Nahisi kuna kitu hakipo sawa kwa sisi Watanzania

Nahisi kuna kitu hakipo sawa kwa sisi Watanzania

Kweli mtu anamwagiwa mafuta na kuchomwa moto, huku mnaangalia na watoto wenu

Kisa kaiba shati la mtumba?
Kweli kabisa naamini kuna tatizo kubwa sana kwenye jamii.

Niliwahi kumuokoa kijana mdogo sana kwa wizi.
Na kuzuia mob wasimuue
Sasa nyie mnaangalia mtu anapambana kuingizwa kwenye gari mnaangalia tu.
Halafu bado mna audacity wa kuchukua na video kabisa
Poleni sana
Ulifanya vizuri sana, hata mimi nilimwokoa kijana mmoja alikuwa amebanwa kisawa sawa na njemba mbili. Nilichokifanya nilimgonga mmojawapo na jiwe akaanguka chini, baada ya hapo na yule wa pili akalala mbele, kwa hiyo yule kijana akawa amepona.
 
1. Inawezekanaje watu wanatekwa na watekaji pengine tunawafahamu lakini tuna kigugumizi cha kuchukua ngumu na za haraka dhidi ya hao watekaji?

2. Inawezekanaje wakati mwingine mtu anatekwa hadharani mchana kweupe na mbele ya umati wa watu lakini waliopo hawachukui hatua kuwadhibiti na kuwashikisha adabu watekaji?

3. Inawezekanaje mtu aliyekupora ushindi wa uchaguzi ambaye unakaa naye mtaa mmoja au mmepanga nyumba moja kila siku mnaonana unashindwa/mnashindwa hata kumuuliza tu kwamba, kwa nini aliiba kura?

Zamani za utoto wangu kule kijijini watu walikuwa wababe sana. Ilikuwa wakichangiana watu labda wawili kukupiga, wewe unasubiri siku atakapokuwepo mmoja kati yao. Hapo ilikuwa unamshughulikia kweli kweli. Ilikuwa ukifanya hivyo, siku nyingine hawarudii tena kukuonea.

Mimi nathubutu kusema, hawa watekaji na waovu wengine wote TUMEWALEA sisi wenyewe. Angetekwa mtu mmoja tu nasi tukamtafuta kwa wivu mkubwa huyo mtekaji na tukamshughulikia kikamilifu kwa mujibu wa sheria, leo hii kusingekuwa tena na wimbi la utekaji. Hatujachelewa sana, kuanzia sasa tusiruhusu tena Mtanzania mwingine atekwe au aumizwe.
Nawasilisha.
Nikweli tumewalea sisi wenyewe kama nyoka baadae wamekuwa machatu ya kutumeza tulio walea
 
Ulifanya vizuri sana, hata mimi nilimwokoa kijana mmoja alikuwa amebanwa kisawa sawa na njemba mbili. Nilichokifanya nilimgonga mmojawapo na jiwe akaanguka chini, baada ya hapo na yule wa pili akalala mbele, kwa hiyo yule kijana akawa amepona.
Vizuri sana umefanya.
Sijui kwanini watu wanakuwa waoga au kutokujali mtu anapoona anauwawa kabisa au kupigwa.

Umefanywa uungwana sana
 
Back
Top Bottom