Ingawa jamaa
Komeo Lachuma kaandika kama kejeli Fulani hivi kwa watoto wanaobweteka na vya nyumbani au kishambenga Ila Kuna ujumbe ndani yake.
Sisi weusi tumezoea watoto wanaondoka home wanaenda kujenga makazi yao, wanaleta wajukuu kwa Babu na bibi kuwapa kampani. Ingawa Sasa hivi kwa sababu ya umuhimu wa elimu Bora, wachache Sana wanaopeleka wajukuu kwa Babu. Ni jambo zuri ingawa........
Ikifika wazee wakaishiwa nguvu wanaanza ama kutangatanga kwa watoto wao au baadhi ya watoto (na hasa wa kike) wanarudi nyumbani kuwalea wazee wao mpaka wanakufa, na wakishakufa makazi yanabaki tupu au analetwa ndugu Aishi pale kama mlinzi.
Wewe Bintimkongwe
bitimkongwe Kama Kuna mtu mtoto Kati ya watoto ambaye anaweza kuishi hapo na wazazi akawaangalia na kuwalea na kuwahudumia kadiri wanavyozeeka kwa Nini asiishi nao?
Waarabu na wahindi wanaishi kwenye "boma" yaani plot moja Kuna nyumba nyingi za watoto wamezunguka nyumba ya wazazi wao, wanakuwa karibu na wazazi wao, Ila sisi weusi tunaona furaha na amani kuwaacha wazazi Nkenja sisi tukaishi Bunda. Je ni sawa kwa maoni yako?