwa hazina maana ila walipowekwa kwenye iphones wakaanza kuzisifia, kwa hakika sizitaki mbivu hizi.

IPHONE HAINA ALWAYS ON DIPLAY
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana ukitumia hii feature, Hadi sasa hii feature muhimu haipo kwenye iphones officially.


IPHONE WANACHELEWA SANA KUWEKA MAHITAJI YA WATEJA
View attachment 2166343

Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september, Tukija kwenye widgets za homescreen, iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo kitambo sana.

HUWEZI KUSETI RINGTONE UNAYOTAKA KWENYE IPHONE
View attachment 2166320

Ili kuseti ringtone yako kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari, utaweza kuweka mziki wowote uwe ringtome. kwenye iphones hii kitu hakuna, ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload app ya garageband, uingize mziki kwenye app, ufanye ku save ndio utaweza kuset hio ringtone, shida yote ya nini hii jamani? Hii ndio sababu wengi simu zao zina ringtone ile inalia kama vingoma vya Watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.

CAMERA
View attachment 2166341

kamera zimeboreshwa sana kwa simu zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kanera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali tu, hizi ishu za kamera nadhani kwa sasa zipewe kigezo chepesi maana teknolojia ya kamera imekuwa mno, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda sitashangaa simu za elf 80 zikitoa picha kali sana.

ULINZI
View attachment 2166338

Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand ni simu yenye ulinzi kamili walipoombwa kiroho safi waifungue wenyewe simu ya gaidi ila wakakataa, wataalam wakaingia kazini wakaifungua chapchap bila msaada, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. Pia nawakumbusha sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza nywila zako utadukuliwa tu, n.k.

JAIL BREAKING (IPHONE) v/s ROOTING (ANDROID)
View attachment 2166335

Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.


Ohhh mambo ni mengi sana jamani, wacha niishie hapa nisije wachosha zaidi
Wewe jamaa una iq ndogo.
Hayo yote uliyosema kuwa iPhone hawezi Mbona Mimi nayafanya.
 
Yani mtu ananunua kitu bila info halafu analalamika kuwa hakifanyi hiki, ni sawa ununue samaki halafu useme mbona haina taste ya nyama.
Watu hawajui tu iPhone ni simple sana kuitumia hasa kwa sie tusiokuwa wataalam wa IT kikubwa ni kujua kucheza na iCloud drives na ku-link up na PC yako na bila kusahau password ya icloud email
 
Mbona kuna option ya ku-share files zako na PC bila itune yaani naweza nikatengeneza folders kwenye iCloud drive na nikifungua PC nakuta zile files
Kwa lugha fupi utagharamika kununua bando ili udownload hizo files, shida yote ya nini hii wakti android ukipachika cable yako unaanza kazi.
wakati ukweli simu ni kifaa saidizi
hebu sahisha hapo, andika iphone ndio kifaa saidizi, simu gani haina hata redio 🤣🤣
mtu amenunua iPhone maana yake ana vifaa vingine vya ziada ambavyo vipo linked na simu yake
Acha kuropoka aisee, hapa bongo wapo watu kibao tu wana hizo iphones ila hawana hata laptops
 
Unanunua cm ili uckilize Dw [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na by the way sony hata hayuko top 10 ya wanaongoza kuuza simu that means people don't give a fu*ck about memory sticks 🤣🤣🤣
By the way hizi simu za sony zina features za professional video cameras hivyo sishangai kuwa na memory card maana zimetengenezwa kwa ajili ya kutumika kushoot mivideo.
Hata wewe hujainunua, yale yale ya blackberry kusema iphone itafail coz haiwezi kaa na charge kumbe people dont give a fu*ck about charge.
Jiulize kwanini iPhone anatoa highend phones na bado yuko top 3 ya mauzo?
Wakati wenzake humo wamemix hata simu za lak 2
huku hatununui simu kwa kufata mkumbo, tunaunua kulingana na mahitaji yetu.

Android ni kama mbuga ya serengeti utaweza kuona wanyama wengi sana na vivutio vya asili kwa gharama unayostaili kulipia na ukaridhika, iphone ni kama kwenda mbuga ghali ya dubai yenye wanyama wachache alafu unaaminishwa (branding) kwamba umefaidi kuzidi Serengeti
 
i cloud inakupa gb 5 bure na hii ndio wabongo wengi wameizoea, sasa vuta picha una files zako gb 200 huko, zitatosgha huko i cloud ? hata kama mtu kanunua space ya i cloud atalazimika tena kununua bando la laki 2 hapo kufanya backup tena itabidi asubirie hata masaa 7 ili kupandisha hizo gb 200..

ukiwa na memory card yako unahamisha fasta tu
GB5 yani robo ya kile wanachotoa G-DRIVE
 
mafundi simu wanaangalia jinsi ulivyo, kioo utachouziwa wewe laki 8 mjanja anauziwa laki .... ,

Hapa umeongea pumba kubwa tena kali mno, vioo vinauzwa kwenye maduka ya accessories kama hawa mawakala kina excellent au Samsung wenyewe

Watu wote wanajua bei ya kioo cha Samsung ni almost 40% ya original price ya simu
 
zipo simu kibao za High end kwa android, Samsung akitoa wenzake wanaweka.

Android ni mbuga yenye simu kibao, sio lazima kutumia samsung.

huku android hakuna mayanyasio kama ya iphone ambae akiamua kutoa kitu flani kwenye simu hakunaga wa kumbishia.
Ndo kinacho kuuma??
 
huku hatununui simu kwa kufata mkumbo, tunaunua kulingana na mahitaji yetu.

Android ni kama mbuga ya serengeti utaweza kuona wanyama wengi sana na vivutio vya asili kwa gharama unayostaili kulipia na ukaridhika, iphone ni kama kwenda mbuga ghali ya dubai yenye wanyama wachache alafu unaaminishwa (branding) kwamba umefaidi kuzidi Serengeti
Kama ni memory card, hiyo sony imeuza unit ngapi?
Ndio maana nimekwambia iphone ni package, ukichanga package ya vitu vyote basi ndio maana inapendwa.
Sio tu eti unanunua simu kisa labda memory card, tu.
 
Kama ni memory card, hiyo sony imeuza unit ngapi?
Ndio maana nimekwambia iphone ni package, ukichanga package ya vitu vyote basi ndio maana inapendwa.
Sio tu eti unanunua simu kisa labda memory card, tu.
Tupo tunaopenda kununua hizo simu sababu ya memory cards, ni sawa na atayeenda kununua laptop hata ikiwa na ukubwa wa 1 terabyte, bado atapenda kuwa na external hard disc kwa matumizi yake mengine binafsi.
 
Tupo tunaopenda kununua hizo simu sababu ya memory cards, ni sawa na atayeenda kununua laptop hata ikiwa na ukubwa wa 1 terabyte, bado atapenda kuwa na external hard disc kwa matumizi yake mengine binafsi.
Ni wachache ndio maana hiyo sony haiko hata kwenye top 10 ya kampuni zinazoongoza kwa mauzo.
iPhone haijawahi kuwa na memory card toka wameanza tengeneza na imekuwa iko top 3 kwa mauzo na hapo anauza highend phones.
Na wengine wamefuata hawana memory card kama yeye.
Iphone haijawahi kuwa na betri la kutoa mwanzo waliisema wee, sasa hivi karibu simu zote highend na low end kampuni almost zote hazina betri la kubandua mfuniko na kutoa.
Iphone kaondoa earphone jack, mwanzo hadi samsung walitoa tangazo la kuimock, sasa almost highend phones zote zinafuata hivyo.
Hata mleta mada sidhani kama ana highend phone ya recently na kama anayo haiwezi kuwa hiyo sony maana hata hawezi kuafford kuinunua hiyo sony ni ghali sana, maana tayari ashalalamika bei huko juu.
 
kama ikiibiwa au kupotea.iphone ndo simu ambayo huwezi kubadili account , ambayo ni icloud. hata ufanyeje hutaitoa labda ubadili hardware.
 
Back
Top Bottom