Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

We Chalii skia hata Mimi nishawahi kukutana na changamoto kama yako na Nina mzazi mmoja tu my lovely mummy dingi alitutema

Fanya hivi jifanye wewe ndio una makosa shuka chini kabisa,akikuita nenda akikuambia ufanye chochote ndani ya uwezo wako just do it

Utanishukuru arif

Wewe baada ya kuwa mtiifu kwa maza .Nini kilitokea?
 
Ukifikaa Chuo kuna uhuruu flani unategemea uwe naoo mpaka mama akipiga simu Kila siku kukujulia hali unahisi kama anakuzongaa sanaa.. Anywat ni Balehee hiyo inakusumbuaa na ubaya ukute wew ndo mtoto wa pekee wa kiume au pengine wa pekee kwa mama yako lazima ujifunze Kujishusha na kukubali kwenda sawa na mama...! Mama yako anakuhitaji sana kipindi hiki tokana na upweke aliokuwa nao jitahidi umsikilize na kumjali maana hayo mapenzi Baba zetu hawanagaaa kabisa.
 
Haki ya mzazi aliyesoma na asiyesoma hazifanani.
Atende Haki.
Kwenye familia hakuna kitu inaitwa haki mkuu. Labda Ulaya huko ila hapa kwetu hizo haki za mama na mwana hazipo.

Hata kwenye mabaraza ya usuluhishi huwa hawasuluhishi kwa kufuata hizo haki. Wanasuluhisha kuleta amani, na ndio maana mambo mengine hata polisi huwaasa mkamalizane kifamilia, imagine sehemu uliyotegemea itendeke haki mnaambiwa hayo ni mambo ya kifamilia, mmalizane kifamilia.

Kwenye familia hatuiti haki tunaita Busara.
 
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu. Kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa muda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi. Mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kuwa nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani.

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi.

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae. Hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia.

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi.
Unafeli sana mdogo wangu..
Jirekebishe maana tatizo ni wewe. Mpende mama yako angali hai, usifanye asononeke kwa mambo madogo kama hayo.
Jitafakari na urudi kwenye mstari. Maisha ni mafupi na siku ikitokea umempoteza nakwambia hautakuwa sawa.
 
Wewe shida ipo.kwako inaelekea ukienda kwenu ni kula kulala na kuchezea simu kuna uzi.ulisema upendi kabisa kuamshwa kwenda kanisani wewe bado mtoto ukumbuke

Nje ya hiyo una asili ya kiburi mbishi na utaki kukubalina na ukweli
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna ile unakuwa ushazoea maisha ya chuo alafu urudi kijijini ukutane na bard la asubuh likupige utaomba chuo mrudi kesho hio tuachane nayo maana we nikama mtu wa mjini hatakama sio mji mkubwa ushazoea hayo maisha ya kujitawala hutak shida ila kumbka huyo ni mama tena umesema ndo mzazi uliebak nae ukipata mtu wa hvyo bas mthamini sana maana wengine hio nafasi ya hao watu hatuna niishie hapo nikutakie utekelezaji mwema
 
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu. Kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa muda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi. Mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kuwa nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani.

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi.

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae. Hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia.

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi.
Sometimes unatakiwa kusafiri nae kwenda sehemu zenye natural therapy,tafuta maeneo kama Tanga,Mwanza,Tukuyu na Mafinga,tembelea milima,mito na baadae msaidie kupika chakula cha jioni Kisha kila mmoja analala kwenye tent yake then utajua kitu,anamkosa mumewe alifariki dunia kama sikosei,kuna ugonjwa wa upweke hua unatesa Sana watu wazima
 
Vijana wengi mliofika level ya vyuo hasa vyuo vikuu kwa sasa mnajitia sana ujuaji hasa baada ya kukutana na vitoto vya kike huko vyuoni. Mnajifanya mmesoma sn maadili ya magharibi na kudharau ya kwenu. Waheshim sn wazaz wako no matter what.
 
Back
Top Bottom