Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Ukiwa mtu wa familiar au umelelewa kwenye maadili haya mambo huwa ni magumu kufanya maamuzi sababu ya watoto.
Tofauti na ukitokea single family
 
Point of correction dokta, eda ya kufiwa ndio miezi minne na siku 10.
 
Ukiwa mtu wa familiar au umelelewa kwenye maadili haya mambo huwa ni magumu kufanya maamuzi sababu ya watoto.
Tofauti na ukitokea single family
bonge 1 la point... nawasifu wale wanaowezaga kupiga chini wife mpk watoto
 
Kuchepuka ni tabia ya mtu umbali una nafasi asilimia kumi kuchangia usaliti.
Unaweza ishi nae kila siku anakula dozi na Bado akauchafua nje mwili wake akuletee nuksi ndani.
Usaliti ni ishu ya kujitambua mtu anaejitambua huwezi kuta anajichafua nje
 
Maamuzi yoyote utakayofanya yana athari kubwa mbele. Chagua ambalo unaona ni rahisi moyo kulibeba. Sometimes ukifikiria sana kuhusu hali ya watoto itakuwaje malezi ya bila wazazi wote endapo mkiachana matokeo yake wanakupoteza wewe. Sio wakati wote ufikirie watoto itakuwaje? Fikiria wakikupoteza itakuwaje. Stress and depression vinaua ndugu yangu
 
Mkuu kwa umri wako uliofikia sio umri wa kuangaika tena kuanza kutafuta wachumba wa kuoa tena ukizingatia mko na familia ya watoto watatu.
Hapo ni kumsamehe tu,maana kwa maelezo yako ni kwamba mnaishi sehemu tofauti kwa muda wa miezi 6 hapo lazima ndoa iingie dosari mwanamke lazima ataingiwa vishawishi vya watu wabaya hiyo ni nature haikwepeki ndugu na hata ukioa mwingine ukimuacha mbali pia utasalitiwa tena.
Hapo Suluhu ni kuwa naye karibu na mkeo either wewe uchukue uhamisho au yeye achukue uhamisho mkae pamoja japokuwa mwanamke huwa halindwi kama ni tabia yake ya tangu zamani hata ukiwa karibu pia ana uwezo wa kukusaliti.
Najua hili jambo linakuumiza moyo na limekupa stress lakini pia ukimuacha ukaanzisha familia na mke mwingine stress zitaongezeka zaidi kwa kuwa na familia mbili tofauti na stress zake huwa ni za kudumu.
Halafu kwa hesabu za haraka haraka nimegundua huyo mkeo anakupenda ila ilitokea tu ameshawishika akaingia mtegoni si unajua wanaume huwa tuna mbinu nyingi tukimtaka mwanamke,sababu ya kukwambia hivyo ni kwamba mwanamke asiyekupenda baada ya kumshika ugoni huwa hajutii kwa kilichotokea na wala huwa hashtuki ukimtishia talaka atakujibu tu potelea mbali.
Na kitu kingine huyo mwanamke alikuwa anakuheshimu sana ndio maana umembana akakwambia ukweli kilichotokea ila kama ni mwanamke aliyepinda hawezi kukwambia hata umfanye nini atagoma tu na kuukataa ukweli maana haukuwa na ushahidi wowote.
Nimejitahidi kuandika comment ndefu hivi maana nimeguswa na nawaonea huruma watoto wako watakavyoteseka pindi utakapochukua maamuzi ambayo si sahihi.
 
Kuchepuka ni tabia ya mtu umbali una nafasi asilimia kumi kuchangia usaliti.
Unaweza ishi nae kila siku anakula dozi na Bado akauchafua nje mwili wake akuletee nuksi ndani.
Usaliti ni ishu ya kujitambua mtu anaejitambua huwezi kuta anajichafua nje
Ni kweli lakin kila mtu ana wakat wake mbaya wa kufanya maamuz mabaya so kuwa karibu na mkeo kuepusha madhara
 
Yeah kwenye ishu ya kuhama naye ni jambo la muhimu sana vinginevyo jamaa wa microfinance ataendelea kumsumbua na kumkumbushia jinsi walivyoenjoy siku ya kwanza hatoweza kumkwepa.
 
Alivyobakwa hajajiua na amekaa kimya ila kupewa talaka eti anataka kujiua anakuzingua tu huyo.
 
Ni kweli lakin kila mtu ana wakat wake mbaya wa kufanya maamuz mabaya so kuwa karibu na mkeo kuepusha madhara
Labda umfunge kamba.
Kumbuka wapo ma ex wake wanamjua Hadi ufunguni
 
Wanyamwezi mwadila mpola....kwangu msaliti ni teke moja mpaka nje ya fence....usaliti ni tabia hawez acha ila atatafuta mbinu mpya ya kuliwa!!watoto isiwe kigezo cha wewe kuish na msaliti,lakin kama na wew una mchepuko basi msamehe hapa aggregate ni 3-3....
 
Hivi unakubali vipi kuwa ulisaliti na hujakutwa red handed?
Huyo mwanamke alirogwa au? Poleee yenu.
 
Point of correction dokta, eda ya kufiwa ndio miezi minne na siku 10.
Namimi Ni.eandika Miezi Minne Na nusu, Nimekosea?
Ok Ngoja Nikueleweshe kwanini Nimesema Miezi Minne na Nusu..

Mwezi unawiki 4 Na Wiki Mbili ni Nusu Ya mwezi..
Kwanyo Siku 10 ni Wiki mbili kasoro Siku 4..

Kwahyo kuandika Miezi Minne na Nusu Niko sawa na Kuandika Miezi Minne na siku 14 au Miezi minne na siko 10 Umenielewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…