Nahisi nimeuziwa mbuzi ndani ya gunia.

Nahisi nimeuziwa mbuzi ndani ya gunia.

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
5,313
Reaction score
2,657
Tayari nimetoa ng'ombe za mahali kwao na binti Evelyn Salt ndoa ilipangwa jumamosi ilee iliyopita, mshenga pamoja na kamati nzima walinihakikishia kuwa ndoa itafungwa saa tisa jioni pia walinitaka ninunue kitanda kingine kipya niachane na kile cha futi 2.5 kwa 6 wazo ama ushauri toka kwa mwenyekiti Baba V alipendekeza niwe na kitanda kikubwa kama chake cha futi 10 kwa 6,jambo hilo nililifanikisha mapema sana kwa msaada wa dada zangu Arabela na king'ast. Hapa nahitaji msaada wenu wa kisheria kabla sijawaburuza mahakamani mshenga na mke wake watu8 mwenyekiti wa ndoa Baba V copy kwa: Arushaone Madame B charminglady Mamndenyi na mumewe Vin Diesel manoah bila kumsahau rafiki yangu kipenzi Dr.zero sharifaa na Bishanga pamoja na hayo natoa tangazo kwa mwanasheria yeyote atakae tetea haki yangu nitamlipa kiasi chochote cha pesa.
 
Last edited by a moderator:
manoah naomba kesho niwe mgeni wako nataka kuzaliwa kwako jana nilipita hapo nikamuona sharifaa
 
Last edited by a moderator:
Wee Slave vipi tena.!?? si ulisema mmefunga ndoa ya kimila kimyakimya kuepuka wanga, kila mtu hapa jamvini anatambua kuwa wewe na Evelyn Salt ni wanandoa, sasa malalamiko yametoka wapi..!?? njooni huku King'asti , Arabela na MMAHE mnipe ufafanuzi wa hili jambo
ugomvi wangu mimi na wewe ni juu ya Evelyn Salt kuwa anakuota kila siku,istoshe kuanzia juzi sijamuona nyumbani kwao mpaka nimefikia maamuzi hayo ujue kweli limenikaba.
 
Last edited by a moderator:
ugomvi wangu mimi na wewe ni juu ya Evelyn Salt kuwa anakuota kila siku,istoshe kuanzia juzi sijamuona nyumbani kwao mpaka nimefikia maamuzi hayo ujue kweli limenikaba.

Suala la kuniota sidhani kama ni baya na ukizingatia mie ndo mwenyekiti wenu niliyefanikisha kuungana kwenu, kwa hiyo anaweza kuwa ananiota kwa mema tu, kuhusu hili la kutoonekana nyumbani inabidi tukae kama kamati pamoja na mshenga na dada zako tujue tunafanyaje
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom