Rejea kichwa cha habari hapo juu, nahitaji mwanaume wa kunipa ujauzito kwa makubaliano kua huyo Mtoto atakua wa kwangu peke yangu,
Niliwahi kuja hapa na kutoa ushuhuda kua ninajihusisha na mapenzi ya jinsi moja, nilipata shauri mbali mbali wengi walinambia niende kanisani na wengine walinambia niolewe nizae,
Nimefata ushauri wa kuzaa lakini sikua peke yangu kwenye shauri hilo niliwashirikisha familia kua sitaki kuolewa lakini nataka kuzaa ilikua vuta nikuvute hatimae wakakubali,
Ninazaa sababu napenda watoto na umri unaniruhusu lakini sio nazaa ili nibadilike hivi nilivyo au niweke mwamvuli kwa jinsi nilivyo HAPANA,
SIFA ZA MWANAUME WA KUZAA NAE:
1. Awe na Akili Timamu
2. Awe tayari kupima Magonjwa yote ya Zinaa na mbegu zake kama nzima (tutaenda hospital pamoja)
3. Asiwe busy sana sababu nataka awe focused na kunipa ujauzito zile siku zote za upevushaji tutakazokutana
4. Asinipende na kutaka kunifanya girlfriend wake mara aje na sera za kutaka ndoa sijui kunibadilisha
5. Asiniombe Pesa kwenye jambo hili, kwani mimi nitakua nina safari ndefu ya kulea Mtoto siwezi kununua mbegu
6. Azingatie Mimba ikiingia mimi na yeye tunakata mawasiliano
7. Umri usizidi miaka 40 sitaki Mtu mwenye changamoto zozote za kiafya
SIFA ZANGU:
1. Nina Akili Timamu
2. Lesbian
3. Ready kua Mama
4. Umri miaka 28
5. Nipo Dar es salaam
NB: Sio lazima uwe wewe Mwana Jf unaweza kua na Ndugu au Rafiki ukatuunganisha.
Mawasiliano yawe PM.
Natanguliza Shukrani.