nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,106
- 12,916
Kijana...kama una mzuka na biashara ya magari achana na mambo ya shule.Habari za muda huu, Mimi ni kijana wa miaka 20, hivi karibuni ninatarajia kupokea 40mil, je ni biashara gani ya uhakika naweza kuifanya yenye pesa..Mimi binafsi sipendelei maduka kabisa Wala sifikirii, Ila nilikuwa nawaza kununua coaster hata kama used kwa mtu, nimpe mtu afanyie kazi kwa siku iwe inakuja atleats 70k huku nikiendelea na chuo...
Nawakaribisha mnipe mawazo yenu. Asante
Shule uliyo nayo yatosha kabisa kwa nchi hii.
Kama unataka Coaster nunua 14B,halafu kaa mlangoni mwenyewe,usisubiri kuletewa hesabu.
Vinginevyo
Nunua DCM ni bei nafuu, linatengenezeka...Chukua route either ya Msumi au Mpigi magohe,kaa mlangoni mwenyewe,
pesa utaiona,
Tafuta dereva mtu mzima ishi nae vizuri,kla jioni mtoe kwa kadiri ya imani yako...
Kwa wastani njia hii baada ya kutoa gharama zote unabakiwa na 230,000/=mpaka 260,000/=
Pale Mbezi kuna Branch ya CRDB jitahidi ku deposit 200,000 daily
Kwa maana hiyo kwa mwezi utakuwa na 6,000,000/=........kwa nchi hii hakuna mtu anaweza kukulipa pesa hiyo kwa mwezi(ndo maana nakujuza usipoteze muda wako shule)
Ndani ya miezi kumi utakuwa na milioni sitini,sasa hapa CRDB wanakudhamini basi jipya,TATA,,,,,na hapo baada ya miaka miwili utakuja nishukuru kama fulani na fulani.
TAHADHARI.
Vishawishi,Pombe,fegi,mademu ni mianya na milango ya umasikini katika kazi hii.
Wengi wanalalamika biashara hailipi sababu ni hizo.
1.Komaa mwenyewe kudaka nauli.
2.Zingatia service na matengenezo
3.Penda kazi yako usafi ,boresha mazingira ya kazi PIMP chombo chako.