Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Kwanza kabisa epusha ugomvi na mzazi wako na tena umesema ndo huyo mmoja uliyebak naye
Nmesoma kwa umakini kidogo nilichogundua mzazi wako anahitaji uone au anatamani sana kuona mjuu wake nadhani ukifanya hivyo utamfurahisha na ugomvi wenu utaishia hapo
 
Namanisha mzazi wako anataka uoe yani uwe na mke
Pale alipokwambia anaona kuna mwanamke uko naye na umempa mimba hiyo ndo furaha yake
Fanya siku moja kwenda kumtambulisha umpendaye uone jinsi atakavyo furahi
 
niko chuo bro hata miaka 20 sina
 
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu. Kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa muda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi. Mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kuwa nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani.

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi.

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae. Hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia.

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi.
Jishushe dogo

Utapotea
 
niko chuo bro hata miaka 20 sina
Daah pole sana kama hilo haliwezekani basi epuka ugomvi usio wa lazima na mzazi wako
Wazazi wetu wanapenda sana kuongea na sio kila analolisema ww umjibu acha aongee akimaliza muombe msamaha mwambie naomba nisamehe kama kuna mahala nmekukosea na hiyo iwe kauli yako
 
1. Wewe bado mtoto. Msikilize Mama kuna mienendo anaiona kwako inamtia hofu. Yupo katika mapambano ya kukuokoa.

2. Kinachofanya usirudi home ni hofu ya kukosa uhuru wa kufanya utoto wako unaoufanya ukiwa chuo.

3. Kuna vijitabia umejifunza chuo unajua utashtukiwa na maza na itazusha maneno.
 
Kuna madeni mawili lazima ulipwe hapahapa duniani kabla hujafa,

Kuwadharau wazazi lazima watoto wako waje wakudharau hapahapa kama ulivyofanyia wewe.

Zinaa, kitendo cha kuwazini watoto wa watu lazima naww uje ulipwe Kwa wanao,,

Mchezee tu mzazi wako subiri chamoto utakipa hapa hapa
 
Anza kuona umuhimu wa yale mengi mazuri ambayo mzazi amefanya, no one is perfect...anatamani ukaribu nawe unamuweka mbali, it's natural love, anajali na ndo maana anakua mkali wakati mwingine...

Chukua mda kuwaza maisha bila ya uwepo wake hapa duniani, nadhani itakufanya uapriciate yeye kuwepo...wazaza sometime wanazingua ila ndio wazazi wetu dear...just learn to love and respect them, avoid an necessary quarrels with them
 
mi nilisovu kwakufatisha matakwa yake,maana wazazi wakike huwaga hawajiamini katika malezi,huwaga na mawazo yakukumiliki kifikra na kwa vyovyote vile ili utii kama unavyo mtii baba ako,sio kwamba hakupendi ila anataka uwechini yake uishi anavyotaka yeye kwahili chunguza kwa wale ambao wanamapenzi na mama zao wanaamuliwa kila kitu na mama zao,akiona hufati anavyotaka yeye lazima mfarakane tu.chakufanya sasa ishi kiakili mpe heshima yake kama mzazi usimfokee, mi naendaga namaliza siku2,3 wiki napotea ,simupi nafasi ya kuniamlia kila kitu kama anavyotaka yeye,ilanapokeaga ushauri tu na kukosolewa na ninaondoka akiwa anahamu na mimi tunaagana vizuri kabisa na baraka juu,wazaz wa kike ni changamoto.kama ni maswala ya kiroho nenda kwa mwamposa,maana huwez jua nyuma ya pazia kunanini...unaenda kumcheki una maliza wiki unasepa atajijua mwenyewe ili mladi unamheshimu na kumtii na usimupuuze, maanake ushauri wakike samtaimu hachelew kukwambia ohh babako alikuwa mbaya,nimekusomesha pekeangu,mara ohh mkeo simtaki...
 
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu. Kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa muda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi. Mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kuwa nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani.

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi.

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae. Hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia.

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi.
Achana na matatizo endelevu.
Leta majibu ya maswali yafuatayo kwanza;

1. Wewe ni jinsia gani?
2. Una umri wa miaka mingapi?
3. Una wazazi wote wawili au mmoja?
4. Km una mzazi mmoja,7bu iliyo watenganisha ni kifo ama migogoro?
5. Kama ni mgogoro,je ulikuwa na umri gani kipindi hicho?
6. Je,ulikuwa upande upi kati ya wawili hao?
7. Mvutano wako na mzazi wako una uhusiano na kutengana na mwenza wake?
8. Je,mama kamkaribisha mrithi wa baba yako na wewe hukubariani na uamzi wake?
9. Unadhani mienendo na matendo yako yanakubalika ndani ya jamii yako?

Nitaendelea baada ya kupata mrejesho wako.
 
Back
Top Bottom