Poleee my cisy...kama umefanya yote hayo na bado jamaa haeleweki, maybe anapitia magumu anashindwa kukwambia, hebu lia na Mungu wako aokoe ndoa yako, ipeleke ndoa yako kwa Mungu...mrudishe mumeo katika mstari wa kumjua Mungu,something is wrong na bila kukifahamu mtazidi kupotea, anza kubadilika, anza kuabudu kwa kumaanisha, ongea na Mungu kila unapohisi kufanya hivyo, lia sana mbele zake, angalia wapi ulikosea, kama aliona unafaa kuolewa kwanini hayo? Sema na Mungu dada, hakikisha mumeo anamjua Mungu, hakikisha anasali tena kwa kumaanisha, sio rahisi na itachukua mda ila majibu utayaona, zaidi usiache kumuombea, endelea kua na subira na huruma juu yake, angalia wapi ulienda tofauti nae..
Update ndoa yako ( fanya vitu vipya , like new dishes, kama alishazoea usiku ni wali samaki ,try new dishes, sometimes muombe mpike pamoja, try new outfit , ikibidi likizo peleka watoto kwa bibi, mpate mda wawili tuuu,maybe anamiss ile kua wawili..
Make him feel special)....
Jipende,tafuta new hobbies, like kusoma hata vitabu, movies,football( karibu timu la taifa yanga[emoji28][emoji28][emoji28])...just be happy ma...life is too short to stress yourself, wakati unapambana kumpa furaha, usijisahau na wewe...
Muheshimu sana mumeo,.stop complaining, maybe hiyo fact ya kuacha kazi unaizungumzia sana kwake kama unavyoielezea hapa, like unajuta kwa vile maisha yamekua, kutoka kupaka lotion hadi kupaka Vaseline...ni kwamba hapana pesa ya kununua lotion au umeamua tuu? Maybe majukumu yamemzidia anashindwa kukwambia, Kuna mdau ameshauri kuhusu kufanya ufugaji, hebu chakarika upate ya lotion kwanza mamito...I think hata kuku wanaweza kukuweka bize ukapunguza makasiriko na huyo kiumbe...
Make him miss home....zaidi ya yote , Mungu akupe nguvu dada...ukiona bado magumu na yanakuzidia ,wazazi na watumishi wa Mungu hapa ni mahala pao Sasa...ukimya ukizidi huleta mauti.....
Be blessed....