Nahisi nimekuwa mlevi wa Coffee, natamani kuacha

Nahisi nimekuwa mlevi wa Coffee, natamani kuacha

Huwa ana short temper, basi huwa mimi na Manyanza tunamchokoza akipandisha mori tunacheeka😂😂😂😂

Hivi Satoh Hirosh ni njere?moran
Hivi Manyanza ni mkaazi wa Dar? Najua wewe upo chuga.

Siku Mnione mpate kahawa kidogo wakuu. Kahawa ni Bora kwa afya. Bodi ya kahawa (TCB) soon itaanza kampeni ya kuhimiza unywaji wa kahawa hapa Dar es salaam,watakuwa na migahawa inayotembea ya kahawa.
 
Mm isio nasukari ndio napenda zaidi. ..naweza kunywa na kitu chochote. .kwangu max ni 2 cups na maji mengi yakunywa. .kunywa maji mengi nikm una dilute ilekahawa
Unafanya vema.

Kahawa inapaswa kunywewa pasi na sukari ili kupata ile taste halisi.
 
Haina madhara. Japo inashauriwa kubadilibadili viungo usile aina moja ya viungo kila siku. Kubadili ni muhimu. Lakini usitumie tu viungo vyenye nyongeza.
Huwa nakunywa asubuhi ila siku za kazi Huwa sinywi kilasiku mara moja moja ila jioni Huwa nakunywa ila shida ndo iyo kujaza tangawiz na black pepper
 
Unafanya vema.

Kahawa inapaswa kunywewa pasi na sukari ili kupata ile taste halisi.
Hivi inasaidia nn kitaalamu
Pwani niliuliza kwann Wazee wanakunywasana kahawa nikaambiwa wanatak wasilale waikeshee 😂😂
Ila kunakipind nilitak kupunguza uzito nikawa natumia nachanganya na limao na tangawiz aisee nilipungua balaa ila sijui inasaidia nn hasa mwilini
 
Kukosa usingizi. Kinywa kutoa harufu mbaya, inaweza kuamsha vidonda vya tumbo, matumizi makubwa na yaliyopitiliza ya kahawa yanaongeza acid mwilini ambayo ndio huleta shida ya vidonda vya tumbo kama unavyo.

Kimsingi unatakiwa kuwa moderate kwenye matumizi ya kahawa sababu ni kinywaji ambacho kina umuhimu mwilini ila matumizi yake yanataka umakini na balance.

Kunywa maji kwa wingi ili ubalance. Tumia kahawa baada ya kupumzika vizuri yaani usitumie ukiwa katika hali ya kuchoka na haujapumzika. Kama una pressure ya kupanda kahawa haitafaa. Kama una pressure ya kushuka kahawa ni nzuri kwako.

Enjoy kikombe chako cha kahawa.

By the way mimi kahawa yangu ambayo napenda tumia ni Brand ya Nestle ile chupa yake ni ya kioo. Halafu ni ya chenga chenga kubwa yaani sio unga ule mlaini kama hii kahawa ya Africafe.

Huwa napenda kutumia maziwa fresh ya ng'ombe, ngamia au mbuzi yale mazito sana.

Kuiandaa huwa nachukua maji ya moto nachemsha natia kwenye chupa ya chai kwanza kwaajiri ya baadae.

Tumia maziwa fresh ya mnyama yoyote kati ya hao nimetaja. Maziwa fresh yakichemshwa huwa yanaweka utandu kwa juu wakati yanapoa kama cream nzito sana.

Huwa nauchota kwa kijiko kikubwa kile cha kuchotea mboga nauweka huo utandu kwenye chombo pembeni kwaajiri ya kuhifadhi kwenye friji. Ili upate huo utandu maziwa hakikisha maziwa yawe yale ambayo yana mafuta ambayo yanatokana na ng'ombe,mbuzi au ya ngamia wanaolishwa vizuri wanatoa maziwa yana unjano njano. Hayo maziwa ukichemsha yanatengeneza layer kubwa ya hii cream nzito.

Unachukua ile cream ya maziwa iliyo kwenye chombo unachanganya na maziwa ya unga unapiga kama vile unavyopiga yai kwenye kibakuli ili ijichanganye freshi.

Kisha unachukua kahawa unakadiria uhitaji wako. Mimi huwa natumia mug so huwa natumia kijiko kikubwa cha chakula (table spoon [emoji1633]) naweka viwili kwenye kikombe.

Naweka yale maji ya moto kidogo yaani kama ujazo wa kale kakikombe kadogo sana ka chupa ya mtoto ya uji. Naweka maji kidogo ya moto ili kuiyeyusha ile kahawa ila isiwe nyepesi sana sababu ya kikwekwa maji mengi. So unaweka kidogo hayo maji ila iwe nzito sana isiwe nyepesi utaharibu.

Kisha napasha ile cream kwenye moto kidogo tu iwe ya moto kisha naitoa. Namimina kwenye ule mchanganyiko wa kahawa na maji ya moto. Then natia sukari, mimi huwa natumia kijiko kikubwa kimoja na nusu cha sukari. Then nakoroga.

Inakuwa nzito mithiri ya mtindi so unakuwa ni cream coffee nzuri balaa. Hiyo huwa natumia sana weekends nikiwa nimemka baada ya kulala.
Alooooo…….Ninashukuru Kwa elimu nzuri uliyoitoa.

Ubarikiwe sana mkuu🤛🤛🤛
 
Mimi nalima kahawa usinizoee kijana wa kimaasai😆
Mimi ndiyo mteja wako Sasa pale mnadani Kama wewe ni mkulima. Nanunua na kuuza duniani. Nina wateja Russia,America,Canada, UK,Japan,south Korea,south Africa,German,na sehemu zingine.

Nina mashine za kuprocess Kama xeltron color sorter 9100-LEDS RTK na 12000 LEDS CTK,Pia nina coffee gravity table,destoner na heavy plant bulkin machine.
 
Alafu sijawahi kuiona kahawa yenyew pure Yani mbegu zake zenyew live sijawah ziona Wala kuzigusa naziona kwenye makopo n tv😂😂😂@sato Hirosh
 
Hivi inasaidia nn kitaalamu
Pwani niliuliza kwann Wazee wanakunywasana kahawa nikaambiwa wanatak wasilale waikeshee 😂😂
Ila kunakipind nilitak kupunguza uzito nikawa natumia nachanganya na limao na tangawiz aisee nilipungua balaa ila sijui inasaidia nn hasa mwilini
Nifuate pm nikuambie inasaidia Nini mkuu.

Glenn nitakuwa bize kidogo kutoa somo la kahawa 😅😅😅..Uachage wivu Sasa na wewe!!
 
Back
Top Bottom