Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Mkuu mimi naomba kufahamu jambo hapa ili nitoe ushauri wangu, Ni unatamani kufa au unaogopa kufa? kipi kati ya hivi vinakuchochea zaidi?

Kama ni unatamani kufa, acha ujinga
Kama ni unaogopa kufa, fanya mazoezi, kula vizuri, jumuikana watu.

Fikiria unataka kukwepa majukumu ya kulea watoto watatu kwa kisingizio cha ndoto zako hazijatimia ivyo unaona dalili za kufa. Bro!, sikufokei ila hapa unazingua. Nini kilifanya ukawa na watoto wote hao ili hali unaona wazi hujajipata bado?.

Wapo watakaokupa faraja na maneno matamu ya kukuonea huruma, ila hayo hayasaidii kuinua uchumi wako na familia yako, bali yatakuongezea sonona tu na kujiona mtu wakuonewa huruma huruma.

Amka pambana, acha mawazo a hovyo ya kujikatia tamaa. Dunia ni katili haihitaji kuishi kwa kuonewa huruma

Ni hayo tu Mkuu Prince Mhando
 
Pole sana,jikaze maisha ndivyo yako hivi
Peleka maisha polepole na raha jipe mwenyeweuna tatizo la Afya ya akili nakushauri utafute mtaalam kwa msaada zaidi
 
Kama maisha yamekuwa tofauti sana na matarajio yako epuka kulazimisha maisha kuja vile umepanga.

Fanya yafuatayo

1. KUWA MWEPESI KUBADILISHA MSIMAMO

Kama binadamu wengine utafanya makosa katika maamuzi yako.Kwa wastani binadamu hufanya makosa kwa 70% ya maamuzi yake ya kila siku hivyo uwezekano wa kufeli katika malengo yako ni mkubwa sana.

Alipata kusema Viktor Franklin kwamba kama huna uwezo wa kubadilisha hali ambayo unapitia,unatakiwa kubadilisha mtazamo wako eneo hilo.

Kutumia njia ileile ambayo haileti matokeo mazuri itafanya upoteze muda mwingi sana badala yake badili njia yako ikiwa njia ya awali haina matokeo mazuri

2. DHIBITI KILE KIPO NDANI YA UWEZO

Alisema Marcus Aurelius mfalme wa Roma ya kale kwamba upo na nguvu ya kudhibiti akili yako sio matukio yenye kutokea nje yako.Huwezi kupanga nini kitokee katika maisha yako ila unapanga ufanye nini kwa kila tukio lenye kutokea maishani mwako.
Huwezi kudhibiti tabia au maamuzi ya wengine.Baadhi ya watu ni wavivu wa kufanya maamuzi,wengine ni wepesi,wapo wenye huruma wapo wasiokuwa na huruma,wapo wenye kujali mahitaji ya wengine wapo wenye kujali maslahi yao binafsi

Watu wa aina hiyo utakumbana nao .
Ikiwa mafanikio yako hutegemea sana maamuzi ya wengine basi uwezekano wa kufeli eneo hilo ni mkubwa sana kwa sababu kila mtu huwa na vipaumbele tofauti

3. FANYA YENYE KUKUSAIDIA

Kama umekata tamaa ya maisha jiulize kama huo ni uamuzi sahihi au Lah ,je unaweza kubadilisha maisha yako kwa kukata tamaa?
Epuka kulaumu mwenendo wa wengine,epuka kulaumu mbinu za mpinzani wako,epuka kurekebisha tabia za wengine,tumia muda wako kuboresha tabia yako utakuwa na amani na utulivu
Makosa ya wengine waachie wenyewe,tabia za wengine waachie wenyewe, maamuzi ya wengine waachie wenyewe wekeza nguvu kurekebisha tabia zako tu ndio zipo ndani ya uwezo wako

4.KUWA MVUMILIVU
zipo nyakati unaweza kufanya kila kitu kwa usahihi lakini hupati matokeo mazuri unaweza kuvunjika moyo lakini hayo ndio maisha yalivyo.
Zingatia kwamba hakuna kitu chochote chenye kudumu milele haijalishi hali ambayo unapitia ni ngumu sana au nzuri sana haiwezi kudumu milele.
Kuna nyakati hali nzuri ya maisha inaanza kwa kuleta majanga makubwa sana yenye kuumiza na kuvunja moyo hivyo kuwa mvumilivu eneo hilo

5. HUZUNI NA FURAHA

Kama upo na furaha sana hivi sasa na endapo utachunguza sana chanzo cha furaha yako utagundua kwamba sio furaha bali ni yale màumivu makali sana moyoni ambayo ulikuwa unapitia ndio yamegeuka kuwa furaha.
Kila chozi la furaha huwa ni matokeo ya kupitia màumivu makali sana na uchungu moyoni.Hivyo wingi wa màumivu moyoni mwako huwa wingi wa furaha yako ikiwa hutokata tamaa eneo hilo.
Ikiwa umejiwekea malengo vikwazo vitakuja njiani kukuonyesha njia sahihi tofauti na ile ulipanga wewe kuitumia
Vikwazo vya mafanikio yako ndiyo njia ya mafanikio yako.
Usilaumu vikwazo angalia mbinu zako za kukabiliana na vikwazo hivyo eneo hilo ndio nguvu zako zipo.
Prince Mhando
 
If you truely love your kids, then be strong!
 
Nenda Prince. Nenda mwanamfalme. Nasi safari yetu moja. Bila shaka hujamuachia mkeo mzigo mzito wa malezi. Angalau umeweka akiba ya ada ya miaka miwili mbele kwa kila mtoto. Nenda kaka. Nenda kiume
 
You nailed it Dada, Watu tumepitia magumu sana na bado tume survive and still life goes on. Kuna Uzi niliuandika nitaku tag
 
Sitegemei wewe prince kuandika ulichoandika.
Don't expect much from this world we are here kwaajili ya kuishi.
Achana na mambo yako ya kukata tamaa.
Wapo wenzako tunapitia kadhia mbali mbali. Na hatukati tamaa wewe ni nani?
Tunaachana na wapenzi wetu,
Biashara zinakufa mpaka tunarudi kulala ndani.
Maugomvi ya kila siku. Na tuna familia zinaishi vzuri ila ttunaumia wenyewe moyoni.
Acha hizo bwana. Maisha haya ya muda mfupi, usidhihaki maisha bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…