Nahitaji mtu mwenye wazo la Kibiashara ambalo litatusaidia kutengeneza pesa nyingi

Nahitaji mtu mwenye wazo la Kibiashara ambalo litatusaidia kutengeneza pesa nyingi

Je,unafahamu Tooth Pick Kwa Kiswahili inaitwa "Kimbaka",Kuna muda nawashangaa sana BAKITA na haya Majina Yao!


Any way


Wakuu nahitaji mtu yeyote mwenye wazo la Kibiashara ambalo liko tofauti na biashara ambazo zimezoeleka hapa Bongo!,Binafsi ninafanya biashara ya nafaka,pia Nina mashamba makubwa nalima,hivyo nikaona angalau tusaidiane na Vijana wenzangu ambao Wana mawazo na wameshindwa kuyafanyia kazi!

Nahitaji wazo hasa likiwa la kiteknolojia itakuwa poa sana!

Mtu aje na wazo na alitolee ufafanuzi namna wazo lake hilo litakavyoisaidia Tanzania au Afrika Mashariki kutatua changamoto,sitaki tuanze mbali Bali nataka tuanzie hapa hapa Tanzania Then tutafika Afrika Mashariki yote!

Binafsi nitatoa kiasi chote kitakachohitajika,pesa ipo ya kutosha na nimejipanga Kwa yeyote mwenye wazo zuri la biashara nzuri,maana kila nikaingalia naona wafanya biashara wengi ni kama wanaigana tu!

BIASHARA AMBAZO SIZITAKI

1.Biashara ya Nafaka (Hii naifanya na naijua nje ndani)

2.Biashara ya Usafiri
3.Biashara ya Viwanda vya Maji na Juisi
4.Biashara ya Mavazi
5.Biashara ya Nyumba au Real Estate (Hii naifanya na naifahamu nje ndani)
6.Biashara ya Wanyama (Ufugaji)

Akitokea mtu mwenye wazo la Biashara ya kiteknolojia nitafurahi zaidi!

Mtaji nilionao haupungui Tsh 500 milioni!

Kijana mwenye Idea hebu Lete wazo lako naamini tukaunganisha nguvu tutaweza!
kaka karibu kwenye fursa za madini ya dhahabu kuna teknolojia nzuri ya uchenjuaj wa dhahabu na kwa bei nafuu mm pia ni mtaalamu wa hizo teknolojia tuwasiliane kama utakua tayari napatikana kanda ya ziwa hasa geita 0659997074 au 0766927074
 
kaka karibu kwenye fursa za madini ya dhahabu kuna teknolojia nzuri ya uchenjuaj wa dhahabu na kwa bei nafuu mm pia ni mtaalamu wa hizo teknolojia tuwasiliane kama utakua tayari napatikana kanda ya ziwa hasa geita 0659997074 au 0766927074
Hio nasikia inabidi upite kwa Babu kwanza kuweka mambo sawa ukiingia kichwa kichwa lazima uliwe kichwa
 
Mkuu unaifaham mgeninani? Kule kuna sehemu ina mkomdo wa bahari unaitwa msende sema. Ule mkondo unakutoa mpaka kurasini mpaka posta bahari kwa bahari.

Ule mkondo tunaenda kuuchimba kuongeza kina alafu tunaweka kabandari kadogo kupitia kule watu kutoka mbagala kwenda mjini watumie boti zitakazokuwepo. Hakuna foleni... ishu ni Kibali tu!
kwa 500m?
 
Je,unafahamu Tooth Pick Kwa Kiswahili inaitwa "Kimbaka",Kuna muda nawashangaa sana BAKITA na haya Majina Yao!
Halafu hizo terms wanazifahamu wao tu kwenye kikundi chao na wamefanya siri yao, ila mtu akitaja kitu kwa kiingereza ndipo wanajitokeza kukosoa
 
Kwenye tasnia ya madini kunafursa nyingi sio kuchimba tu kama watu wanavyokariri ukisikia fursa ya madini anawaza kuchimba, ni sawa na tasnia ya kilimo sio lazima uwe mkulima unaweza ukauza pembejeo unaweza ukakodisha mashamba unaweza ukalangua mazao unaweza ukawa muuza mtaalam wa umwagiliaji unaweza ukawa mkodisha trekta za kulimia n.k
 
Back
Top Bottom