Nafurahi Watanzania wameanza kuamka JF na mitandao mengine katika kuwakataa wanaharakati na kuhubiri Amani

Nafurahi Watanzania wameanza kuamka JF na mitandao mengine katika kuwakataa wanaharakati na kuhubiri Amani

Na upande wa pili wa Tsh pia ni wa muhimu kuutazama.

waTanzania wasio na hatia baadhi waliuwawa wakati wa operation ya kizuia machafuko ya oct, sasa ikibaki kama colateral damage, kuna siku tu uchungu unaovumiliwa na wahanga utalazimika kuwatoka halafu katika kuudhibiti watauwawa tena wengine, circle itaendelea.

Lazima wapatikane wa kuwajibishwa kwa mauaji ya wasio na hatia, wale ambao hawakuwa wakiiba, wakichoma wala kuandamana.

Lisifunikwe kombe kwa kuhitimisha kuwa ile nguvu iliyotumika ni sahihi, watekelezaji wa lile tukio ni binadamu, lazima kuna waliofanya makosa nje ya weledi wa askari, makosa ambayo hayana budi kulipiwa, watafutwe waliokosa weledi katika ile operation na kupelekea vifo visivyo na hatia washtakiwe mahakamani kwa mauaji.

Hii itapunguza idadi ya wenye chuki na serikali sababu ya oct 29, idadi ya raia wenye hasira inaweza kupunguzwa kwa uwajibikaji.
amna mwanajeshi anaweza kuondoa uhai wa mtu asie na hatia kwa kukusudia, kuna ambao bahati mbaya katika vita pale lakini wengi walikua na nia mbaya hivo lazima msako uendelee
 
amna mwanajeshi anaweza kuondoa uhai wa mtu asie na hatia kwa kukusudia, kuna ambao bahati mbaya katika vita pale lakini wengi walikua na nia mbaya hivo lazima msako uendelee
Ni vigezo gani vinaepusha uwajibikaji kwa makosa yaliyoondoa maisha ya raia mwema kwa bahati mbaya?

Hata raia wa kawaida, anapoua kwa bahati mbaya anashtakiwa ajieleze mahakamani. Kwanini si kwa hawa askari waliotumwa kudhibiti vurugu?

Hawa wa bahati mbaya wana ndugu, jamaa na marafiki, wataambiwa tu ni bahati mbaya kisha wasahau? idadi ya wahanga inaruhusu hili kutokea bila hatari ya kulimbikiza hasira zitakazohitajika kudhibitiwa huko mbele na kusababisha uwezekano wa damu nyingine kumwagika? ni swali ambalo binafsi sina jibu.

Binadamu hachagui kuwa na hasira, ni jambo la kibiolojia, hizi hasira za baadhi ya watu zinaweza kuisha kwa wepesi tu iwapo kutafanyika sorting ya askari waliotekeleza amri ya kudhibiti vurugu nje ya weledi wa kiapo chao.

Sijui, anyway ukweli mnaujua watendaji. Wengine tunatoa maoni na kushauri. Muda utahitimisha uhalali wa kilichotokea. Kwa sasa ngoja turejee makazini tukafanye kazi.
 
Hiyo para ya mwisho umeandika nini?!
Ningependa kuona hao unaowasifia wameandika nini humu kuhusu HAKI, watu kupotezwa hovyo, na mauaji.
 
Maria anawaambia watu waelekee Ikulu,?eti wasiogope seriousily...Yeye hata kuja kumzika Baba yake hakuja kisa anaogopa hao hao Kina Samia.Vijana msidanganyike yeye mwenyewe amekimbia nchi kisa Samia.Leo nyie anawaambia muandamane kwenda Ikulu. Sipendi serikali ya CCM ya Samia.Ila tusijitoe ubongo .Hawa tutawashinda tu.Ila si kwa kujitoa ubongo. Wana vyombo vya ulinzi vote.
Kwa hiyo njia nyingine hiyo ni ipi.

Or you're holding your cards close to your chest.
 
wanadhani wote tunaohubiri Amani ni machawa na tunapendezwa na yote yanayoendelea hilo sio kweli bali hatutaki njia mbaya za fujo , machafuko na ghasia ambazo zinakwenda kuathiri wote haswa raia wa chini bila mafanikio yeyote.
Nyie wote ni machawa wahed maana hamjawahi kusikika mkikemea ufisadi, wizi wa uchaguzi, utekaji, ufiraji, mauaji - ambazo ndizo baadhi ya kero kubwa za wananchi
 
Nyumbu wezi na waharibifu wa mali wanaohamasishana maandamano uchwara ya kihalifu lazima wapelekewe moto , wakileta unyumbu ni mwendo wa risasi bila huruma
 
Popoma umekimbia ID yako, Sasa unatumia hii ili tusigundis mashudu yako
 
Kwanza kabisa nashukuru Mwenyewezi Mungu kwa kujalia hali ya usalama na kuepusha jambo baya lilipangwa dhidi ya nchi yetu 09 December.

Pia natoa pongezi kwa Makamanda wa kuhubiri amani Jf stakehigh Victoire GENTAMYCINE Robert Heriel Mtibeli Ertugrul Bey iamwangdamin na wengineo hapa Jf na kwengineko.

Watu wanashindwa kuelewa wanadhani wote tunaohubiri Amani ni machawa na tunapendezwa na yote yanayoendelea hilo sio kweli bali hatutaki njia mbaya za fujo , machafuko na ghasia ambazo zinakwenda kuathiri wote haswa raia wa chini bila mafanikio yeyote.

Nawasihi wapenda Amani wote , tuwaelekeze wenzentu kwa njia nzuri bila kuwakejeli wala kuwatusi na tusichoke katika harakati hizi , tukikaa kimya kama mwanzo wao watatawala katika kueneza mambo ambayo yanayopelekea uvunjifu wa amani na machafuko.

Nimefurahi kuona sasa karibia mitandao yote watu wanajitokeza kuwakataa wanaharakati uchwara na kukataa njia zao mbaya za kudai haki. Wabongo sasa wameamka na kustuka.

Cheki hapo wakimjibu Maria Sarungi Leo katika mtandao wa X.View attachment 3513821

Mwengine.

View attachment 3513822

Kingene kinachofurahisha zaidi Raia hawapendi kabisa hali ya lockdown na fujo kiasi ambacho hawapendi kutafuta riziki zao za kila siku kwa ajili Yao na familia zao na wengi hawataki hizi hali zijirudie.
VIVA TANZANIA , VIVA AMANI , TANZANIA NI KISIWA CHA AMANI , KISIMA CHA UPENDO . TUDUMISHE MILA NA DESTURI ZETU , WAJINGA WACHACHE WANATAKA KUTUTETEMESHA NA KUVUNJA UMOJA WETU. SAY NO TO WANAHARAKATI.
 
Kuna wakati ukikaa kwa kutafakari kwa umakini utagundua kuna wanaharakati walitaka kutupeleka siko..hawahubiri Maandamano ya amani bali wao wanataka watu watoke waandamane(Fujo,kuharibu miundombinu na Ghasia)
 
Acheni kuteka na kuua watu 📌
Tendeni haki 📌
Wasikilizeni wananchi 📌
Punguzeni ufisadi 📌
Ruhusuni katiba mpya 📌
Inueni uchumi wa watu wenu 📌
Ruhusuni tume huru ya uchaguzi 📌
Shughulikeni na ajira kwa vijana 📌
Punguzeni nepotism 📌


Kutoyazingatia haya machache kutazidi kuchochea moto mioyoni mwa watu. Na nchi haitakuwa salama. Kunaweza kuwa na utulivu lakini kusiwe na amani. Ni kama kuwa na bomu chini ya kitanda chako!

Kwa sasa mnaweza kufurahi na kupongezana kuwa mmefanikiwa kuzuia maandamano tena kwa gharama kubwa ya ku-mobilize jeshi utafikiri nchi imo vitani lakini wananchi mnaowaongoza wana hasira na visasi. Na huwezi kutawala watu ambao hawakukuchagua na hawakutaki. Wengi walishajaribu wakashindwa na hawakuwa na mwisho mwema.

Samia atajaribu kutawala kwa kutumia mitutu ya bunduki, kuteka na kuua watu lakini hataweza na, kama historia ni mwalimu sahihi, hatakuwa na mwisho mzuri. Na ataishia katika pipa la takataka la historia kama kiongozi katili, muuaji, fisadi na asiyejali.

Anajua hakuchaguliwa na wananchi. Anajua hakupata kura milioni 32. Anajua hakushinda kwa 98%. Anajua uchaguzi ulivurugika. Anajua alijiapisha kimagumashi. Anajua siyo rais halali. Anajua anaongoza serikali haramu. Basi angalau ajaribu kutenda haki ili ajikongoje na hii miaka mitano yake ambayo itakuwa mirefu na ya mateso sana kwake hasa akiendelea na huu udikteta wake.

Mungu Aendelee kuibariki nchi yetu hii nzuri yenye kila kitu lakini inaharibiwa na wanasiasa wasio na maono, walafi, wauaji, mafisadi na wasiojali! 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿

IMG-20251209-WA0008.jpg
 
Ndugu yangu Invisible Mafia nashukuru sana kwa kutambua nia yetu dhabiti ya kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha Amani

Pongezi kwako kuwa sehemu ya team hii muhimu sana kupinga fujo na uvunjifu wa amani tupo pamoja kwenye harakati muhimu kwa amani ya nchi yetu
Kwa bahati mbaya hamuwezi kufanikiwa kwenye hayo mahubiri ya amani ni kama kutwanga maji kwenye kinu.
 
Kwanza kabisa nashukuru Mwenyewezi Mungu kwa kujalia hali ya usalama na kuepusha jambo baya lilipangwa dhidi ya nchi yetu 09 December.

Pia natoa pongezi kwa Makamanda wa kuhubiri amani Jf stakehigh Victoire GENTAMYCINE Robert Heriel Mtibeli Ertugrul Bey iamwangdamin na wengineo hapa Jf na kwengineko.

Watu wanashindwa kuelewa wanadhani wote tunaohubiri Amani ni machawa na tunapendezwa na yote yanayoendelea hilo sio kweli bali hatutaki njia mbaya za fujo , machafuko na ghasia ambazo zinakwenda kuathiri wote haswa raia wa chini bila mafanikio yeyote.

Nawasihi wapenda Amani wote , tuwaelekeze wenzentu kwa njia nzuri bila kuwakejeli wala kuwatusi na tusichoke katika harakati hizi , tukikaa kimya kama mwanzo wao watatawala katika kueneza mambo ambayo yanayopelekea uvunjifu wa amani na machafuko.

Nimefurahi kuona sasa karibia mitandao yote watu wanajitokeza kuwakataa wanaharakati uchwara na kukataa njia zao mbaya za kudai haki. Wabongo sasa wameamka na kustuka.

Cheki hapo wakimjibu Maria Sarungi Leo katika mtandao wa X.View attachment 3513821

Mwengine.

View attachment 3513822

Kingene kinachofurahisha zaidi Raia hawapendi kabisa hali ya lockdown na fujo kiasi ambacho hawapendi kutafuta riziki zao za kila siku kwa ajili Yao na familia zao na wengi hawataki hizi hali zijirudie.
AMANI BILA HAKI NI UTUMWA ...Hivyo ukimsikia mtu sna hubiri amani bila haki jua mtu huyo ajenda yake ni kukugeuza mtumwa
 
Yalikuwa ya amani yakavurugwa na Risasi na mabomu ya polisi
Hayakuwa Amani tokea starting point.

1. Kwenye Magroup ya maandamano walikuwa wanahamasishana kuchoma choma na uharibifu hata hapa Jf Lord Denning kila post yake alikuwa anasisitiza kutia moto miundombinu

2. Siku ya maandamano kabla ya polisi kuingia kati walishaanza kuchoma vitu na wengine kufanya wizi
 
Natoa pongezi kwa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kwa kuhakikisha utulivu na amani inarejea nchini.

Hawa wachochezi wengi ni diasporas, na wengine watakuwa wamejichimbia hapo kenya, natoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama wawasake kimyakimya mpk waishe.

AMANI YA NCHI YETU IWE KIPAUMBELE.
Vyomba vya ulinzi wameupiga mwingi mno Kongole kwao
 
Wanaopiga kelele za amani ni wezi na wahujumu wa nchi, wanataka kula pesa za wananchi bila kupigiwa kelele, haiwezekani
Huwezi kuhubiri amani pasipo haki, penye wizi na udhalimu,
Aliejirundikia mali za wizi na ubadhirifu wa fedha za uma anataka amani ya kula pesa zake
Haki, uwajibikaji, utawala bora vikipatikana amani inakuja yenyewe
 
Na pia usihusishe watanzania kwenye hisia zako, sema wewe na huyo aliemkataa/kuwakataa
 
Back
Top Bottom