Wazo lako ni zuri sana,uwe unatania au hautanii watu humu jukwaani ila tunahitaji mada za namna hii kila siku ili watu waweze Kujikomboa na Umaskini wa kutisha.
Mimi nakushauri wekeza katika sekta ya Madini,binafsi nipo kwenye sekta hii na naona faida yake.
Sekta ya Madini inaweza kuifanya hiyo 500m kuwa 5B ndani ya miaka 2 hadi 3.
Wazo la Kwanza tafuta maeneo yenye Madini ya Kimkakati (Critical Minerals)omba Leseni ya utafiti mkubwa au Uchimbaji mdogo,wekeza kiasi kidogo cha kutoa sampuli za kupeleka maabara,majibu yakitoka vizuri na miamba ikaonekana tafuta wabia kutoka Korea,China, Australia au Canada.
Madini ya Kimkakati ni kama;
Copper
Rare Earth Elements
Lithium
Nickel
Graphite.
Wazo la pili tafuta sehemu nzuri yenye uzalishaji wa Dhahabu,nunua Karasha 1 au 2, tengeneza vat leaching plant, tengeneza na elution plant kazi yako itakuwa kukusanya makinikia yenye ppm nzuri na kuozesha kwenye plant zako.
Karibu Katavi