Nahitaji ushauri kwa mtaji wa 40 milionI

UTT inamaana gani, kwa sababu hizi terminology za kibiashara sizijui mda mwingi nimekaa shule za bweni nikisoma sayansi
UTT ni kampuni ama taasisi ya serikari Iko chini ya wizara ya fedha na mipango, inajihusisha na masuala ya uwekezaji wa pamoja, inafanya kazi kama mutual fund.

UTT inajihusisha na kuwekeza kwenye soko la HISA DSE na hati fungani za serikari.

UTT Ina mifuko mingi ya kuwekeza Kila mfuko una taratibu zake,ila mfuko wa bond fund naona ndio mzuri sera ya uwekazaji kwa asilimia kubwa pesa zenu zinawekezwa kwenye hati fungani za serikari za muda mrefu.

Ukitaka maelezo kwa kina unaweza Kuni DM maana hata Mimi nimeweka za.
 
Kwa maisha ya kiuchuo chuo ni return nzuri kwake kupata laki 4 kila mwezi wakati huo huo mtaji wake unakuwa salama.

Nafikiri apate elimu zaidi ya UTT imsaidie kufanya maamuzi
 
Pamoja sana bro
 
Itatekegemea na thamani ya soko wakati huu, but muhimu akaenda kupata abcd kwenye ofisi zao za dsm na kwingineko.

Ila UTT inaweza kuwa sehemu sahihi kwake kulinda mtaji wake kuliko kwenye biashara ya daladala
Aje nimuelekeze Hadi aive! asipolizika nitampa mawasiliano ya mtumishi wa UTT aelekezwe vizuri.
 
Ukiweka UTT utapata 400,000 kwa mwezi. Biashara gani utaingiza hiyo pesa kwa mwezi bila usumbufu
 
Ukiweka UTT utapata 400,000 kwa mwezi. Biashara gani utaingiza hiyo pesa kwa mwezi bila usumbufu
Hili nalo neno maana bishara usumbufu mtupu.
So ukiweka mil 20 unapata laki mbili
 
Wazo zuri Sana umempatia,na asisahau na bei ya madawa,Ila kama angeanza na ng'ombe 40 kwanza...
Sahihi kabisa achague mwenyewe aidha azifuge Bank au afanye huo mradi mpaka akimaliza chuo ngoma inakimbilia 100 milion na ikikata hela yake mimi namlipa[emoji3][emoji3][emoji2][emoji23]
 
UTT ni mfuko wa uwekezaji ambao unaweza kuwekeza kupitia kununua hisa na kuuza.

Unaweza kufika ofisini kwao ili kupata taarifa sahihi
Hivi haiwezekani kujisajili online na kuanza kununua vioande bila kufika ofisini kwao?
 
Inamaana kuna muda zinakushaka thamani??
Ni kama biashara ya dollar kupanda na kushuka Mkuu, but vyema upate taarifa sahihi kwa wahusika.

Kila la kheri kwenye uwekezaji wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…