Nafurahi Watanzania wameanza kuamka JF na mitandao mengine katika kuwakataa wanaharakati na kuhubiri Amani

kwa wanaotaka kuharibu heshima ya amani, msako uendelee
Hiyo ndiyo silaha sio pindi ukishikwa mkono usiendelee kukwapua mali na rasilimali za taifa ama chaguzi sio?
 
Lakini wananchi wanapenda sana watekaji, wanaonajisi box la kura na kuiba fedha zao. Ni hivi, njia zote sahihi za kudai haki zilifuatwa lakini mkawa na kiburi. Sasa machafuko ndio njia pekee inayoweza kuleta heshima ndani ya nchi hii. Na huu si mwisho wa maandamano, bali ni mwanzo tu wa kupata mabadiliko ya kweli.
 
kuna hela yako imeibiwa?
 
Ndugu yangu Invisible Mafia nashukuru sana kwa kutambua nia yetu dhabiti ya kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha Amani

Pongezi kwako kuwa sehemu ya team hii muhimu sana kupinga fujo na uvunjifu wa amani tupo pamoja kwenye harakati muhimu kwa amani ya nchi yetu
 
Mafanikio makubwa kabisa ya huu utawala unaotawala bila ridhaa ya wananchi ni kutengeneza machawa wa kutosha.
Mifano iihai ila nawakumbusha kubebana na akili zao wasisiache nyumbani kama ilivyomazoea yao.
 
Ila pia mkumbuke kutokuimba tu kikasuku Amani,je hiyo amani imepotezwa na nini na nanikachangia vinginevyo hiyo unayoitaa ni nia njema isijekuwa unatengeneza kingine usichokijua?
 
Maria anawaambia watu waelekee Ikulu,?eti wasiogope seriousily...Yeye hata kuja kumzika Baba yake hakuja kisa anaogopa hao hao Kina Samia.Vijana msidanganyike yeye mwenyewe amekimbia nchi kisa Samia.Leo nyie anawaambia muandamane kwenda Ikulu. Sipendi serikali ya CCM ya Samia.Ila tusijitoe ubongo .Hawa tutawashinda tu.Ila si kwa kujitoa ubongo. Wana vyombo vya ulinzi vote.
 
hawa wahalifu lazima tushuhulike nao, kwa kifupi hatujamaliza lazima msako uendelee
Na upande wa pili wa Tsh pia ni wa muhimu kuutazama.

waTanzania wasio na hatia baadhi waliuwawa wakati wa operation ya kizuia machafuko ya oct, sasa ikibaki kama colateral damage, kuna siku tu uchungu unaovumiliwa na wahanga utalazimika kuwatoka halafu katika kuudhibiti watauwawa tena wengine, circle itaendelea.

Katika waliotumwa kudhibiti yale matukio hawakosekani waliotoka nje ya naadili ya kiapo cha ulinzi wa raia. Lazima wapatikane wa kuwajibishwa kwa mauaji ya wasio na hatia, wale ambao hawakuwa wakiiba, wakichoma wala kuandamana.

Lisifunikwe kombe kwa kuhitimisha kuwa ile nguvu iliyotumika ni sahihi, watekelezaji wa lile tukio ni binadamu, lazima kuna waliofanya makosa nje ya weledi wa askari, makosa ambayo hayana budi kulipiwa, watafutwe waliokosa weledi katika ile operation na kupelekea vifo visivyo na hatia washtakiwe mahakamani kwa mauaji.

Hii itapunguza idadi ya wenye chuki na serikali sababu ya oct 29, idadi ya raia wenye hasira inaweza kupunguzwa kwa uwajibikaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…