1. Hata samsung s22 na nyingine high end android phones hazina eearphone jack. Kama kawaida uwa akianza iPhone anapondwa hadi na samsung wenyewe nao baadae wanafuata.
Aliacha kuweka charger akapondwa nao wakafuata.
2. Unasema huwezi kufanya multi tasking kwenye iPhone, mkuu umewahi kuitumia au unasema tu?
3 Kuhusu apps, hivi ni bora kuwa na nguo chache lakini za maana au kuwa na bag la nguo nyingi hata ambazo hazina maana yani ukiivaa ukajitazama kwenye kioo unaivua. Ndivyo playstore ilivyo. Ina apps nyingi ambazo unaistall unakuta haifanyi hata walichosema inafanya unaiondoa. Kwasababu ni rahisi kuweka app playstore wakati istore wanamchakato serious.
4. Mwendo wa kustream ndio maana kuna maspotify na stations ziko kwenye mtandao.
5. Kuhusu kujailbreak, hata android kila toleo anakaza nati ili simu iwe ngumu kuroot. Android 11 au 12 sio sawa na android 6 hata kuroot si kawaida au rahisi. Ipe miaka 3 mbele utaona atakavyokaza kabisa.
6. Shida mkuu unasahau kuwa iPhone anatoa simu ambazo ni highend tu, ni kwa miaka ya hivi karibuni ambapo ametoa simu midrange hizi SE. So ukicompare simu zake highend compare na bei ya samsung ya mwaka huo.
Pia hata midrange anaweka processor ya highend. Mfano SE ya mwaka huu ina A15 bionic chip ambayo ndiyo chip yenye nguvu kwa sasa na ndio iko kwenye iPhone 13.
Natumia android kwa sasa, ila iOS ni habari nyingine.
Jinsi inavyofanya kazi, ilivyo smooth, vitu vinainteract, ecosystem ya apple, yani safi kabisa.