Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Watu wamecoment upande mmoja wa lawama kwa kijana pekee, lakini wamesahau pia sisi wazazi tuna shida. Kuna mzazi amchukia mwanae mpaka dunia inashangaa...mwingine anaomba hela kila siku na mtoto asipompa ni maneno mazito yatamtoka mzazi mpaka mnajiuliza ni mzazi wake kweli?!

Kama ni shida basi ziangaliwe pande zote. Ila kwa maelezo yake between the lines huyu dogo ana mzazi toxic...(probably mama yake ni mchaga, sorry to say this)
 
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu.... na kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa mda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.....

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi.... mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kua nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani....

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi....

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae.... hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia....

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi....
kijana acha utukutu...

Kwa mzazi yakupasa kujinyenyekeza hata kama hakupendi au anakuona chizi maarifa.. peleka na vizawadi mpe komaaa hadi atafungua moyo.. peleka zawadi nzuri apendayi
 
Una tatizo linataka kufanana na mimi.

Nikiwa mbali tunakuwa na uhusiano mzuri na mama ila nikiwa home duu tunagombana sana bila sababu za msingi.Kwasasa nilishafanya maamuzi nitakaaa huku niliko ili tuendelee kuwa na uhusiano mzuri.
tafta suluhisho mzee, generally ni vibaya
 
Siku ukimpoteza huyo mzazi wako ndio utaijua thamani yake,but itakua too late,

Tatizo lako unataka kushindana na mzazi wako,

Kuzozana nae ina maana kila mmoja kati yenu anajiona yupo right ila wewe ndio ulitakiwa umsikilize mzazi wako,wala usijifanye mjuaji mbele yake,

Hata kama atakwambia "Tembo anaweza kuruka angani" wewe mkubalie tu kua yupo sahihi,hutogombana nae tena na huo ndio utakua mwisho.
 
Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi
Sema ukweli, wakubwa wakusaidie😂😂
 
Acha kujidanganya chaliangu jishushe tulizana ishi vizuri na mama, Kuna mda wamama hua wanazingua lkn kuna namna ya kistaarabu unaweza ukaepuka mzozano na yy!

Kwa saiv unaweza kua unamtunishia misuli lkn ipo siku utajuta utatamani hata usikie sauti yake bila kujali hyo sauti inasema nn! Epuka ligi na mzazi ishi vzr na mzazi
 
Back
Top Bottom