Pole kwa yote uliyopitia
Mariposa ni hatua nzuri uliyofikia.. Mimi nizidi tu kukuombea na kukutia moyo! Kuna baadhi ya taasisi wanauza mbegu hivyo unaweza kwenda huko!
Hofu yangu ni future ya mtoto atakayezaliwa..! Udogoni sio tatizo sana lakini kadiri atakavyokua hasa maisha ya shuleni akisikia wenzake wakisimulia kuhusu baba zao wakati yeye hana/hamjui anaweza kuathirika kisaikolojia na kutengeneza tatizo jipya
Kwa hatua ya kutaka kubeba mimba tena bila kupandikiza mbegu ni hatua nzuri sana kwakuwa inaweza kumaliza tatizo ulilonalo! Bila kutegemea wala kupanga mimba ikishatungwa hisia zinaweza kuanza kubadilika na kuanza kumhitaji mzazi mwenzako awe karibu nawe.. Mimba huja na mengi
Ikikutokea hivyo na huyo mzazi mwenza mtarajiwa akaku handle vema utakuwa umemaliza tatizo moja kwa moja.. Ila akizingua ndio basi tena
Yote kwa yote NAKUOMBEA