Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Ukiwa mtu wa familiar au umelelewa kwenye maadili haya mambo huwa ni magumu kufanya maamuzi sababu ya watoto.
Tofauti na ukitokea single family
 
Hahaha Ila Comment za Humu Nimecheka Sana!
Wengine Badala ya kushauri wanasimanga🤣🤣

Mdogo wangu!
Nisilize Maisha yanatia Hofu sana, Ila Moyo ni hofu zaidi ya Hayo maisha...

Kama moyo wako bado una machungu na Mkeo hakikisha Unakaa naye mbali uwezevyo kwa muda jipe muda wa Kupona maana nimeona Umeandika mahali kwamba licha ya maumivu una hasira..

Sasa nisikilize Usikae Naye nyumba moja ukiwa bado unajiponya Hicho kidonda..

Stress +Hasira+ Deppresion Sio Combinantion nzuri Maana kitakachoendelea Unaweza ukamdhuru na kusababisha matatizo makubwa sana..

Nimeona Umeandika kuwa umetoa Talaka 2 so obvious wewe ni mwislamu..

Eda Ina miezi minne na nusu tumia Eda Kufikiria maamuzi yako na Kujiponya mwenyewe..
Na kama utaona kuna haja ya Kumrudia Fanya hivyo..

Asante!
Point of correction dokta, eda ya kufiwa ndio miezi minne na siku 10.
 
Ukiwa mtu wa familiar au umelelewa kwenye maadili haya mambo huwa ni magumu kufanya maamuzi sababu ya watoto.
Tofauti na ukitokea single family
bonge 1 la point... nawasifu wale wanaowezaga kupiga chini wife mpk watoto
 
Kabla hujafanya maamuz yoyote jiulize haya maswali.
Wewe binafs hujawah kumsaliti?
Watoto wako watalelewaje bila mama yao.
Mazingira ya mbali ndio chanzo cha yote hayo?
Nikimsamehe nitapungukiwa na nini.
Maamuz yoyote unayochukua yalenge watoto sio ubinafs wenu.
Mwisho, bila umuhim. Biblia inasema aliwazalo mtu ndilo humtokea. Msiishi kwa kushika simu zenu au hayo ma meditation just amin mkeo unamuamin muombee maisha yaende.
Kuchepuka ni tabia ya mtu umbali una nafasi asilimia kumi kuchangia usaliti.
Unaweza ishi nae kila siku anakula dozi na Bado akauchafua nje mwili wake akuletee nuksi ndani.
Usaliti ni ishu ya kujitambua mtu anaejitambua huwezi kuta anajichafua nje
 
Maamuzi yoyote utakayofanya yana athari kubwa mbele. Chagua ambalo unaona ni rahisi moyo kulibeba. Sometimes ukifikiria sana kuhusu hali ya watoto itakuwaje malezi ya bila wazazi wote endapo mkiachana matokeo yake wanakupoteza wewe. Sio wakati wote ufikirie watoto itakuwaje? Fikiria wakikupoteza itakuwaje. Stress and depression vinaua ndugu yangu
 
Habari wanajamvi naandika Bango Hili nikiwa sijui nini nifanye na nikiwa nimechanganyikiwa Kwa Yaliyotokea na sielewi hili.wala lile.

IKo hivi Mimi ni Kijana mwenye Umri wa Miaka 46, Nilikuwa nina Mke wangu ana Umri wa Miaka 34 Tulikuwa Tunaishi naye lakini kutokana na mambo Ya kimajukumu Ukabidi Niende Dodoma kama miezi mitano au sita Ilopita Na yeye Nikamuacha Tabora.

Tulikuwa tunawasiliana Vizuri tu na kuna kipindi Ilitokea Shida kidogo mwezi mmoja baada ya mimi Kuondoka, Kulitokea Hitilafu Kwenye Ujenzi tunaofanya hapo Kahama kwakuwa nilikuwa mbali na yeye Ni mfanyakazi wa Serkali nikamuomba akakope Pesa Kiasi halafu nitakuja Kufidishia (Ndiyo Tinavyofanya siku zote).

Kama Jukumu likiwa la kwangu na yeye akiwa na means ya kufanya bhasi anafanya Mimi naandika deni.

Kwakuwa Benki walikuwa wanachelewa Ikabidi aende kwa wanaoacha Kadi akafanikiwa na kupata pesa na kila mwezi akawa anakatwa pesa zake na alikuwa anafata kiasi kinachobaki hapo ofisini..

Wiki Moja kabla nikawa Nahisi Kama Kuna uwezekano Mke wanhu ananisaliti (Mimi ni mtu wa Kufanya Sana Meditation Hivyo Hisia zikinijia bhasi lazma nizifanyie Meditation Kwa siku angalau mbili na huwa napewa clear Picture)..

Kipindi nafanya Meditation nikawa naona kabisa Mke wangu ananisaliti sasa Baada ya miezi minne kuondoka huko Nikawa namuuliza Huko ni salama mbona kama kuna kitu kibaya unafanya jibu lake hakuna shida yoyote.

Guyz huyo jamaa wa Microfinace simjui na Sijakutana naye ila kuna kitu kikawa kina niambia nimuulize Wife na nimkazanie kuhusu Huyo mtu kwa nguvu mpaka aseme ikibidi Nitumie uongo wowote kama mwanaume..

Nilifanikiwa Kimlazimisha na kumuuliza hatimaye akaamua kugunguka kuwa yule Jamaa wa Microfinace alimbaka Yeye alipokuwa Ofisini kwake Kuchukua Kiasi cha Pesa Kilichobaki na wala haikuwa dhamiri yake.

Nikamuiliza Umereport tukio hilo akajibu "Hapana"
Nikamuuliza Ulipiga kelele akajibu "Hapana maana nisingesikika wala watu wasingeniamini"

Nikawaza sana huyu Wife nimezaa Naye watoto watatu..
Na anassma alimbaka Miezi minne Exactly tangu nilivyoondka ila nisingemuuliza Nadhani ingeendelea Kuwa story ya siri yake..

Ninawaza kumpa Talaka Tatu ila bado nahofu na watoto wangu Nimempa Talaka 2 ila akili yangu bado inaona nimeumizwa sana nastahili kufanya kitu ila bado moyo unavuja damu nifanye nini??

Naombeni wan JF mnishauri Nifanye Nini maana naumia Sana.

Na kwa maelezo yake Bado siamini kabisa.

Naombeni sana Ushauri maana ametishia Kujiua endapo sitamrejea
Mkuu kwa umri wako uliofikia sio umri wa kuangaika tena kuanza kutafuta wachumba wa kuoa tena ukizingatia mko na familia ya watoto watatu.
Hapo ni kumsamehe tu,maana kwa maelezo yako ni kwamba mnaishi sehemu tofauti kwa muda wa miezi 6 hapo lazima ndoa iingie dosari mwanamke lazima ataingiwa vishawishi vya watu wabaya hiyo ni nature haikwepeki ndugu na hata ukioa mwingine ukimuacha mbali pia utasalitiwa tena.
Hapo Suluhu ni kuwa naye karibu na mkeo either wewe uchukue uhamisho au yeye achukue uhamisho mkae pamoja japokuwa mwanamke huwa halindwi kama ni tabia yake ya tangu zamani hata ukiwa karibu pia ana uwezo wa kukusaliti.
Najua hili jambo linakuumiza moyo na limekupa stress lakini pia ukimuacha ukaanzisha familia na mke mwingine stress zitaongezeka zaidi kwa kuwa na familia mbili tofauti na stress zake huwa ni za kudumu.
Halafu kwa hesabu za haraka haraka nimegundua huyo mkeo anakupenda ila ilitokea tu ameshawishika akaingia mtegoni si unajua wanaume huwa tuna mbinu nyingi tukimtaka mwanamke,sababu ya kukwambia hivyo ni kwamba mwanamke asiyekupenda baada ya kumshika ugoni huwa hajutii kwa kilichotokea na wala huwa hashtuki ukimtishia talaka atakujibu tu potelea mbali.
Na kitu kingine huyo mwanamke alikuwa anakuheshimu sana ndio maana umembana akakwambia ukweli kilichotokea ila kama ni mwanamke aliyepinda hawezi kukwambia hata umfanye nini atagoma tu na kuukataa ukweli maana haukuwa na ushahidi wowote.
Nimejitahidi kuandika comment ndefu hivi maana nimeguswa na nawaonea huruma watoto wako watakavyoteseka pindi utakapochukua maamuzi ambayo si sahihi.
 
Kuchepuka ni tabia ya mtu umbali una nafasi asilimia kumi kuchangia usaliti.
Unaweza ishi nae kila siku anakula dozi na Bado akauchafua nje mwili wake akuletee nuksi ndani.
Usaliti ni ishu ya kujitambua mtu anaejitambua huwezi kuta anajichafua nje
Ni kweli lakin kila mtu ana wakat wake mbaya wa kufanya maamuz mabaya so kuwa karibu na mkeo kuepusha madhara
 
Options
1.Kama kweli mkeo amenyanduliwa na huyo jamaa ameambie halipi hiyo balance iliyobaki.

2.Chukua mkeo na hama naye mkoa,nendeni mkapime afya zenu mkiwa safi endeleeni na maisha yenu.
Ila mpe ONYO kubwa akirudia atakula kwake.
Swali la kizushi je wewe ulimkuta bikra huyo mkeo?
Pole sana mzee wa makamo.(usipende kujiita kijana wewe tayari ni maji ya jioni)
Yeah kwenye ishu ya kuhama naye ni jambo la muhimu sana vinginevyo jamaa wa microfinance ataendelea kumsumbua na kumkumbushia jinsi walivyoenjoy siku ya kwanza hatoweza kumkwepa.
 
Alivyobakwa hajajiua na amekaa kimya ila kupewa talaka eti anataka kujiua anakuzingua tu huyo.
 
Ni kweli lakin kila mtu ana wakat wake mbaya wa kufanya maamuz mabaya so kuwa karibu na mkeo kuepusha madhara
Labda umfunge kamba.
Kumbuka wapo ma ex wake wanamjua Hadi ufunguni
 
Wanyamwezi mwadila mpola....kwangu msaliti ni teke moja mpaka nje ya fence....usaliti ni tabia hawez acha ila atatafuta mbinu mpya ya kuliwa!!watoto isiwe kigezo cha wewe kuish na msaliti,lakin kama na wew una mchepuko basi msamehe hapa aggregate ni 3-3....
 
Hivi unakubali vipi kuwa ulisaliti na hujakutwa red handed?
Huyo mwanamke alirogwa au? Poleee yenu.
 
Point of correction dokta, eda ya kufiwa ndio miezi minne na siku 10.
Namimi Ni.eandika Miezi Minne Na nusu, Nimekosea?
Ok Ngoja Nikueleweshe kwanini Nimesema Miezi Minne na Nusu..

Mwezi unawiki 4 Na Wiki Mbili ni Nusu Ya mwezi..
Kwanyo Siku 10 ni Wiki mbili kasoro Siku 4..

Kwahyo kuandika Miezi Minne na Nusu Niko sawa na Kuandika Miezi Minne na siku 14 au Miezi minne na siko 10 Umenielewa?
 
Back
Top Bottom