1. Inawezekanaje watu wanatekwa na watekaji pengine tunawafahamu lakini tuna kigugumizi cha kuchukua ngumu na za haraka dhidi ya hao watekaji?
2. Inawezekanaje wakati mwingine mtu anatekwa hadharani mchana kweupe na mbele ya umati wa watu lakini waliopo hawachukui hatua kuwadhibiti na kuwashikisha adabu watekaji?
3. Inawezekanaje mtu aliyekupora ushindi wa uchaguzi ambaye unakaa naye mtaa mmoja au mmepanga nyumba moja kila siku mnaonana unashindwa/mnashindwa hata kumuuliza tu kwamba, kwa nini aliiba kura?
Zamani za utoto wangu kule kijijini watu walikuwa wababe sana. Ilikuwa wakichangiana watu labda wawili kukupiga, wewe unasubiri siku atakapokuwepo mmoja kati yao. Hapo ilikuwa unamshughulikia kweli kweli. Ilikuwa ukifanya hivyo, siku nyingine hawarudii tena kukuonea.
Mimi nathubutu kusema, hawa watekaji na waovu wengine wote TUMEWALEA sisi wenyewe. Angetekwa mtu mmoja tu nasi tukamtafuta kwa wivu mkubwa huyo mtekaji na tukamshughulikia kikamilifu kwa mujibu wa sheria, leo hii kusingekuwa tena na wimbi la utekaji. Hatujachelewa sana, kuanzia sasa tusiruhusu tena Mtanzania mwingine atekwe au aumizwe.
Nawasilisha.