ANDROID INAWEZA KUFANYA ZAIDI YA KITU KIMOJA KWA MPIGO (Multi tasking)
View attachment 2166328
kufanya shughuli Zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho hakipo kwenye iphone, Android unaweza kutumia calculator, kuandika message, kusoma pdf na kucheki video kwa mpigo, screen ikiwa imejigawanya katika vyumba.
KWENYE IPHONE HAKUNA TUNDU LA KUCHOMEKA EARPHONES
View attachment 2166337
hakika huu uamuzi haukuwa na maana, ni uamuzi uliofanyika kibiashara zaidi bila kujali mahitaji ya wateja, kitu walichofanya ni kulazimisha wateja kununua wireless earphone zao au kama watahitaji kutumia earphone za waya basi wanunue kiunganishi chao cha ziada. Kwa android uchagyzi ni wako uamue kutumia za waya au wireless, binafsi headphone za waya zimewahi kunisaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia kuna Rafiki yangu alitaka kuibiwa simu, ilipovutwa alistuka mwizi akakimbia.
IPHONE IMEPIGWA GEPU REFU KWENYE APPS
View attachment 2166329
Sio siri wala kitu cha kubishana, Android kuna apps nyingi sana kuliko Iphone, Sababu kuu ni kwamba ili kuweka app kwenye playstore ya android gharama yake ni elf 50 mara moja tu lakini kwa upande wa iphones kuweka app kwenye apple store ni laki 2 unalipia kila mwaka, pia kwenye android unaweza kudownload na ku install apps ambazo hazipo playstore.
SIMU YA ANDROID YAWEZA KUTUMIKA NA MTU ZAIDI YA MOJA (Multi user)
View attachment 2166326
Hii inaitwa multiple user, simu inaweza kutumika na Zaidi ya mtu moja bila kuingiliana taarifa, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k, utampa simu aitumie bila wasi wasi. simu muhimu ikipigwa unaweza kuseti iite ili akuletee, ukimaliza maongezi unampa simu akaendelee. Unaweza kutengeneza hata accounts 4 za watu tofauti zitumike ofisini. Kwa iphone hawana hii.
ANDROID UTATUMIA INTERNET BURE BILA BANDO
View attachment 2166352
Hapa ndo napopenda aisee! mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, hizo mambo za kujibana hazipo huku android kwenye apps kibao kama ha tunnel, napster, n.k. unacheza tu na settings unaanza kuserereka, unaweza kushusha hata gb 20 kwa siku na wala isiwe habari lakini kwa iphone itabidi ununue kifurushi cha elf 30 ili upate hizo gb, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone matoleo mapya pale mlimani city mtu haoni taabu kulipia milioni 3 na hio simu anaiweka mfukoni, ishu ni hawa ambao wanaokwepa panga la bei kali kwa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.
IPHONE HAINA MEMORY CARD
View attachment 2166333
Iphones hazina memory card, Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ikaleta changamoto kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card , Lakini pia simu inaweza kuwa na gb 500 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card maana funguo mbili za gari ni bora kuliko moja, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ukapoteza kila kitu, ila kama ilikuwa na memory card, hata ikidondoka utachomoa memory card utakuta mafaili yako, hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako, unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu.
BEI
View attachment 2166316
Bei kali ya simu ya iphones ni kwa sababu ya kampuni ya apple kucheza na akili za watu kwenye branding, Kwenye swala zima la bei wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” kwa mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta kuna t shirt zenye ubora wa hali ya juu zinauzwa elf 20 lakini nyingine zina ubora wa kati zinauzwa elf 60, ukiuliza kwanini unaambiwa kwasababu ina nembo ya Nike, Gucci, n.k. wanacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu kwa kununua bidhaa hio, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones pale mlimani city, wengi hawana pesa kwa hio wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished), wengi zaidi hupendelea matoleo ya nyuma zaidi ili kupunguza makali ya bei (umelipenda boga kwanini uchukie maua yake ?), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la pili Mid range mfano OnePlus 8T, daraja la bajeti hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imekamata soko kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.
NI SHUGHULI PEVU KUPERUZI / KUHAMISHA MAFAILI YA IPHONE
View attachment 2166322
huku android tunatumia file managers tunaona mafaili yote kirahisi kwenye folders lakini system ya iphones haishirikiani kwenye kushare storage na apps kirahisi hivyo inakuwa ngumu kuperuzi mafaili yako, Hali inakuwa mbaya zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi, Mimi naweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android nikifika stationary nachomeka fasta tu naprint file, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes, na hapo inabidi anunue bando ili kudownload hio software, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.
IPHONE HAINA RADIO
View attachment 2166334
Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. Nikiwa na android yangu hata kile kipindi cha uchaguzi internet ilivyokatwa niliweza kuendelea kusikiliza vipindi vya redio navyovipenda.
MIPANGILIO YA MUONEKANO IMEBANWA SANA IPHONE
View attachment 2166317
Kwenye iphones kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa gepu refu sana kwasababu android unaweza kuweka launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako, utaweza kujipangilia icon kwa kuweka unazotaka wewe, kuzifinya na kuzitanua, n.k kucheza na elements zozote utakavyo kwenye home screen, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe commands, scrolling effects, lock screen customization, n.k. kuna vitu vichache kama widgets vimeongezewa kwenye iphone mwaka 2020 toleo a ios 14 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo, ajabu ni kwamba hapo zamani watumiaji wa iphones walikuwa wanadai wdgets za android zilikuwa hazina maana ila walipowekwa kwenye iphones wakaanza kuzisifia, kwa hakika sizitaki mbivu hizi.
IPHONE HAINA ALWAYS ON DIPLAY
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana ukitumia hii feature, Hadi sasa hii feature muhimu haipo kwenye iphones officially.
IPHONE WANACHELEWA SANA KUWEKA MAHITAJI YA WATEJA
View attachment 2166343
Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september, Tukija kwenye widgets za homescreen, iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo kitambo sana.
HUWEZI KUSETI RINGTONE UNAYOTAKA KWENYE IPHONE
View attachment 2166320
Ili kuseti ringtone yako kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari, utaweza kuweka mziki wowote uwe ringtome. kwenye iphones hii kitu hakuna, ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload app ya garageband, uingize mziki kwenye app, ufanye ku save ndio utaweza kuset hio ringtone, shida yote ya nini hii jamani? Hii ndio sababu wengi simu zao zina ringtone ile inalia kama vingoma vya Watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.
CAMERA
View attachment 2166341
kamera zimeboreshwa sana kwa simu zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kanera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali tu, hizi ishu za kamera nadhani kwa sasa zipewe kigezo chepesi maana teknolojia ya kamera imekuwa mno, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda sitashangaa simu za elf 80 zikitoa picha kali sana.
ULINZI
View attachment 2166338
Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand ni simu yenye ulinzi kamili walipoombwa kiroho safi waifungue wenyewe simu ya gaidi ila wakakataa, wataalam wakaingia kazini wakaifungua chapchap bila msaada, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. Pia nawakumbusha sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza nywila zako utadukuliwa tu, n.k.
JAIL BREAKING (IPHONE) v/s ROOTING (ANDROID)
View attachment 2166335
Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.
Ohhh mambo ni mengi sana jamani, wacha niishie hapa nisije wachosha zaidi