Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

hii imekaa kihisia zaidi, au ni huu ujana ujana foolish age??😅
 

Mwanaume, matured au Mwanamke hulipa gharama ya kujenga mahusiano na wazazi wake, You pay that cos, and not em, You do that. Utakuwa tu mjuani, hakuna lingine, kumbuka kama sio malezi yao na kujibisha kukusomesha usingekuwa na chuoni pa kukimbilia.
 


Hii ni meme lakini ina ujumbe mzuri sana sijamaanisha kumtukana mzazi wako no, mchukulie hayo ndio madhaifu yake usibishane nae analosema usitumie nguvu nyingi kumpinga aking'ang'ania kitu mkubalie kama hakina madhara kwako mheshimu.

note; acha kujibizana nae wewe msikilize yanayofaa chukua yasiyofaa acha , ila usimdharau ukiona mnaelekea siko katisha maongezi usimkere
 
Acha Kiburi kijana mheshimu mzazi wako msikilize muelewane.
Unasema Kuwa hutaman kuishi naye hilo ni hisia za Upendo kwa mzazi wako na chanzo chake n ugomvi wa mara kwa mara ndo maana humtaki, solution yake acha Kiburi mpende mzazi wako.
Mzazi ni ndo Mungu wako wa Pili Kuwa makini
 
Akienda kwenye nyumba ya milele utajua umuhimu wake. Kwa Sasa utoto unao mwingi Sana. Maana hata maelezo yako usemi tatizo unazungumzia hisia tu. Kwanini unagombana na mama. Nataka kuongea jambo baya. Mungu anisamehe bure. Acha kuishi na mzazi yako Kama mpenzi unae lala naye kitandani. Na ndiyo maana unakosa heshima kwa mama yako. Tatizo lipo kwako na Ni kweli hauna upendo wa mama yako.
 
hii imekaa kihisia zaidi, au ni huu ujana ujana foolish age??😅
Kihisia zaidi kwasababu mmekuwa mkirumbana mara kwa mara...kwa hiyo hapo source/mzizi ya unavyojisikia kuhusu mzazi wako ni ugomvi wa mara kwa mara...kukosa amani

Kwenye mahusiano ya kimapenzi ukigombana na mpenzi kila wakati mapenzi huwa yanapungua hadi kuisha,sasa kwa case yako ni ngumu wewe kuacha kumpenda mama yako hata mkigombana mara ngapi...zaidi ya kujihisi hivyo unavyojihisi

Anza kujitibu kwa kuanza na source(ambayo naamini ni marumbano mnayokutana nayo)...ukianza kwa kumsikiliza anachotaka ufanye utakuwa poa sana
 
Mkuu mlivyosuluhisha hayakuisha,,,

Mzee wako bado ana doubt mienendo yako...

Hujaprove kwake umebadilika...

Au,

Anaona uelekeo wa wewe kurudia yale yale uliyokua unayafanya...

Hakuna mzazi asiye na best interests za mtoto wake..

Akiwa mkali,ni sababu hataki uwe failure..

Ni wewe kuwa submissive kwake...akikuambia jambo usimletee ujuaji..

Na usimuonyeshe unarudi kwenye ile michezo michafu uliyokua unafanya...

Trick ni kujifanya umekua mtu mzima, responsible..

Fanya yale vijana wa age yako ambao wako responsible wanafanya...

Akiwa na reassurance kuwa uko responsible atakua na amani,na conflicts zitaisha.
 
hayo yote kawaida tushayasuluhisha,

hii imekaa kihisia zaidi sielewi sababu
Hapo kwenye hisia. Nadhani kuna kitu hujakiweka wazi kwenye maelezo yako na ndicho kinafanya uhisi hivyo ndiyo maana wachangiaji wengine wamekuuliza kama unavuta bangi kwasababu haiwezi tu kuwa eti hujiskii kukaa karibu nae. Kama na wewe hujui tatizo ni nini basi mwenye tatizo ni wewe na sio mzazi wako. Jitafakari
 
ndio mkuu ndo najaribu kupeleleza
 
Kwani bangi ina shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…