Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Siku ukimpoteza huyo mzazi wako ndio utaijua thamani yake,but itakua too late,

Tatizo lako unataka kushindana na mzazi wako,

Kuzozana nae ina maana kila mmoja kati yenu anajiona yupo right ila wewe ndio ulitakiwa umsikilize mzazi wako,wala usijifanye mjuaji mbele yake,

Hata kama atakwambia "Tembo anaweza kuruka angani" wewe mkubalie tu kua yupo sahihi,hutogombana nae tena na huo ndio utakua mwisho.
Dogo ataki kusikia
 
Nimekua nikipata changamoto kwenye mahusiano na mzazi, kuna kuwa hamna maelewano kati yetu, tunagombana sana, hatuwezi kukaa sehemu moja tukazungumza usitokee ugomvi kati yetu.... na kinachonishangaza zaidi, nikijaribu kuangalia sababu sielewi, hii hali imekua ikiendelea kwa mda mrefu sasa na inanipa mawazo kwa kweli.....

Sasa hii hali imenipelekea kukwepa kwenda nyumbani kwa miaka karibia mitatu sasa, nipo chuo, na nikiwa likizo najiweka mbali na mzazi.... mfano mwaka jana ilitokea mzozo kwelikweli, nilikua nimefunga chuo nikagoma kufikia kwa mama alipokua kikazi, kwasababu hakuweza kua nyumbani kwa muda huo, tuligombana sana mpaka ikafikia hatua ya yeye kunikaripia 'usipokuja kuniona wewe sio mwanangu' basi ikabidi niende kishingo upande ila sikua na amani....

Tumeendelea kuishi hivi hivi kwa kulumbana mpaka hivi sasa, bado ugomvi unatokea mara kwa mara, hivi sasa tumefunga chuo nimebaki huku huku chuo kufanyia field, imekua mzozo kweli kweli mara aniambie simpendi ndo maana sitaki kwenda kumuona, leo tumezozana anadhani naishi na binti huku nimempa mimba, anataka aje kuona nnapoishi....

Najua mtaona kama kuna maovu yangu naficha, ndio maana nagombana na mzazi, nakubali kuna makosa nimefanya nikagombana na mzazi lakini tuliyamaliza, ila hii hali ni tofauti, nikiwa karibu na mzazi nahisi vibaya, sijui kwanini, natamani tu nijiweke mbali nae.... hii hali inanitesa sana, na nikifikiria huyu ndo mzazi pekee niliyebaki nae, naumia zaidi, natamani kuithibiti hii hali, ila inajirudia....

Najua humu kuna watu wazima mmeshapita ujana na changamoto zake, hebu nishaurini kwa mtazamo wenu nifanyeje ili kurudisha mahusiano na mzazi....
Bado uko field baada ya miaka 3?
Unapiga M.D ama?
 
We Chalii skia hata Mimi nishawahi kukutana na changamoto kama yako na Nina mzazi mmoja tu my lovely mummy dingi alitutema

Fanya hivi jifanye wewe ndio una makosa shuka chini kabisa,akikuita nenda akikuambia ufanye chochote ndani ya uwezo wako just do it

Utanishukuru arif
 
Acha utoto na ubadilike hakunaga mkaidi mwenye baraka maishani badilisha nyendo zako yaani usielewane na mzazi wako unataka uelewane na nani?? Siku huyo mzazi wako akikuvua na kukupotezea itakughalimu sana kuirudisha trust yake, lakini piaa vijana wa kileo mmekuwa washamba ukifika chuo unajihisi umekuwa , msomi wewe genius wewe mjanja ni wewe yaani kiufupi watoto wa dizaini yako mpo wengi siku hizi sasa kazi ni kwako utengeneze au ubomoe kesho yako

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Sikia nikupe short story fupi ya mimi nikiwa age yako
Mimi mama yangu alikuwa ataki mambo ya last born ila baba yangu ndio alikuwa ananilea ki last born siku alipo fariki nilikuwa nalia kila siku naona naonewa yaani niombe hela uninyime nashusha machozi na sms ndefu sana

Picha inaanza baada ya baba kufariki dada angu akasema nitolewe shule ile ya highlands nipelekwe jitegemee jkt mgulani pale nimepelekwa na mama siku iyo naona watu waanachezea jalamba ile mbaya nikapewa amr moja niende kuchange nguo nikachange nikarudi nalia namlaum mama kwanini umenileta shule hii

Nilikuwa na majibu mabaya sana nikiinza kugombana na mama yangu hakuna mtu anaweza ninyamazisha katika umri uhu nilipo pelekwa jitegmee adabu ilikuja yenyewe nikawa mtoto mwema nakumbuka siku moja nilipo rudi likizo wakati naondoka mam alisema safari.hii nimenenepa sana hakuna makelele na katika kipindi hiko namtukan ikifika swala la ada ya shule ananiita kabisa alikuwa anasema unaona unavyonitukana lakini na kaa kimya na sijawai kukutishia kuwa silipi ada kwanini najua ipo siku utabadirika achana na ujeuri hakuna mtu mwingine wakukusaidia ukinitoa mimi hapa wimbo wak ulikuwa uho

Nini nataka kusema mzazi ana macho mawili akigundua mtoto wake hayupo kama vile anavyotaka lazima awe mkali sana kuliko kawaida acha ujeuri jishushe mimi nilikuwa natumia udhaifu wa mama yangu kumpunguza hasira kwa kumpikia chakula anachokipenda angalia pia kwa mzazi wako anapenda nini hasa then uwe unafanya mkuu hii imasaidia sana

Pamoja na ubay wangu wote mama yangu hajawai thubutu kuongelea ubaya wangu kwa watu bali siku zote huwa ananisifia na kuweka tumain kubwa
 
Huwezi kushindana na mzazi wako ili eti wewe ndio uwe juu yake au wewe ndio uwe sahihi kuliko yeye,

Mzazi ni mzazi tu hata kama wewe utakua umesoma kiasi gani au una utajiri wa kiasi gani,kadiri umri wake utakavyokua unasogea ndio atakuja kukumbuka hizi comment.
Ujakosea mkuu psychology ya huyu mtoto ni ubishi sana kama unataka kujua fwatlia nyendo zake utagundua mshamba_hachekwi ataki kuelekezwa pale ambapo hajui pia anajiona mkubwa ataki kukubali yeye bado mtoto ilo ajataka kukubali kabisa
 
Sikia nikupe short story fupi ya mimi nikiwa age yako
Mimi mama yangu alikuwa ataki mambo ya last born ila baba yangu ndio alikuwa ananilea ki last born siku alipo fariki nilikuwa nalia kila siku naona naonewa yaani niombe hela uninyime nashusha machozi na sms ndefu sana

Picha inaanza baada ya baba kufariki dada angu akasema nitolewe shule ile ya highlands nipelekwe jitegemee jkt mgulani pale nimepelekwa na mama siku iyo naona watu waanachezea jalamba ile mbaya nikapewa amr moja niende kuchange nguo nikachange nikarudi nalia namlaum mama kwanini umenileta shule hii

Nilikuwa na majibu mabaya sana nikiinza kugombana na mama yangu hakuna mtu anaweza ninyamazisha katika umri uhu nilipo pelekwa jitegmee adabu ilikuja yenyewe nikawa mtoto mwema nakumbuka siku moja nilipo rudi likizo wakati naondoka mam alisema safari.hii nimenenepa sana hakuna makelele na katika kipindi hiko namtukan ikifika swala la ada ya shule ananiita kabisa alikuwa anasema unaona unavyonitukana lakini na kaa kimya na sijawai kukutishia kuwa silipi ada kwanini najua ipo siku utabadirika achana na ujeuri hakuna mtu mwingine wakukusaidia ukinitoa mimi hapa wimbo wak ulikuwa uho

Nini nataka kusema mzazi ana macho mawili akigundua mtoto wake hayupo kama vile anavyotaka lazima awe mkali sana kuliko kawaida acha ujeuri jishushe mimi nilikuwa natumia udhaifu wa mama yangu kumpunguza hasira kwa kumpikia chakula anachokipenda angalia pia kwa mzazi wako anapenda nini hasa then uwe unafanya mkuu hii imasaidia sana

Pamoja na ubay wangu wote mama yangu hajawai thubutu kuongelea ubaya wangu kwa watu bali siku zote huwa ananisifia na kuweka tumain kubwa
1. sijawahi kubishana nae, akigomba hua nakimbia
2. sijawahi kumtukana
3. nikiwa nyumbani nakua mpole

ndio maana nkasema hii ishu ni ya kihisia zaidi mengine hua tunayamaliza
 
Back
Top Bottom