HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Sema iphone 7 ya Makumbusho, na leo watu wapo iphone 13, mwezi wa 9 wanakuwa na 14Natumia Iphone 7 plus, ila huu ni ukweli mchungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sema iphone 7 ya Makumbusho, na leo watu wapo iphone 13, mwezi wa 9 wanakuwa na 14Natumia Iphone 7 plus, ila huu ni ukweli mchungu.
Vipi unazitumia? Narudia tena 0.0001% ndio wananunua simu ya thamani ya mls 3 kuweka emulator wacheze games otherwise consoles zipo kwa ajili hiyo
Hiyo si simu labda anataka hard diskNavutaje picha kwenye kitu kisicho na ukweli.
Gb 200 kwenye iCloud utakua unatunza nini?
Unaaaminisha gb 200 sawa na shilingi laki 2?
Je infinix au tecno zinaweza tunza file la gb 200. Akipoteza simu ana iback up vipi?
Umasikini ndo tatizo lako, na kutojiamini.Umesahau hapo iPhone ni simu za wanawake wadangaji
Mwanaume kununua iPhone ni umama labda uwe shoga shoga
Mkuu mimi kwakweli kupingana na wewe siwezi maana wewe ni kati ya malegendary wa jukwaa hili japo pia na wewe ni mnazi wa android, microsoft, nokia kama alivyo mkbh na Apple 😄😄![]()
PPSSPP - PSP emulator - Apps on Google Play
Play PSP games on your Android device, at high definition with extra features!play.google.com
Downloads milioni 100.
Na most of time playstore wapenda emulators hawaitumii sababu inakuwa na version za zamani.
Hivyo mkuu milioni 100 atleast ni asilimia kadhaa ya watumiaji wa android.
Simu unajaza mafile yote hayo ili iweje?-Sio kila mtu ana computer
-Online unapewa gb 5 tu, simu ikijaa picha, videos, pdf, n.k za gb 100 hapo vp?
-kuhusu kupotea kwa memory card ni utunzaji wako, kama sio mtunzaji utapoteza hata simu,
Alafu cha ajabu ni kwamba huo Uhuru wa android ambao wengi wanauzungumzia ni wa mambo ya kitoto sanaa yaani... Mfano kudownload nyimbo, kubadili rangi ya screen nk🤣🤣🤣Iphone ni multi tasking unless kama mara ya mwisho umetumia iPhone 3gs.
Yes, android kila toleo anakaza. Hata sasa toleo la kuanzia android 11 amezuia hata app kuaccess baadhi ya mafile ya OS ambayo hapo kabla ziliweza kuaccess.
Zamani ulikuwa unainstall tu kiapp unaclick click faster ushaeroot simu. Sasa rooting is not as easy as it used to be.
Yes, ni mbuga yenye wanyama wengi wakubwa na wadogo. Ndio maana nimekwambia ukitaka compare na iPhone kwenye hiyo mbuga chagua highend phones za android uzicompare na iPhone ya mwaka husika kwa bei.
Usije compare sijui Xiomi midrange ya laki tisa na iPhone 13.
Sasa hapo ndipo unakosea, iPhone haikalenga kwenye hilo soko la watu wanaoishi sehem hata network hakuna. Sasa kama network hakuna, why ununue smartphone in the first place? Kumiliki smartphone wakati internet hakuna si bora urudi kwenye torch.
Yes A15 bionic ni the most powerful prpcessor kwa simu as of now. Iko kwwnye iPhone na kama ulitumia iPhone 3gs, hebu jaribu sasa halafu urudi hapa useme kama iPhone sio pure multi tasking.
Na mwisho ni kutaarifu tu, ukiachana na watu ambao wanasubiri miaka ndipo wamiliki hizi simu, watu wengi wanaoafford kununua hizi simu sio watu wa customization. Hata kwenye android watu wengi hata ukiwauliza kuhusu rooting hawajui na wanaojua ni wachache wanaoroot wakafanya la maana out of rooring.
iPhone wanaipenda watu ambao wanapensa kutumia vitu direct kama vilivyo bila kufanya customization. Mmoja wapo ni mimi, nna zaidi ya mwaka nna simu ya android, lakini hata sijaifanyia customization ya aina yoyote hata kuweka ringtone ya wimbo sijaweka. Niko hivyo.
Hata ukikutana na watu wanao afford kununua highend smartphones mfano s22 ilipotoka tu, ni wachache utakaokuta wameziroot na kuweka micustomization ya ajabu ajabu.
Premium users hawanaga mambo hayo.
Na mwisho kabisa, sijui kwanini android users uwa wengi wanakomaa kujicompare na iPhone users wakati ni mara chache iPhone users kujicompare na android users.
Hata zamani Apple alikuwa hacompare products zake na products za wengine. Ilikuwa na toleo jipya dhidi ya toleo lake la zamani. Enzi za steve jobs ilikuwa kama vile other phone manufacturers don't exisist.
Shida ipo kwenye Matumizi. Kaka wewe siyo mtu wa Costomization basi Iphone inakufaa lkn kama ni mtu wa customization nadhani android ni sahihi, ila hata hivyo wengi wananunua simu hawajui wafanyie nini na hizo simu zao, mwingine anaona ufahari tu kumiliki simu ya bei mbaya lkn hata kuscan document hawezi na hajui kama simu yake inaweza kufanya hivyoWatu weusi sisi tuna shida sana..
Mngejua Samsung wanaingiza hela ndefu kwa kufanya biashara na Apple kuliko kuuza hizo simu zao..
80% ya hardware za Apple products anauziwa na Samsung..
All in all simu ni simu tu, kila mtu na mahitaji yake, ila hua nawaonea(ga) huruma sana baadhi ya watumiaji wa iPhone wanavyo hangaika, nakubaliana na mtoa mada wengi wanatumia kwa mikumbo..
Mkuu hiki unachokieleza hapa wengi hawakuelewi lkn ndio ukweli wenyewe. Mtu unaishi kwenye Rough Road unaemda kununua gari ya chini alafu unalalamika Gari uliyonunua haifai🤣🤣🤣Kwanini sasa umeinunua kama haikidhi mahutaji yako?
Yani ni sawa ununue Lambourghini halafu uanze lalamika mbona ukiipotisha kwenye bumps inajigonga chini.
Kama wataka customization, kudownload nyimbo any how chukua android maana ndo selling point yake.
iOS na Android zikifanana kiutendaji basi itakuwa haina maana.
Last month nilianza jifunza kudesing UI nikaanza soma utofauti wa UI ya android na iOS, approach zao ni tofauti kabisa hata katika UI.
Nokia aliwatangulia wenzie miaka kadhaa mbele, akaka kivulini kuwasikilizia wasogee sogee, wenzake wakapita denge, kutahamaki akaacjwa miaka kadhaa nyuma.Sisi wa Symbian tunaruhusiwa kutoa maoni ?
View attachment 2168089View attachment 2168090View attachment 2168091View attachment 2168092
Maji ya Kilimanjaro mara nyingi utayakuta bungeni, mahotel makubwa na sehemu zingine za heshima. Maji ya uhai hata muuza ukwaju anayo anapotembeza ukwaju wake. Itoshe kusema Ni sawa uliyoyaongea na watu wanayafahamu ila ukiona kitu kinatumiwa na wachache jua Kuna Cha ziada. Huwezi kuwa Bora duniani Kama ujafanya kitu Cha ziada. Tununue tu simu zetu hizi hizi za Tecno.siongei sana, wacha tunyoke moja kwa moja kwenye hizi points 20+
Android inaweza kufanya mambo mengi kwa mpigo kirahisi (multi tasking)
View attachment 2167558
Kufanya shughuli zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho kimebanwa sana kwenye iphone, mfano ukitaka kuhamia app nyingine wakati upo kwenye video call basi video call itakata ili uweze kutumia app nyingine, Android unaweza kutumia hata apps hata 10 kwa mpigo na ndio maana kuna kitufe maalum katika vile vitatu ambacho ni maalum kwajili ya multi tasking, kwenye android pia kuna split screen ambayo inafanya screen igawanyike katika vyumba kadhaa kwa shughuli unazotaka kufanya kwa mpigo.
Kwenye iphone hakuna tundu la kuchomeka earphones
View attachment 2166337
Kitu walichofanya iphone ni kulitoa tundu ili kuwakamua pesa watumiaji wao kwa kuwalazimisha wanunue earphone zao zisizo na waya zinazouzwa kuanzia laki 2 na inabidi uzichaji kila siku, wabongo wengi hata iphone wanazonunua ni za mchongo zilizotumika (refurbished) kwasababu za kiuchumi kwahio huwa wananunua earphone wireless za mchina za bei chee, hakika maji hufata mkondo wake. Kwa android uchaguzi ni wako, unaweza uamue kutumia earphone za waya za elf 5 au waweza nunua wireless za laki 4, ni wewe tu. Earphone za waya zina umuhimu wake huwa hazihitaji kuchajiwa kila mara, huwa zinasaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia mtu akitaka kuchomoa simu yako basi unastuka.
Android kuna apps nyingi kuliko Iphone
View attachment 2166329
Sio siri wala kitu cha kubishana kwamba Playstore ya Android kuna apps nyingi kuliko Appstore ya Iphone, Sababu kuu ni kwamba, ili mtengenezaji wa app aiweke app yake kwenye playstore ya android atalipia elf 55 (55,000) mara moja tu lakini kwa upande wa iphone kuweka app kwenye appstore ni lazima ulipie laki 2 na elf 30 (230,000) “kila mwaka”, hapa ndipo watengenezaji wengi wa app wanakimbilia kutengeneza apps za android sababu ni bei rahisi na pia watumiaji wa android ni wengi kuzidi iphone.
Simu ya android yaweza kutumika na mtu zaidi ya moja (multi user)
View attachment 2166326
Hii inaitwa multi user, simu inaweza kutumika na zaidi ya mtu moja bila kuingiliana mambo, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k. utampa simu aitumie bila wasi wasi, wewe unakuwa kama admin flani hivi. Ni nzuri pia kwa mtu anapenda kuazima simu yako ila anapenda kupekua pekua visivyomuhusu.
Iphone inanunua vifaa kutoka makampuni ya simu za android
View attachment 2172257
Samsung huwa wanatengeneza simu za android lakini pia wanawauzia iphone vifaa kama vioo, processor, nano flash, n.k. hii ni kutokana na uimara wa vifaa vya samsung ambavyo vilimvutia iphone...
Android utatumia internet bure bila bando
View attachment 2166352
Mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, lakini hayo mambo ya kujibana hayapo android maana kuna apps kama ha tunnel, your freedom, n.k. zinafanikisha utumie internet bure. unaweza kutumia GB 100 kwa wiki na wala isiwe habari, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone za milioni 3 matoleo mapya pale mlimani city, shida inakuja kwa hawa wa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja na kila muda simu kaishika mkononi ili watu waione, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.
Iphone haina memory card
View attachment 2166333
Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ukasindwa kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card, Lakini pia iphone inaweza kuwa na gb 200 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ila kama ilikuwa na memory card basi utaichomoa kadi yako na ukayakuta mafaili yako yakiwa salama. hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu iende, pia unaweza kuwa na memory card unayohamishia mafaili na kuitunza sehemu salama ili hata simu ukiibiwa isiwe shida.
Bei
View attachment 2172222
Kwenye swala zima la bei Iphone wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta mkanda imara wa ngozi unauzwa elf 20 lakini mkanda wa manyoya unauzwa laki, ukiuliza kwanini unaambiwa mkanda wa manyoya una nembo ya Nike, Gucci, n.k. hii prestige pricing inacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu matawi ya juu endapo akinunua bidhaa hio, Ila sasa ill kuendana na hizi bidhaa huwa inafaa ununue bidhaa dukani na pia toleo liwe jipya, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones matoleo mapya dukani, wengi huwa wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished) na hupendelea kununua matoleo ya nyuma kidogo ili kupunguza makali ya bei (ukilipenda boga kwanini ulichukie ua lake ? ), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la kati “Mid range” mfano Motorola g-200, ama daraja la tatu “Budgjet” hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imelikamata soko kwenye hili kundi kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.
Notch ya iphone inaziba vitu kwenye screen
View attachment 2172218
.Notch ni kile kisehemu cheusi juu kwenye screen chenye camera na sensor, kwenye iphone huwa ni kipana sana na huwa kinakuziba usione video nzima, pia kuna apps nyingine natumia unakuta zimejaa kwenye screen ila kule kwenye notch unashindwa kuona ama kuminya,
Ni shughuli pevu kuperuzi / kuhamisha mafaili ya iphone
View attachment 2166322
huku android tunatumia file manager tunaona mafaili yote kirahisi lakini system ya iphones kwa kuwa haishirikiani vema kwenye kushare storage na apps huwa inakuwa kazi ngumu kuperuzi mafaili, shughuli inakuwa pevu zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi. unaweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android ukifika stationary unachomeka waya wa usb kwenye computer unaprint kazi haraka, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes na hapo inabidi anunue bando ili kudownload itunes, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.
Iphone haina radio
View attachment 2166334
Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. ukiwa na android hata kikifika kipindi cha uchaguzi, internet ikikatwa na tcra bado unaweza kuendelea kusikiliza radio.
Mipangilio ya muonekano imebanwa sana iphone
View attachment 2166317
Kwenye iphone kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa kanzu na android kwasababu kwenye android wanaruhusu kubadili launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako kuanzia muonekano na upangiliaji wa icons, kubadili styles za miandiko, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe actions, scrolling effects, lock screen customization, widgets, n.k. kuna vitu vichache kama widgets za homescreen viliongezewa kwenye iphone mwaka 2020 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo.
Iphone haina always on diplay
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda ukitaka kuangalia muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana, Kuna tetesi matoleo yajayo ya iphones huenda wataweka hii ishu.
Iphone ni lazima utumie bando kuingiza app/game
View attachment 2170901
Kwenye iphone njia pekee ya kuingiza app ni kuzi download kwenye appstore kwa kutumia bando, huku android si lazima kudownload app kwenye playstore, mfano kama unahitaji app flani na huna bando, unaweza kwenda kwa mwenye hio app akakuhamishia file la app kwenye memory card au kwa usb cable, ukipata file unaingiza app bila hata bando. ukitaka ujue thamani ya hii feature chukulia kwamba app kama game ina gb 7 ambazo kifurushi cha data ni shilingi elf 10, kwenye iphone lazima wekundu wa msimbazi ukutoke ili ushushe app ila kwenye android hutalipia hata senti, lakini pia kama sehemu haina network nzuri itabidi usubirie muda mrefu mpaka app imalize kudownload na kama internet imekatwa itabidi utulie tu.
Iphone wanachelewa sana kuweka mahitaji ya wateja
View attachment 2166343
Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september na hapo bila milioni 2 huipati ila toka kitambo kulikuwa na vitochi vya elf 20 vyenye line mbili, Tukija kwenye widgets za homescreen iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo muda mrefu.
Huwezi kuseti ringtone ya muziki kwenye iphone
View attachment 2166320
Ili kuseti ringtone yoyote kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari na ni rahisi, kwenye iphone ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload apps za ziada., hii ndio sababu watumiaji wengi wa Iphones simu zikiita huwa zina mlio kama wa vingoma vya watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.
Camera
View attachment 2166341
kamera zimeboreshwa sana kwa pande zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kamera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali, nadhani hizi ishu za kamera kwa sasa tuzichukulie kawaida, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda tutarajie hata simu za elf 80 zikitoa picha kali mno.
Ulinzi
View attachment 2166338
Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand kwamba wana simu yenye ulinzi kamili kuna kipindi walikataa kutoa ushirikiano kwenye kuifungue simu ya gaidi ila wataalam wakaichokonoa chapchap ikafunguka bila msaada wa kiwanda cha iphone, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, pia iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. nawakumbusha kwamba sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza password zako utaibiwa akaunti yako, n.k.
Jail breaking (iphone) v/s Rooting (android)
View attachment 2166335
Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.
iphone hazina support nzuri ya Emulators za game
View attachment 2172113
Emulators ni app zinazorugusu kucheza games za playstation, psp, n.k. iphone hazina support nzuri ya Emulators. Kama una simu ya Android ya kisasa kuanzia 2018 kupanda unaweza ukacheza games za Nintendo switch, gamecube, Wii, Playstation 2, psp, Sega dreamcast na console kibao za zamani. Iphone kuna emulators chache sana na hizo zilizopo ni uibie uibie ku install. (point kutoka kwa chief - mkwawa)
………………………………………
Jamanni nawaombeni tu niishie hapa maana nimechoka kuandika, mambo ni mengi ila muda umenibana, yani huwezi amini mpaka leo kuna vitu kama kile kitaa cha rangi cha notification hakipo kwenye iphone, Hivi kweli jamani?.., mdebwedo ni mdebwedo tu hata uuzwe milioni 3😂😂
Mkuu hiki unachokieleza hapa wengi hawakuelewi lkn ndio ukweli wenyewe. Mtu unaishi kwenye Rough Road unaemda kununua gari ya chini alafu unalalamika Gari uliyonunua haifai🤣🤣🤣
Yes A15 bionic ni the most powerful prpcessor kwa simu as of now. Iko kwwnye iPhone na kama ulitumia iPhone 3gs, hebu jaribu sasa halafu urudi hapa useme kama iPhone sio pure multi tasking.
yaani... Mfano kudownload nyimbo, kubadili rangi ya screen nk🤣🤣🤣
tushauriane kwa upendo, ila tusipangiane maisha
Hiyo ni feature tu ya app logic behind ni kwamba video unaitazama ukitoka kwenye app ya kutazama inajipause mpaka urudi.Hiyo A15 Bionic ya Apple kama haiwezi kuwasha mziki wa youtube wakati nasoma message za whatsapp then its worthless…
Mbona kuna option ya ku-share files zako na PC bila itune yaani naweza nikatengeneza folders kwenye iCloud drive na nikifungua PC nakuta zile files muda huo huo na uki-save files kwenye PC wakati huo huo unalikuta kwenye iPhone, shida yetu sie Watz tunatumia simu kama mbadala wa PC na ndio maana tunalilia sana na watu wanaomilki simu za iPhone wakati ukweli simu ni kifaa saidizi mpaka mtu amenunua iPhone maana yake ana vifaa vingine vya ziada ambavyo vipo linked na simu yake