Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Mkuu wewe ni suicidal? Hilo ni tatizo la akili labda mshauri anaweza kukusaidia.
Unajua maisha ni kupambana usi give up wala kuback up.
Haijalishi nini unapitia pambana maana aliposema tutakula kwa jasho letu, believe me... hakutania
shukrani bado sijakata TAMAA japo sijioni kuwa hapo mbele mimi nitakuwa nani...!​
 
kiuchumi siwezi kusema nina tatizo kihivyo kwani nina jishughulisha... japo sina kipato kikubwa cha kumsaidia mwingine ila nina uwezo wa kula milo mitatu...!

kwakweli sielewi kwanini nimewaza hivyo...!​
Pole sana mkuu. Nimesoma maelezo yako na nadhani wewe unasumbuliwa na depression. Depression ni ugonjwa mbaya sana na uweza kumpata mtu yeyote japokuwa wewe inaonyesha unakuonea tangu ukiwa mdogo. Hii pengine ni kutokana na familia (kurithi) kwani kuna watu wako vulnerable kwa huu ugonjwa kuliko wengine. Kuna mtu mmoja nilisikia akihojiwa kuhusu huu ugonjwa akawa anasema aliupata na muda wote alikuwa anatamani kufa wakati aliwahi kuugua sana kansa na alikuwa anatamani kuendelea kuishi. Ugonjwa wa depression hufanya mtu kukata tamaa kabisa kabisa, kutokuwa na raha na hata vile vitu ambavyo alikuwa vinampa burudani anakuwa havipendi. Ushauri wangu kwako ni uende hospital inayoaminika uonane na dr bingwa umwelezee shida yako. Kuna dawa na therapies za kuweza kukuondoa kwenye hiyo hali na baadae ukawa na furaha kama zamani.
 
Wengi tu tulio na shida ila hatufikii hatua hii. Mtu wa Mungu, elewa unao wategemezi nyuma yako, utawatesa sana. Wewe una stress na hujawa resilient, umekata tamaa na huna solutions kwa changamoto ulizonazo. Be strong, be man enough to look for self courage. Ujue wanaokufa huwa hawarudi, so usitamani kufa as if it is a solution
nifanye nini...?
 
ni kweli ila ina bidi tuzoee tuu kwani mwisho wa siku kila nafsi lazima ionje Umauti 😭😭😭
Uamini Mungu, usiamini Mungu, Kifo kitatia Timu tu,hata hii misemo ya sijui "Nafsi itaonja Umauti" ni misemo ya kujipa Moyo tu kifo kinakuja tu.
 
Wala hata usihofu mkuu, hafi mtu hapq, unataka uende wap na maisha haya magumu umuachie nani? Uwakimbie Wanao wakabak kuteseka pekee yao ?

We kunywa maji mengi relax. Hufi wala nink japo chamoto unakiona ila kufa sio leo wala kesho. Nakuhakikishia mwaka huu unautoboa vyedi kabisaa.

JUst back to drawing board, plan and plan and plan.
i know that i must, I can and I will but how....?
 
Halafu kitu kingine. Umefanya vizuri sana kuweka kinachokusibu hadharani. Ujasiri tu wa kuelezea masaibu unayopitia bila kuona aibu ni njia nzuri sana ya kuanza safari mpya ya matumaini. Kutoa tatizo ulilonalo moyoni ni njia nzuri ya kupunguza ''mzigo'' (ugonjwa)
ndio wanadai healings is a process... hope nipo kwenye heal zone 😭😭😭
 
kwenye swala la michezo kwakweli mimi sio mwana michezo... labda jogging ila sina ushabiki kabisa wa mchezo wowote...!

na mimi ni aina ya wale watu ambao usipo nizoea siwezi kukuzoea...! hivyo kujichanganya na watu hii kwangu itakuwa mtihani sana... nita jaribu​
Nafikiri ni vizuri kufanya jata hiyo jogging kila siku, pia waone wataalam wa afya, ila hii dunia hakuna kukata tamaa, mapambano yaendelee tu! Pole sana.
 
Back
Top Bottom