Mimi ni kijana ambae nina mshukuru sana Mungu tokea nimezaliwa hadi hapa nilipofikia, watu wamenisaidia na bado wana nisaidia.
Kuna Muda huwa nina kufuru au kukana kutkukubaliana na uwepo wa Mungu😭 hii ni kutokana na asilimia kubwa ya matarajio yangu tokea nikiwa mdogo hayakuwahi kutimia.
Maisha yangu yamekuwa ya mitihani sana, kila nilichojaribu kuanzisha hakikuwahi kufika mwisho 😭😭😭 kwakweli nimeishi nikiwa na huzuni na furaha chache, mpaka hapa nilipofikia nina watoto wa 3 ambao ninawapenda mno.
Vipo vitu vichache ambavyo vinanitokea hivi sasa vinapelekea mimi kuhisi pengine siku zangu hapa Duniani zina karibia kuisha.
Hivi karibuni kichwa changu kimekuwa kizito mno kutoa maamuzi na ni kama kichwa kinanielemea, kimekuwa na maumivu fulani mithili ya kichwa kilicho toka kuuma!
Kwa taaluma mimi ni Mwandishi wa Habari ambaye napenda sana kusoma vitabu na asilimia kubwa ya vitu vingi nimejifunza kutokana na kusoma vitabu, lakini hivi karibuni nimepatwa na hali ya kutokuelewa kila ninacho kisoma.
Vitabu vyote ambavyo nilikuwa navipenda nikivisoma nahisi vinanichanganya, hata baadhi ya mada nilizokuwa nazipenda hapa JAMIIFORUMS nazo pia nimekuwa sizielewi.🥲
Nimepatwa na hofu hata nikikaa karibu na watu ninaowapenda sifurahii uwepo wao, nahisi kujitenga tu nikae peke yangu tu muda wote.
Ikitokea hamjaniona hewani mwezi mzima mfululizo mjue siku zangu niliziona kabisa zinahesabika hivyo malaika mtoa roho atakuwa amesha fanya yake.
Sifikirii kabisa kujiua kwa aina yoyote ile japo kwenye maisha yangu udogoni mwanangu nilishawahi mara 2 kujaribu kujiua. 😭
Mara ya kwanza nilijaribu kunywa sumu haikuniua, hapo nilikuwa na miaka 9 au 10, mwaka mmoja baadae nilijaribu kujinyonga bahati mbaya kile kitanzi pia hakikuondoka na maisha yangu.
Hivyo nichukue fursa hii kuwaaga ndugu zangu wana JAMIIFORUMS ambao tumeishi wote humu ndani kama familia. Kuna member humu nimesaidiana nao bila hata kufahamiana nao big up sana.
Kuna wengine tumekuwa ndugu na hata nje ya JAMIIFORUMS tumekuwa tukionana kwakweli sina cha kuwalipa.
Mimi niseme kitu hapa,
Jaribu kuwafikiria hao watoto watatu utakao waacha bila mtu (baba) umejaribu kuwaza Hilo...??!
Hiyo Hali inawatokea wengi na Wana survive mfano Mimi kichwani nilikua nipo vizuri Sana sijawai kufail na hata hii title ya udocta sio uchwara...
Niweke wazi kwenye hii miaka mi 5 nimekua busy Sana kwenye kompyuta 24/7 kwa siku 365*5 years no likizo no Sunday...
Nikajikuta ule uwezo wangu wa upeo na akili imepungua + loosing appetite ya mambo mengi..
Embu jaribu kwenda hospital mfano ocean roads, Moi, mloganzila kaangalie watu wanavyo pambania uhai wao (utakuja ku realize your wrong)
Jifunze ku """COUNT YOUR BLESSINGS""
NB.
Mwezi mmoja na wiki Sasa niliweka Uzi wangu wa ajari ya kugongwa na gari nikiwa Kama abiria kwenye BODABODA nikavunjika mguu wa kushoto..
Nili enda hospital this week nikafunguliwa P.O.P nikawekewa P.O.P nyingine pia nimeambiwa nianze mazoezi ya kukanyagia
Weight yangu hii 84 na kulala kitandani mwezi mzima bila kujigeuza
Ndio najifunza Tena kusimama na kutembea with CRUTCHES
MHANDO it's not easy Maumivu , pressure za kimaisha Ila mungu Ni mwema ndugu naamin with time ntaweza kusimama Tena na kutake care majukumu yangu..
Unaweza kuona wewe una shida wapo wenye tabu zaidi na shida zaidi YAKO
Mwenyezi Mungu atusaidie sanaa