Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Ila mi mkali,sio tunaanza project halafu ghafla unaniambia unaahirisha ni ngumu Bora ufe!walah nitakununulia Asali ya Tabora na tango mwenyewe ule uone Cha moto😜
🤣🤣🤣🤣🤣nimecheka kwa sauti hadi nimepaliwa... kitu kinacho nifanya niwe hivi nilivyo... ujue mimi ni mtu ninae penda kuona matokeo ya mambo ninayo fanya...!

hivyo siwezi kukuangusha...!​
 
NJOO TUKUVUTISHE BANGI NA POMBE KALI ILI UWE NA ROHO MBAYA YA KUJUA WEWE DUNIANI UTAKIWI KUWA MZEMBE .PAMBANA HAKUNA KUCHOKA.
UKIANZA KUJIKATIA TAMAA NA MWENYE CHAMA CHA CHAUMA ASEMEJE
🤣🤣🤣 kwakweli kichwa changu hakiwezi kuhimili mzigo wa kilevi chochote kuliko nitumie vilevi kwakweli bora ni rest in peace tu...!

 
🤣🤣🤣🤣🤣nimecheka kwa sauti hadi nimepaliwa... kitu kinacho nifanya niwe hivi nilivyo... ujue mimi ni mtu ninae penda kuona matokeo ya mambo ninayo fanya...!

hivyo siwezi kukuangusha...!​
🤣🤣🤣Bora umecheka,Dunia Ina vingi vya kufurahia....

Sawa,ntakuchek
 
Nachokushauri Prince Mhando kwa sasa kwa tatizo lako sio kuwa Muone therapist..

Na pia fanya Meditation Angalau Dakika 10 mpaka 15 kila siku kwa Siku hata 30 mpaka miezi sita kila asubuhi na Usiku
 
mimi mziki napenda ila kwaya... japo mimi ni muislam... kuna muda haswa kipindi hiki nyimbo nikisikiliza nahisi kama zinanipigia kelele...!

hivyo sio mpenzi san wa kelele...!
napenda kusikiliza motivation speaking haswa mahubiri... Mara kadhaa nilishawahi kufungulia radio zenye mahubiri hata ya mwamposa na mwakasege... nikisikilizaga mahubiri kidogo napata kaunafuu...!

japo kuna muda hata hayo mahubiri huwa siyaelewi...!​
Mkuu; nyimbo/muziki ni TIBA mubashara kwa mtu mwenye msongo wa mawazo. Mahubiri sio muziki na huenda baadhi ya mahubiri yanakuwa kama yanakushitaki rohoni mwako i.e yanakuongezea mawazo. Katika Uislam kuna kitu kinaitwa qaswida. Ukisikiliza na kuwaona waimbaji live itakusaidia sana. Ukiwa mpweke na ukajaribu kuimba wimbo wowote au kufuatilia wimbo unaoimbwa (video au audio clip) wakitumia vifaa vya mziki mwororo e.g. key board au kinanda kwa muda walau kwa dk 15 (robo saa) utagundua unakuwa relaxed sana. Kama unaweza kupata kifaa cha muziki jaribu kupoteza muda kwa kujifunza kukitumia. Lengo hapo huwa ni kuupa ubongo wako alternative work badala ya kufikiria, kuwaza na kuwazua, kujilaumu etc.
Kumbuka sote binadamu tuna changamoto nyingi na kwa kila mmoja zipo kwa aina tofauti lakini tunasonga mbele, tunapambana na maisha yanaendelea. Hakuna mtu aliyewahi kusema eti ameridhika na hali aliyonayo.
 
🤣🤣🤣 kwakweli kichwa changu hakiwezi kuhimili mzigo wa kilevi chochote kuliko nitumie vilevi kwakweli bora ni rest in peace tu...!

No,unatakiwa unywe 1 glass ya white sweet wine ni nzuri Kwa ubongo wako,inastimulate hormones za relaxation hicho kichwa hiyo misuli iliyokaza inalegea yoteee
 
Nipo dar es Salaam ila nafikiria kuhama tu huu mji
mkuu kama unaweza kuendesha pikipiki jikite hata kwenye bodaboda... huwezi kukosa elfu 10 kwa siku... na kupata pikipiki hapa mjini ni rahisi SANA...!

kama uwezi kuendesha nina weza nikakutafuta nikakufundisha ikawa ni zawadi yangu kwako🥲🤣🙏​
 
No,unatakiwa unywe 1 glass ya white sweet wine ni nzuri Kwa ubongo wako,inastimulate hormones za relaxation hicho kichwa hiyo misuli iliyokaza inalegea yoteee
sio chungu... au ngumu kama konyagi🤣🤣🤣
 
MT. :11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Mtwike Yesu mizigo yako yote Yeye ameahidi kutupumzisha na yale yote yatusumbuayo. Mimi najitolea kukuombea mkuu
 
Mimi ni kijana ambae nina mshukuru sana Mungu tokea nimezaliwa hadi hapa nilipofikia, watu wamenisaidia na bado wana nisaidia.

Kuna Muda huwa nina kufuru au kukana kutkukubaliana na uwepo wa Mungu😭 hii ni kutokana na asilimia kubwa ya matarajio yangu tokea nikiwa mdogo hayakuwahi kutimia.

Maisha yangu yamekuwa ya mitihani sana, kila nilichojaribu kuanzisha hakikuwahi kufika mwisho 😭😭😭 kwakweli nimeishi nikiwa na huzuni na furaha chache, mpaka hapa nilipofikia nina watoto wa 3 ambao ninawapenda mno.

Vipo vitu vichache ambavyo vinanitokea hivi sasa vinapelekea mimi kuhisi pengine siku zangu hapa Duniani zina karibia kuisha.

Hivi karibuni kichwa changu kimekuwa kizito mno kutoa maamuzi na ni kama kichwa kinanielemea, kimekuwa na maumivu fulani mithili ya kichwa kilicho toka kuuma!

Kwa taaluma mimi ni Mwandishi wa Habari ambaye napenda sana kusoma vitabu na asilimia kubwa ya vitu vingi nimejifunza kutokana na kusoma vitabu, lakini hivi karibuni nimepatwa na hali ya kutokuelewa kila ninacho kisoma.

Vitabu vyote ambavyo nilikuwa navipenda nikivisoma nahisi vinanichanganya, hata baadhi ya mada nilizokuwa nazipenda hapa JAMIIFORUMS nazo pia nimekuwa sizielewi.🥲

Nimepatwa na hofu hata nikikaa karibu na watu ninaowapenda sifurahii uwepo wao, nahisi kujitenga tu nikae peke yangu tu muda wote.

miaka ya nyuma nilikuwa na ndoto pengine za kuwa fulani nikawa naziishi ndoto hizo kwa kuzipambania kwa vitendo lakini siku bahatika kuishi maisha ya ndoto zangu.

siku hizi ni kama siioni future yangu kabisa... muda mwingine mpaka najiona kabisa kama napoteza tuu muda 😭😭😭😭

kama ninge kuwa simu hope ingekuwa kwenye flight mode ✈️🤣🤣🤣

Ikitokea hamjaniona hewani mwezi mzima mfululizo mjue siku zangu niliziona kabisa zinahesabika hivyo malaika mtoa roho atakuwa amesha fanya yake.

Sifikirii kabisa kujiua kwa aina yoyote ile japo kwenye maisha yangu udogoni mwanangu nilishawahi mara 2 kujaribu kujiua. 😭

Mara ya kwanza nilijaribu kunywa sumu haikuniua, hapo nilikuwa na miaka 9 au 10, mwaka mmoja baadae nilijaribu kujinyonga bahati mbaya kile kitanzi pia hakikuondoka na maisha yangu.

Hivyo nichukue fursa hii kuwaaga ndugu zangu wana JAMIIFORUMS ambao tumeishi wote humu ndani kama familia. Kuna member humu nimesaidiana nao bila hata kufahamiana nao big up sana.

Kuna wengine tumekuwa ndugu na hata nje ya JAMIIFORUMS tumekuwa tukionana kwakweli sina cha kuwalipa.​
Oya hauko peke yako, mimi ni kama wewe sema nimejizima data yaani nikipata ka sijapata na nisipopata ka nimepata tangu nimeanza kujitambua kua mimi si special kaliko maskini wengine, wagonjwa wengine na hata hao wakongo wanaouana kila siku why should i stress myself???

Sasa nimenenepa na kuzidi kua handsome
 
Kuna walimu wapo humu..
Hebu mcheck min -me
shukrani sana nitamtafuta.... niliwahi kutaka kujifunza... 2018 nilipata rafiki wa kikorea walikuwa pale mlalakuwa... mikocheni karibu na makao makuu ya jkt... yule mama alikuwa anapenda sana tukutane ila kipindi hicho nilikuwa busy nikawa simpi attention.
kingine nilikuwa naogopa yale mazingira sikuwa na mazoea na watu wanaoishi ushuani kwenye maappartment🤣🤣🤣

siku niliyo amua kumpa attention wiki 2 hizo akawa busy kushughulikia safari muda wake hapa tz ulikuwa umeisha... siku bahatika kupata hata introduction kutoka kwa huyo mama wa kikorea... alikuwa ananipenda sana.

napo alipo kuwa anaishi kila nilipo kuwa naenda nilikuwa nawakuta watu zaidi ya 10... wa mataifa mbali mbali... wakenya, wachina...!

wamekaa kwenye vigodoro kama mito ya makwisheni... najutia sana kulikosa hili darasa



alivyoondoka siku pata mawasiliano nae tena hadi leo...!​
 
Oya hauko peke yako, mimi ni kama wewe sema nimejizima data yaani nikipata ka sijapata na nisipopata ka nimepata tangu nimeanza kujitambua kua mimi si special kaliko maskini wengine, wagonjwa wengine na hata hao wakongo wanaouana kila siku why should i stress myself???

Sasa nimenenepa na kuzidi kua handsome
hongera sana Rafiki yangu... uliwezaje...!
 
Na Dunia ya Sasa inataka watu wa namna hii,yaani ni ubishi na kukaza mpaka kieleweke, yaani ni ubishi kama Muha,plan A ikifeli unahami plan B
Mm mkuu sahiv Niko plan C mana hii A na B zilifeli.. nkakimbilia Zanzibar kutafta maisha. Kuanza tu nikapata kazi ya ulinzi.. kila mwezi naenda kupigwa sindano sita hospitali mana malaria uhakika.

Hapo nimekimbia dar baad ya kuona ndugu wananiwangia. Mm hapa nilipo hata baba angu aliyenizaa Hana namba yangu na siwasiliani nae. Hao ndugu ndo kbisaaa mana nimeona ishara ya uchawi ulitukuka ukoo ule. POTELEA MBALI

Ipo siku tu
 
Back
Top Bottom