Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Kama hii misimamo yako ya u atheist ni mpaka nyumbani lazima mzazi wa kiafrika avurugwe.

Mzazi wa kiafrika akitajie Mungu halafu umwambie dhibitisha kama huyo Mungu yupo lazima mgombane
hii kweli ni ishu sikatai😅
 
Siku ukimpoteza huyo mzazi wako ndio utaijua thamani yake,but itakua too late,

Tatizo lako unataka kushindana na mzazi wako,

Kuzozana nae ina maana kila mmoja kati yenu anajiona yupo right ila wewe ndio ulitakiwa umsikilize mzazi wako,wala usijifanye mjuaji mbele yake,

Hata kama atakwambia "Tembo anaweza kuruka angani" wewe mkubalie tu kua yupo sahihi,hutogombana nae tena na huo ndio utakua mwisho.
Huku kwetu ndio tunajali sana wazazi hata kama wanatukosea, tunajirudi kiimani na kiutamaduni kwamba mkubwa hakosei.

Kuna siku nilisoma page fulani Instagram mtoa post alitaka walio na mama zao wapo hai basi wanafuraha sana na washukuru sana Mungu.

Wachangiaji wengi walikuwa wanasema huyo mama asiwe kama mama yangu,..mama yangu hanipendi,...mama yangu hajali lolote kuhusu mimi nk

So hata huku wapo wazazi wanaofanya matendo au kuonesha hisia za chuki kwa watoto wao.
 
1. sijawahi kubishana nae, akigomba hua nakimbia
2. sijawahi kumtukana
3. nikiwa nyumbani nakua mpole

ndio maana nkasema hii ishu ni ya kihisia zaidi mengine hua tunayamaliza
How kwahiyo unahisi unaonewa? Unahisi akupendi? Kuna vitu bado unaficha ujataka kuweka wazi hapa unaogopa unajaribu kuonyesha ubaya wa mama yako tu mimi siwez kukutetea mpaka uwe open
 
Asipojifunza hapa labda dishi limeyumba,Mimi nilikua napewa maneno makali na bi mdashi nashikwa na hasira kweli coz mi binadamu navunga!
Akishamaliza napewa chakula nakula tunapiga story mbili tatu tunaanza kucheka Sasa

Nikajifunza kitu kimoja wanawake wameumbiwa mdomo na hasa akina mama kazi zao kubwa biological ni kulea

Mama yako hawezi kukuona unaangamia akanyamaza hata kidogo hata kama umetenda kakosa kadogo
 
How kwahiyo unahisi unaonewa? Unahisi akupendi? Kuna vitu bado unaficha ujataka kuweka wazi hapa unaogopa unajaribu kuonyesha ubaya wa mama yako tu mimi siwez kukutetea mpaka uwe open
sijasema yeye ni mbaya, nimesema yaani nimepoteza mazoea nae sijiskii vizuri kukaa nyumbani, najua ni vibaya najaribu kuzuia hali ila nashindwa
 
Ahahhaha kuna siku aliwai kusema anavuta bangi hapa hapa je kuna Mzazi ambae anapenda kuona mwanae anavuta bangi?
Huyu dogo mi nampenda ila hata mi ningekua mama yake lazima ningekua nqmbananisha sana.
Imagine bangi.
Ni atheist halafu kuna sehemu niliona kaandika eti yeye kwenye mizagamuano haoni shida kushikwa popote.

Ukute mzazi wake ana stress keshaona mwanae hayuko sawa.Huyu nae akirekebishwa anaona anafuatiliwa maisha yake.
 
Mimi naona njia nzuri ni kuepuka ugomvi na njia ni kukaa mbali naye tu hakuna namna.

Kuna wazazi wanazingua sana, nilikua na rafiki yangu aisee mama yake alikywa mzinguaji kweli kweli jamaa alikuwa analua kabisa anamwambia mama unaniaibisha maza mzinguaji kweli ni mshangazi plus chapombe.

Jamaa aliondoka kabisa mkoa na hajarudi kwao hadi leo tangu 2010 na yupo happy na life lake. Ila aliondoka kweli kweli
 
Huyu dogo mi nampenda ila hata mi ningekua mama yake lazima ningekua nqmbananisha sana.
Imagine bangi.
Ni atheist halafu kuna sehemu niliona kaandika eti yeye kwenye mizagamuano haoni shida kushikwa popote.

Ukute mzazi wake ana stress keshaona mwanae hayuko sawa.Huyu nae akirekebishwa anaona anafuatiliwa maisha yake.
Kumbe mnamjua [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna shida ya kiroho hapo
Na hapo ndio Baraka zake zitaendelea kufungwa..

Kadiri atakavyokuwa anapambana atoke kimaisha ndivyo Kwa nguvu hiyo hiyo Mama yake atakuwa anamuinukia..

Hatimaye ni mvurugano daily na kila atakachogusa hakitakitakuwa.

Mleta Mada sijui ni muamini katika Imani ipi? Ilaa sidhani kama anajua nguvu ya wazazi katika ulimwengu..
 
Back
Top Bottom