Nahisi "house girl" anayedaiwa kuua mtoto ni muhanga

Hichi kisa kwa kiasi kikubwa kinafanana na kisa kilichotokea huku Zanzibar miezi kadhaa iliyopita. Kuna mume alimuua mke wake halafu msala ukamuangukia house girl. Sema kwa mujibu wa mauaji yalivyotendeka intelijensia/saikolojia ya polisi ikakataa kwamba mauaji ya aina ile yanaweza kufanywa na binti wa kazi ambaye kiumri na kimuonekano haendani kabisa na tukio lile. Wakati binti wa kazi anahojiwa na askari mwanzoni alikuwa anasita kufunguka ukweli na wakati yupo ndani (kituoni) aligoma kula kwa masaa kadhaa...ila mwisho baada ya kumrai sana ikabidi afunguke ukweli na jinsi tukio zima lilivyotokea...ikaonekana ni mume ndo aliyeua kinyama mke wake...binti alieleza kuwa kaka (boss wake) alimwambia asimwambie mtu kilichotokea vyenginevo angemuua, kisha yule jamaa akamshikisha kisu yule binti na kumpakaza damu mwilini...jamaa akasepa akamuacha binti na maiti ndani...wakati jamaa anamchinja mkewe huyo binti alitoka kwenda kumpeleka mtoto wa boss wake kupanda gari ya shule...sasa wakati anarudi ndo ndani anakuta jamaa amegeuza mkewe bucha.

Binti alieleza kuwa siku moja kabla ya tukio hao mabosi zake waligombana.

Kama ilivyo kwa kisa hiki cha hapo Dar, wapo baadhi ya watu wajuaji wa mtaa wakaanza kusambaza 'voice note' za kwamba house girl kaua bosi wake wa kike, tena wakahadithia kama walishuhudia vile wakati binti anaua na kuwatahadharisha watu wawe makini.😂 mwish wa siku uchunguzi wa polisi ukawaumbua...yule binti akabadilishwa 'status' badala ya kuwa mtuhumiwa akageuka kuwa shahidi huku akiwa chini ya ulinzi madhubuti wa dola.

Kesi ya huyo jamaa bado ipo mahakamani na askari wanaendelea kukamiliisha baadhi ya mambo ya kiushahidi, kisha shauri lianze kusikilizwa.

So, katika hili pia tuvuteni subra mengi yataibuka au yataibuliwa.
 
Hii tayari ni CV yako inatosha kuomba kazi ya ukolokoroni na ukapata.
 
kama sikosei hii habari si ngeni na wahusika walisema kuwa cctv camera ilitumika kumbaini housegirl akitekeleza mauaji sasa hapo sielewi kuna uchunguzi gani tena labda ueleze kuwa uchunguzi ufanyike kujua ni kwa nini mdada alifanya haya mauaji hayo.
 
Mbona nilisikia nyumba ina CCTV na zilithibitisha uhhsika wake.
Ila hata mimi nahisi there is more to this story. Yani siku ya tatu afanye maafa na asikimbie
 
Niko mbali kweli na mji, kumbe kuna tukio tena la house girl kusababisha mauwaji.

Apumzike kwa amani huyo mtoto,pole kwa wazazi na ndugu.

Kama mleta mada alivyosema hakika kuna hitajika uchunguzi wa kina kwa tukio hili, hakuna tukio kama hili linakokosa sababu tena zenye mantiki.
 
Fingerprints zinafanya kazi kama zitakuwepo kwenye database

Kama mhusika hana kitambulisho chochote kile na hayupo hapo ni ngumu sana kupata fingerprint zao

Pia finger print matching ni ngumu kwenye mwili wa marehemu maana miili mingi huguswa na watu wengi...

Kama hapo print matching lazima itamhusu msaidizi wa kazi za nyumbani...

Swali linakuja kwanini kabaki baada ya mauaji?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
No 4,Hapooo eneo alojenga alipewa na mjomba wake ina semekanika Ana mgogoro na watoto Wa mjomba Hawa kufurahishwa na yeye kimaisha katoboa! Na pia walikuwa na mpango Wa kuhama hapo
 
Binti katumika hapo anawajua waliomnyonga. Au maskini bila kujua alitembelewa na watu akawakaribisha na wao wakafanya yao kisha wakatiririka.
 
-Mtu aue halafu apige simu kwa bosi wake [emoji848]
-Mtu aue halafu asikimbie[emoji848]
-Mtu anasiku 3 hata mateso ya uhousegirl hajayapata bado halafu alipize[emoji848]
-Hapo wangekuwa FBI au CIA au interpoll police ukweli tungeujua ila hawa polisi wa Tanzania tusahau na hii habari itavuma wiki moja tu halafu kimya hakutakuwa na mwandishi wa kufuatilia tena
 
Yah. Wa match na watu wa karibu. House boy na dada wa kazi? Izo za maeneo ya shingoni.

Usishangae anaweza dada akawa kafanya kitendo na still akabaki kama kubabaisha watu aonekane innocent. Na kama dada bado ni mdogo lbd below 18 yrs anaweza akawa hajapata maarifa ya nn cha kufanya after kutekeleza adhma yake.

Ila binafsi sikubali kama dada ndio kaua. Otherwise awe agent wa shetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…